Pengine ushasikia kuhusu Perfect Storm.Sijui tunaweza kuiitaje kwa Kiswahili lakini kwa kifupi ni hivi: kadri idadi ya watu inavyoongezeka duniani,mahitaji ya chakula,maji na nishati nayo yanaoongezeka.Pasipo jitihada za makusudi na za haraka kufanyika,inatarajiwa kufikia wakati flani bei za vyakula zitakuwa hazikamatiki,watu lukuki watakabiliwa na njaa kutokana na uhaba wa chakula,na idadi wa "wakimbizi" kuongezeka kutoka mahala kwenye uhaba kuelekea kwenye nafuu (ambayo itapelekea sehemu hizo zenye nafuu nazo kujikuta zikishindwa kuhimili mahitaji ya "wakimbizi" hao).
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo,inatarajiwa kwamba kufikia mwaka 2030 idadi ya watu duniani itafikia bilioni 8 kutoka bilioni 6 ya sasa,mahitaji ya chakula yatapanda kwa asilimia 50,mahitaji ya maji yatapanda kwa asilimia 30 na ya nishati nayo asilimia 50.
Kama ilivyo kawaida ya majanga makubwa,nchi masikini huwa waathirika wakubwa zaidi kutokana na uwezo duni unaochangiwa pia na viongozi mafisadi walio maarufu zaidi kwa ngonjera kuliko vitendo.Kabla ya hiyo 2030,tayari kumeanza kujitokeza kinachoitwa "ukoloni mpya wa ardhi" ambapo baadhi ya makampuni ya katika nchi zilizoendelea yamekuwa yakinunua ardhi kwa kasi katika nchi masikini.Hali hiyo inajionyesha zaidi huko Ulaya Mashariki,lakini kuna kila dalili kuwa upepo unaelekea kwenye "shamba la bibi",yaani bara letu la Afrika.Urahisi wa Afrika unachagizwa zaidi na mitizamo mifupi ya baadhi ya viongozi wetu kuwa hatuwezi kuendelea pasipo ushiriki wa "wawekezaji" katika mipango yetu ya maendeleo (kana kwamba "wawekezaji" hao ni wazalendo wenzetu).
Itakumbukwa kuwa miezi michache iliyopita viongozi wetu waliwashawishi "masikini wa ardhi" kutoka Saudi Arabia kuja kuwekeza Tanzania huku wakihakikishiwa umilikishwaji ardhi wa muda mrefu.Nawaita Wasaudi "masikini wa ardhi" kwa vile asilimia kubwa ya nchi za Ghuba,Arabia na Mashariki ya Kati zina uhaba mkubwa wa ardhi ya kilimo (sehemu kubwa ni jangwa) japo wana utajiri wa mafuta.Tatizo sio kuwakaribisha Wasaudia au Makaburu,bali ni udhaifu sugu tulionao kwenye udhibiti wa raslimali zetu.Uzoefu tulionao katika namna madini yanavyokombwa kwa pupa na " wawekezaji" huku tukiambulia mrahaba " cha mtoto" ambao asilimia kubwa unaishia mifukoni mwa mafisadi,ni dhahiri kukodisha ardhi kwa wageni kutapelekea kuiweka rehani nchi yetu,achilia mbali wakulima kuporwa ardhi yao kama inavyoshuhudiwa kwenye maeneo yenye madini.
2005 CCM iliahidi Maisha Bora kwa Kila Mtanzania,lakini kabla hatujapewa tathmini ya utekelezaji wa wimbo huo,kunakuja hadithi nyingine ya Kilimo Kwanza.Huu ni usanii wa kisiasa.Kilimo Kwanza mwaka mmoja kabla ya uchaguzi?Kwanini haikuwa kwenye Ilani ya 2005?Na kwa aliyepata muda wa kusoma kilichomo kwenye "kibwagizo" hicho cha Kilimo Kwanza atabaini kuwa ni muendelezo uleule wa kupiga risasi kisha kulenga (shooting then aiming).Yaani,watu wanakurupuka na mawazo ya ajabu ajabu,yanashindikana kisha zinaanza semina elekezi za kujadili kwanini mkakati ulishindwa.
And these people can't be serious kwa vile wakati wanakuja na Stimulus Package (sijui imeishia wapi) "walisahau" kuwa kilimo bado ni uti wa mgongo wa uchumi wa Tanzania,with exception of mafisadi ambao uti wa mgongo wa uchumi wao ni ufisadi.
Ni katika mazingira hayo tunalazimika kujiuliza itakuwaje hapo 2030 tunapotarajia hiyo Perfect Storm.Of course,sie tushazowea storms mbalimbali miaka nenda miaka rudi.Tunaambiwa taifa letu changa lakini tunamudu kuongeza maradufu mishahara ya wabunge huku walimu wakitishia kugoma kutokana na madai yao ya malimbikizo ya mishahara yao kiduchu.
Kitakachotunusuru ni kudra za Mwenyezi Mungu pekee kwa vile sote tunajua nini kitatukumba come hiyo Perfect Storm tukiwa na wababaishaji kama hawa waliopo sasa.