Wednesday, 24 December 2008


HIVI TUNA UHABA MKUBWA SANA WA WATENDAJI NA VIONGOZI WAZURI HADI TUENDELEE KUWANG'ANG'ANIA HATA WALE WALIOKWISHAFANYA MADUDU HUKO NYUMA?KUNA STORI KATIKA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU ALIYEKUWA MKURUGENZI WA MANISPAA YA TEMEKE,JOHN LUBUVA,AMBAYE ALISIMAMISHWA KAZI KUTOKANA NA SAKATA LA UBOMOAJI NYUMBA HUKO TABATA DAMPO.CHA AJABU ETI KWA SASA NI MKURUGENZI WA MANISPAA YA SHINYANGA VIJIJINI.HII SIO TU DHARAU KWA WAKAZI WA MANISPAA HIYO ILIYOLETEWA "MTENDAJI MPYA" BALI PIA NI MUENDELEZO WA HAKA KAMTINDO KA KUNG'ANG'ANIA VIONGOZI WALIOPUNGUKIWA NA SIFA.JE,KUMREJESHA KIONGOZI HUYO MADARAKANI HAKUWEZI KUWA KICHOCHEO KWA VIONGOZI WENGINE KUREJEA MADUDU KAMA YA MWENZAO ALIYEBORONGA,AKAPEWA MAPUMZIKO MAFUPI KISHA AKAREJESHWA MADARAKANI?TANGU LINI ADHABU KWA MAKOSA YA UONGOZI IKAWA KUHAMISHWA KUTOKA TEMEKE NA KUPELEKWA SHINYANGA?HIVI AKILIKOROGA TENA HUKO SHINYANGA ITAKUWAJE?THIS IS NOT ONLY UNFAIR BUT INAKERA NA KUCHUKIZA PIA.


Serikali imeridhia Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA- JKT), liongezewe nguvu kiutendaji na kuwa kampuni ya ulinzi itakayotoa ushindani kwa makampuni binafsi ya ulinzi yanayotoa huduma hiyo kwa kiwango kisichoridhisha. 

Kwa sasa SUMA, imejikita katika ujenzi wa nyumba za serikali, barabara na kutengeneza samani. 

Uamuzi wa JKT kuwa na kampuni ya ulinzi, una lengo la kuajiri vijana wanaohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi. 

Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Kanali Ayoub Mwakang’ata, alitoa taarifa hiyo jana wakati akihutubia katika kilele cha mafunzo ya Operesheni Uadilifu yaliyokuwa yakifanyika katika Kambi ya 835 JKT Mgambo wilayani Handeni. 

Katika taarifa yake alisema kuwa serikali kwa kushirikiana na Jeshi hilo wameridhia kampuni hiyo kuanza kazi rasmi mapema mwakani. 

Kampuni hiyo imepanga kuboresha huduma za ulinzi kwa kuajiri askari waliopitia Jeshi hilo pekee na kuwasambaza katika maeneo mbalimbali nchini kote wakichuana na makampuni mengine yaliyoko sasa, lakini bila ya kuathiri utendaji wao. 

``Suma JKT itakuwa kampuni ya ulinzi rasmi kuanzia mwakani na itachukua vijana waliohitimu mafunzo ya awali ya kijeshi na si askari wa akiba wa mgambo, mpango huu ni maalumu kwa ajili ya kuwasaidia vijana kama hawa kupata ajira za uhakika baada ya kuhitimu mafunzo haya… na ukweli ni kwamba hatua hii itakuwa ni changamoto kwa vijana wengi wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kujiunga JKT,``alisema. 

Awali Ofisa Utumishi wa JKT Makao Makuu, Meja Elvis Massawe alipohojiwa kuhusiana na hatua iliyofikiwa hadi sasa na Kitengo hicho cha SUMA alikiri kwamba Ofisi hiyo imeshapokea maombi zaidi ya robo tatu ya vijana waliohitimu katika Jeshi hilo nchi nzima wakisubiri kuajiriwa rasmi. 

Kwa mujibu wa Ofisa huyo ni kwamba Kampuni hiyo mbadala ya ulinzi itachukua askari wa rika mbalimbali bila kujali umri wao na kwamba bado jeshi hilo linapokea maombi ya yawanaotaka kujiunga na kampuni hiyo...

CHANZO: Nipashe

SINA HAKIKA KAMA UMEFANYIKA UTAFITI WA KUTOSHA KUHUSIANA NA MAAMUZI HAYA MAZITO (IT'S PERSONAL KWANI NAMI NI MMOJA KATI YA WALIOPITIA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA MIAKA YA 90).NAAMINI TATIZO KUBWA LINALOKWAZWA KUIREJESHA JKT KUWA KAMA YA ENZI HIZO NI PAMOJA NA MIPANGO DHAIFU ISIYOANGALIA MBALI.SIJUI BABA WA TAIFA HUKO ALIKO AKISIKIA JKT INATAKA KUGEUZWA KAMPUNI YA ULINZI ATAJISIKIAJE LAKINI KWA HAKIKA NI JAMBO LINALOTIA SHAKA SANA HASA IKIAZINGATIWA KWAMBA JESHI SIO TAASISI YA BIASHARA.NI VIGUMU KUTUAMINISHA KWAMBA JKT ITAWEZA KUHIMILI USHINDANI WA KIBIASHARA KATIKA SEKTA YA ULINZI BINAFSI ILHALI UFANISI WA VITENGO VYA KIBIASHARA KATIKA JESHI HILO (KWA MFANO SUMA NA MRADI WA KOKOTO KUNDUCHI) WENYE MUSHKELI.

JKT INGEWEZA KUWA KITUO CHA KUZALISHA AJIRA KWENYE SEKTA YA KILIMO NA HATA UJASIRIAMALI IWAPO KUTAKUWA NA MAANDALIZI SAHIHI.MSISITIZO WA JKT NI KUWAANDAA VIJANA KULITUMIKIA TAIFA LAO KWA UZALENDO NA SIO KWENDA KULINDA MALI ZA WATU (INCLUDING MAFISADI).HATA KAMA WAZO LA BIASHARA YA ULINZI NI ZURI BADO KUNA WASIWASI KUHUSU MASLAHI YA VIJANA HAO,JAMBO AMBALO LISIPOANGALIWA KWA MAKINI LINAWEZA KUZAA MAJAMBAZI BADALA YA WALINZI BINAFSI.ULINZI NI TAALUMA NYETI NA ISIPOTENGENEZEWA SERA MAKINI INAWEZA KUZAA MAYHEM KATIKA JAMII.


Tuesday, 23 December 2008

SAFARI YA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI BADO NI NDEFU NA YENYE VIKWAZO LUKUKI.KATIBA NA SHERIA ZINAZOWATOFAUTISHA VIONGOZI NA WANANCHI WA KAWAIDA ZINATUMIKA KAMA KINGA DHIDI YA MATENDO AMBAYO KWA NAMNA MOJA AU NYINGINE YANAHUSU UVUNJAJI WA SHERIA.PIA KINGA HIZO ZINAWEZA KUWA KICHOCHEO KIZURI KWA VIONGOZI WAPYA KWANI KAMA WATANGULIZI HAWAKUCHUKULIWA HATUA WALIPOBORONGA (KWA VILE WANA KINGA) THEN KWANINI WALIOPO MADARAKANI WAOGOPE KUBORONGA?HIVI KAMA WENZETU HUKO MAREKANI WANADIRIKI KUMHOJI RAIS MTEULE,IWEJE VIGUMU KWETU KUMHOJI RAIS MSTAAFU?ANYWAY,SOMA STORI HII HAPO CHINI KISHA TUENDELEE NA MJADALA WETU
Rais Mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, hachunguzwi kwa kosa au tuhuma yoyote ya jinai, imeelezwa. Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), katika taarifa yake kwa umma iliyotolewa Dar es Salaam jana, ilisema uvumi kuwa Rais huyo mstaafu anachunguzwa na vyombo vya dola ikiwamo taasisi hiyo, hauna ukweli wowote. 

Tamko la taasisi hiyo limekuja huku kukiwa na uvumi katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa kiongozi huyo anachunguzwa na Takukuru, kutokana na vitendo vingi vya ufisadi vinavyodaiwa kufanywa wakati wa uongozi wake. 

Tayari mawaziri wawili Basil Mramba na Daniel Yona waliowahi kushika nyadhifa nyeti katika Serikali ya Awamu ya Tatu ukiwamo uwaziri wa Fedha, wameshafikishwa mahakamani kwa tuhuma za kutumia madaraka yao vibaya na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7. 

Lakini pia baadhi ya watuhumiwa katika kesi za kuchota mabilioni ya fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) katika Benki Kuu (BoT), ambao wamefikishwa mahakamani, wanadaiwa kufanya wizi huo kati ya mwaka 2004 na 2005 kipindi ambacho Rais Mkapa alikuwa madarakani. 

Ofisa Uhusiano wa Takukuru, Doreen Kipwani alisema jana kuwa, taasisi yake haina uwezo wa kumchunguza kiongozi huyo kutokana na Katiba ya nchi kutotoa nafasi hiyo katika Ibara ya 46 (3) ya Katiba ya Tanzania. Kapwani alieleza kuwa taasisi yake inaheshimu Katiba na ina wajibu wa kuilinda na kuheshimu matakwa hayo ya Katiba. 

“Takukuru inawafahamisha wananchi kwamba uvumi huu hauna ukweli wowote, hatumchunguzi kiongozi huyu kwa kosa au tuhuma yoyote ya kijinai,” alisema. “Ni kwa msingi huu, Takukuru imeona ni vyema kuwafahamisha wananchi ukweli dhidi ya uvumi huu. 

Tukumbuke wakati wote kwamba taifa letu lina Katiba ya Nchi ambayo imeweka misingi mikuu ya kuendesha nchi yetu, haki na wajibu wa kila Mtanzania. Katiba kama sheria mama imeweka pia mipaka katika kushughulikia mambo mbalimbali ya nchi na kwa mantiki hii, haina budi kuheshimiwa wakati wote.” 

Kifungu hicho cha Katiba kinaeleza kuwa “Ni marufuku kumshitaki au kufungua mahakamani shauri lolote la jinai au la kumdai mtu aliyekuwa anashika madaraka ya Rais baada ya kuacha madaraka hayo kutokana na jambo lolote alilofanya yeye kama Rais wakati alipokuwa bado anashika madaraka ya Rais kwa mujibu wa Katiba hii.” 

Kapwani alisisitiza kuwa Takukuru itaendelea kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba na sheria ya nchi na sio vinginevyo. Katika siku za karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vinaripoti kuwa Mkapa anachunguzwa na Takukuru licha ya kuwa ana kinga ya kutoshitakiwa. 

Vyombo hivyo vimekuwa vikimwandama kwa madai kuwa ufisadi mkubwa umefanyika katika kipindi ambacho alikuwa madarakani. Watu wenye mtazamo huo wamekuwa wanataka kiongozi huyo aondolewe kinga na afikishwe mahakamani kujibu tuhuma mbalimbali za ufisadi. 

Wiki hii, Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo alieleza kusudio la kuwasilisha hoja binafsi katika kikao kijacho cha Bunge kuomba kifungu kinacholinda marais wastaafu kutoshitakiwa kirekebishwe. Mkapa anatajwa katika tuhuma kuhusu ununuzi wa ndege ya Rais, ununuzi wa rada, wizi wa mabilioni ya EPA, uuzaji wa nyumba za serikali, mikataba yenye utata kama ya NetGroup, Alex Stewart na ubinafsishaji wa mgodi wa Kiwira.
CHANZO: Habari Leo

UFAFANUZI HUO WA TAKUKURU HAUWEZI KUZIMA KELELE ZA WANAOTAKA KUMUONA TUHUMA DHIDI YA MKAPA ZINATHIBITISHWA KWENYE VYOMBO VYA SHERIA.PAMOJA NA KUILINDA NA KUIHESHIMU KATIBA,TAKUKURU INA WAJIBU WA KULINDA NA KUTETEA RASLIMALI ZA WATANZANI ZINAZOFUJWA NA MAFISADI.LAKINI TUKIACHANA NA EXCUSE HIYO YA TAKUKURU (WAMESHATOA LUKUKI) THIS IS A WAKE UP CALL KUHUSU HIZI KINGA DHIDI YA VIONGOZI WASTAAFU (NA PENGINE HATA KWA WALIO MADARAKANI).WAKATI WAZO LA KINGA NI ZURI LIKITUMIWA VIZURI,KWA MFANO DHIDI YA WANAOTAKA KUDHALILISHA VIONGOZI KWA SABABU BINAFSI AU KISASI,WAZO HILO NI HATARI KWA VIONGOZI WALIOZITUMIA VIBAYA OFISI ZAO WALIPOKUWA MADARAKANI.MAHALA PEKEE PANAPOWEZA KUMSAFISHA MKAPA NI MAHAKAMANI NA WALA SIO KWA KAULI ZA KULINDANA KAMA HIZO ZA TAKUKURU.


WAKATI Ripoti ya kitaalam ikionyesha namna bora ya kupunguzwa matumizi ya magari ikiwamo ya kifahari maarufu kama mashangingi, serikali imeanza utekelezaji wa mpango mwingine mkubwa wa kuingiza magari mapya 792 kutoka Japan.

Mpango huo mkubwa wa serikali umekuja wakati ripoti ya kitaalamu inayotaka ijipunguzie matumizi yasiyo ya lazima katika ununuzi wa magari ikiwemo ya kifahari ikiwa imewasilishwa mezani kwa Katibu Mkuu Kiongozi Philemon Luhanjo tangu Aprili mwaka huu.

Waziri Mkuu Mizengo Pinda ambaye wiki moja iliyopita alitoa angalizo kwa makatibu na manibu makatibu wakuu wa wizara kuhusu kupunguza matumizi ya magari ya kifahari, alinukuliwa na gazeti dada la The Citizen, akisema serikali haiwezi kupiga marufuku ununuzi wa magari hayo wakati imeshaagiza lakini alisisitiza kuwa hiyo itakuwa mzigo wa mwisho kuagizwa na mashangingi kiasi hicho.

Ingawa Pinda hakufafanua, lakini duru huru zaidi za habari kutoka serikalini zilidokeza gazeti hili jijini Dares Salaam jana kwamba, tayari magari 300 yalishaingizwa chini ya mpango huo. "Sehemu kubwa ya magari hayo ni Toyota Pickup, tayari 300 yameingizwa nchini chini ya mpango huo maalumu wa serikali," zilisema duru hizo za habari.

Kwa ufafanuzi zaidi, duru hizo zilisema katika orodha hiyo pia yapo mashangingi Vx na GX ambayo jumla yao ni kati ya 100.

Chini ya mpango huo, duru za habari zilisema gari nyingine ambazo ni nyingi ni pamoja na Toyota Land Cruiser Hard Top ambazo kwa takwimu za kiserikali moja hugharimu kati ya sh 72 hadi 75 milioni.

"Ukiacha Vx na Gx 100, magari mengine mengi katika orodha hiyo ni Toyota Land Cruiser Hard Top na Pickup ndiyo mengi katika orodha hiyo ya magari 792," kilifafanua zaidi chanzo hicho.

Waziri Mkuu Pinda alikaririwa jana na gazeti dada la Mwananchi, The Citizen, katika mahojiano maalum akisema uamuzi wa kuzuia ununuzi wa magari hayo hauwezi kuchukuliwa kwa sasa, kwa kuwa tayari yameshaagizwa na yataanza kuingia nchini hivi karibuni.

“Uamuzi wa kuzuia ununuzi wa magari hayo hauwezi kufanyika sasa kwa kuwa magari 800 tayari yameshaagizwa kutoka kampuni inayoyatengeneza nchini Japan na yanatarajiwa kuanza kuingia nchini hivi karibuni,” alisema Pinda katika mahojiano hayo.

Hata hivyo, Pinda alieleza kuwa katika mwaka wa fedha ujao mambo yatakuwa tofauti kutokana na kuwataka makatibu wakuu kutoagiza magari hayo na fedha zitazopatikana katika zoezi la kuacha kununua magari hayo zinunue matrekta ambayo yatakuwa na matokeo yanayoonekana katika kilimo.

Hakuna mtu anaweza kufa kwa kutopanda gari la kifahari (Toyota Land Cruiser VX, GX) lakini kwa kukosa chakula itakuwa ni tatizo,” alisema Pinda katika mahojiano hayo.

Alisema uamuzi wake huo umekuwa ukiungwa mkono na Rais Jakaya Kikwete, ukiwa umelenga kumkomboa mkulima ambaye amekuwa anatumia jembe la mkono kwa miaka 47 ya uhuru wa nchi hii.

“Magari haya ya kifahari yamekuwa yananunuliwa kutokana na baadhi ya watumishi (wakurugenzi) kutaka kuendana na wakati wa magari ya kifahari yaliyopo sokoni,” alisema Pinda huku akisema serikali sasa inataka kuondokana na dhana hiyo.

Alipoulizwa mbona serikali imeamua kuendelea kununua magari hayo japokuwa yamekuwa yanasemwa kuwa ni mzigo kwa serikali, Pinda alisema wakati anaingia tayari magari yalikuwa yameshaagizwa na hivyo mpango huo utaanzia kwenye bajeti ijayo ya serikali.

Aliongeza kuwa “Nimeongea na makatibu wakuu wiki iliyopita nimewaambia kuhusu suala hili la uagizaji magari ya kifahari, sasa tuachane nalo na badala yake tujikite kwenye kilimo cha kisasa,”

Duru hizo zikieleza kwa kina mpango huo, Ripoti ambayo iko kwa Luhanjo na gazeti hili kufanikiwa kuona nakala yake, inaonyesha namna bora ya serikali kupunguza ununuzi wa magari hasa ya kifahari.

Katika mpango huo, moja ya jambo lililopendekezwa na watalaamu ni kuhakikisha gari la moja aina ya VX au Gx hubadilishwa na kukunuliwa jingine kila baada ya miaka saba tofauti na sasa, ambapo waziri, naibu au makatibu wakuu hubadili magari hayo kila baada ya miaka miwili.

Ripoti hiyo pia inaonyesha orodha ya viongozi wanaopaswa kutumia magari hayo kwa kupunguza viongozi wanaopaswa kutumia Vx na Gx, ambao wanapaswa kutumia ni mawaziri, manaibu, makatibu wakuu na manaibu wao, huku kuanzia wakurugenzi wakipasawa kutumia magari mengine ikiwemo Land Cruiser za kawaida.

Pia kumekuwa na pendekezo la kufuata utaratibu ambao hutumiwa na serikali kama ya Afrika Kusini, Namibia na Botswana ambazo hutumia Kampuni ya Emperial kwa ajili ya usimamizi wa kiteknolojia kwa ajili ya magari yote ya serikali ili kuyaangalia na kudhibiti yasitumike katika shughuli binafsi.

Emperial kwa kutumia teknolojia hiyo huweza kuonyesha hatua ya kila gari kwa kutumia mfumo maalumu wa usalama na pia kuzuia wizi hata wa mafuta katika magari ya serikali ambayo sasa hivi hakuna mfumo wa kuyadhibiti.

CHANZO:Mwananchi

NANI KASEMA MATREKTA KWA WAKULIMA NI MUHIMU KULIKO NYONGEZA YA MASHANGINGI KWA WAHESHIMIWA?EBO?NYIE MNATAKA WAHESHIMIWA WAKAGUE MAENDELEO WAKIWA KWENYE MATREKTA?UHESHIMIWA NI PAMOJA NA KUWA KWENYE GARI LA KIFAHARI.HIZI NDIZO PRIORITIES ZETU ZITAKAZOMWEZESHA KILA MTANZANIA KUWA NA MAISHA BORA HIVI PUNDE TU!



PICHA HIZI ZINAONYESHA UHARIBIFU ULIOSABABISHWA NA VURUGU ZINAZOENDELEA NCHINI UGIRIKI KUFUATIA POLISI KUMUUA MTOTO MMOJA.BAADA YA KUANGALIAPICHA HIZO,HEBU SOMA HABARI IFUATAYO KUHUSU VIFO VYA WATOTO WATATU HUKO KILIMANJARO.
WATOTO watatu wa jamii ya wafugaji wa Kimasai, wameuawa kwa kupigwa risasi na askari polisi waliopo kwenye mazoezi ya kulenga shabaha katika Kijiji cha Embukoi, wilayani Siha, mkoani Kilimanjaro.

Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Embukoi, Peter Pekasi, alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea majira ya saa 10 jioni, ambapo watoto hao walikuwa wakipita eneo kwenda kusaga nafaka katika mashine iliyo jirani na kijiji hicho.

Mtendaji huyo aliwataja watoto wanaodaiwa kuuawa kuwa ni Lyomo Orkwari (7), Laata Mollel (15) na Samwel Josia(8), wote wakazi wa kijiji hicho cha jamii ya Masai.

Pekasi alisema eneo la tukio limekuwa likitumiwa kwa muda mrefu kama kituo cha kulenga shabaha kwa askari waliopo mafunzoni katika Chuo cha Mafunzo ya Polisi Moshi (CCP) na kuhatarisha maisha yao.

Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa kwa Mkuu wa Wilaya ya Siha, Anarose Nyamubi.

Kamanda wa Polisi mkoani Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alipoulizwa kuhusiana na tukio hilo, alisema hana taarifa kamili za tukio hilo na kuongeza kwamba ametuma maafisa wake eneo la tukio.

“Jamani nimepata taarifa hizo muda mfupi kabla hujaja hapa, nimetuma maofisa wangu eneo la tukio, kwa sasa siwezi kuzungumzia chochote, nitatoa taarifa zaidi baada ya kupata maelezo ya kina kutoka kwa askari wangu,” alisema Ng’hoboko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Siha, Nyamubi, akizungumza kwa njia ya simu jana, alithibitisha kupata taarifa hizo, lakini hakuwa tayari kuzungumzia kwa undani na kwamba ametuma maofisa wake eneo la tukio.



NA HAITOSHANGAZA IWAPO HAKUNA ATAKAYEWAJIBIKA KWA VIFO VYA WATOTO HAO WASIO NA HATIA.


Monday, 22 December 2008

AISEE,ILE ISHU YA KUMTWANGA GEORGE W BUSH NA KIATU INAENDELEA KUVUTA HISIA.LATEST,JAMAA ALOTENGENEZA VIATU VILIVYOTUMIKA KUMTWANGA BUSH AMEJIKUTA AKIPATA DILI KIBAO,YAANI CHATI NDIO IMESHAPANDA.SINTOSHANGAA TUKISKIA NA HUKO HOME SHOE-SHINER FLANI KAPATA DILI BAADA YA KIATU ALICHOKUWA AKIKIHUDUMIA KUTUMIKA KUMRUSHIA FISADI FLANI....NAJUA HIYO NI PIPE-DREAMING KWA VILE MAFISADI WENYEWE WANALETWA MAHAKAMANI NA MASHANGINGI,WAKIWA LUPANGO WANALAZWA VIP KAMA KEMPINSKI,NA WAKIPATA DHAMANA WANACHUKULIWA NA MA-VOGUE YAO!BACK TO STORI YA IRAQI,KONG'OTA HAPA USOME ZAIDI

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget