Monday, 5 January 2009
13:23
Unknown
No comments
ALIYEKUWA Mkuu wa Majeshi Nchini, Meja Jenerali, Robert Mboma, amesema anaamini kitambi alicho nacho kimesababisha kushindwa katika kura za maoni za Chama cha Mapinduzi (CCM) za ubunge wa Jimbo la Mbeya Vijijini.
Mboma aliyasema hayo juzi wakati akiwashukuru wananchi katika uzinduzi wa kampeni za chama hicho za kinyang'anyiro cha ubunge wa jimbo hilo.Alisisitiza kuwa anaamini kilichochangia kutopata kura nyingi zaidi ni kitambi hicho alichokuwa nacho na kwamba hali hiyo itamkomaza kisiasa.
Mboma ambaye aliwashangaza baadhi ya watu walioshuhudia uzinduzi wa kampeni hizo uliofanywa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi katika kijiji cha Ilembo Mbeya vijijini.Alisema kkuanguka kwake katika jimbo hilo kumetokana na wananchama wa chama hicho kumnyima kura.
Alisema kitendo hicho hakiotamuathiri bali wanamkomaza kisiasa na kwamba endapo kama angeteuliwa kuwa Mbunge wa jimbo hilo angelepeleka maendeleo."Kwa kweli nanawashukuru wananchi mlionipigia kura nilizozipata ingawa hazikuwa ndogo lakini ninasikitika na ninawashukuru ambao hawakunipigia kura na kuniangusha wakati wakijua wazi kuwa mimi ni mzaliwa na hapa na mngenichagua ningewaletea wananchi maendeleo katika jimbo la Mbeya vijijini," alisema.
Aliendelea kusema kuwa sio mbaya hata kama wamemchagua Mchungaji Mwanjali kwa sababu anaimani atawaletea Maendeleo na kurithi yale yote aliyatarajia kuyafanya aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Marehemu Richard Nyaulawa katika kuboresha huduma za jamii hususan maji, umeme na kuboreshea miundombinu...HABARI HII INAENDELEA HAPA.
NILIDHANI WANAJESHI WANASTAHILI KUJIWEKA FIT HATA BAADA YA KUSTAAFU MAJUKUMU YAO.HOW COME MKUU WA MAJESHI AMEJIACHIA KIASI CHA KUWA NA KITAMBI KIKUBWA "KILICHOPELEKEA KUANGUSHWA KWAKE KWENYE KINYANG'ANYIRO HICHO"? BY THE WAY I DONT BUY HIS LAME EXCUSE.NADHANI HAKUFANYA RESEARCH YA KUTOSHA KABLA YA KUJIINGIZA KWENYE COMPETITIVE POLITICS.WATANZANIA WAMEANZA KUTOFAUTISHA KATI YA UMAARUFU WA MTU NA UWEZO WA KUWALETEA MAENDELEO.AND IT'S THE LATTER THAT LED TO MBOMA'S FAILURE TO WIN HIS PARTY'S NOMINATION.
HII DHANA YA KWAMBA ANGEPATA UBUNGE ANGEWEZA KUWALETEA MAENDELEO WANA MBEYA VIJIJINI SIO TU POTOFU BALI PIA MUFILISI.KWANI ILI KULETA MAENDELEO YA WANANCHI WENZIO NI LAZIMA UWE KIONGOZI WAO?ALISHINDWAJE KUWALETEA MAENDELEO ALIPOKUWA KIONGOZI WA KITAIFA (MKUU WA MAJESHI) LAKINI AWEZE ATAPOPATA UBUNGE?NI UKOSEFU WA WASHAURI WAZURI AMBAO WANGEPASWA KUMKUMBUSHA HISTORIA YA MA EX-CDF WENZIE.

Magazeti mbalimbali ya leo huko nyumbani yameongozwa na habari za uzinduzi wa kampeni za CCM katika uchaguzi mdogo wa jimbo la Mbeya Vijijini unaotarajiwa kufanyika baadaye mwezi huu.Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi ndiye aliyezindua kampeni hizo na kufanya kila ambacho kwa muda mrefu kimekuwa adimu katika duru za siasa za vyama vingi huko nyumbani.Kwa mujibu wa habari hizo,Mwinyi,maarufu kama Mzee Ruksa,alitumia sehemu kubwa ya hotuba yake kuzungumzia maslahi ya wana-Mbeya Vijijini katika uchaguzi huo badala ya kuipigia debe CCM pekee.
"Mwinyi...hakuonyesha unazi kwa CCM wala mgombea wake wakati alipozindua kampeni za chama hicho jana katika kata ya Kijiji cha Ilembo kilicho tarafa ya Isangati wilayani Mbeya Vijijini.Badala yake, Mwinyi alisisitiza amani, mshikamano na maendeleo ya wilaya ya Mbeya Vijijini, akiwataka wananchi wa eneo hilo kuhakikisha wanabakia na mshikamano wakati wanasiasa watakapoondoka jimboni humo baada ya purukushani za uchaguzi..." linaandika gazeti la Mwananchi.
Tanzania Daima linamnukuu Mwinyi akisema kwamba "Vyama vya siasa vishindane kwa sera, visitumie lugha za matusi, kejeli, dharau na uongo wakati wa kampeni, uungwana wenu viongozi wa siasa utawapa matumaini wananchi kuchagua chama au mtu wanayemtaka ili kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi yanakua kwa kasi".
Akionyesha kuthamini zaidi maslahi ya wananchi wa Mbeya vijijini kuliko ya kisiasa,Rais huyo mstaafu aliwausia wapiga kura jimboni humo "kumsikiliza kila mgombea kwa makini na baadaye kila mmoja amchague yule anayeona sera za chama chake zinakidhi matumaini ya wananchi wa Mbeya Vijijini, " na kuhakikisha "kwamba wakati wanasiasa wetu wanapoondoka Mbeya Vijijini baada ya kampeni nyinyi mnabaki kuwa kitu kimoja katika umoja wenu," linaeleza Habari Leo.
MIONGONI MWA MAMBO YANAYOKWAZA MAENDELEO NI KUWEKA MBELE MASLAHI YA KISIASA BADALA YA YALE YA WANANCHI.OF COURSE,VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WANAPASWA KUSIMAMIA MASLAHI YA VYAMA VYAO LAKINI NI MUHIMU KWAO KUTAMBUA KUWA JUKUMU KUU LA VYAMA HIVYO NI KUWAHUDUMIA WANANCHI NA NI WANANCHI HAOHAO WANAOWEZESHA KUWEPO HAI KWA CHAMA IN THE FORM OF WANACHAMA.KWA MANTIKI HIYO,WANANCHI,REGARDLESS YA POLITICAL AFFILIATIONS ZAO,WANA NAFASI NA UMUHIMU WA KIPEKEE KWA VYAMA VYA SIASA HASA IKIZINGATIWA PIA KWAMBA WAO NDIO PIA CHIMBUKO LA UONGOZI KATIKA CHAMA CHOCHOTE CHA SIASA.
BAADA YA KUNG'ATUKA KATIKA ACTIVE POLITICS,BABA WA TAIFA ALIJITAHIDI KUCHUKUA NAFASI YA UANASIASA WA KITAIFA BADALA YA KICHAMA AMBAPO MARA KADHAA ALIWEKA MKAZO KATIKA MASUALA YANAYOHUSU TAIFA KWA UPANA BADALA YA YALE YA CHAMA CHAKE CHA CCM PEKEE,LICHA YA KUWA YEYE NDIO ALIKUWA MIONGONI MWA WAASISI WAKUU WA CHAMA HICHO TAWALA.KWA UPANDE MWINGINE,MWINYI NAFASI YA MWINYI BAADA YA KUSTAAFU UENYEKITI WA CCM IMEPEWA ATTENTION NDOGO NA WACHAMBUZI WA SIASA PAMOJA NA MEDIA KWA KUTOFANYA REFERENCE YA NAMNA KIONGOZI HUYO WA ZAMANI ANAVYOJITAHIDI KUFUATA FOOTSTEPS ZA BABA WA TAIFA KATIKA KUTANGULIZA ZAIDI MASLAHI YA WANANCHI NA TAIFA KWA UJUMLA BADALA YA KUENDEKEZA UNAZI WA KISIASA PEKEE.
NI MATUMAINI YA WATANZANIA WOTE WAPENDA MAENDELEO KWAMBA MFANO HUU WA MZEE MWINYI UTAIGWA NA WANASIASA WETU WOTE KAMA KWELI NIA YAO NI KUTUHUDUMIA KUPITIA VYAMA VYAO.LAKINI PIA WANANCHI NAO WANAPASWA KUFUMBUKA MACHO NA KUTAMBUA KWAMBA UNAZI WA KISIASA HAUPASWI KUWA INFRONT OF MASLAHI YAO KAMA WANANCHI,NA KWA MANTIKI HIYO TOFAUTI ZETU ZA KIITIKADI HAZIPASWI KULETA MGAWANYIKO AU KUPELEKEA KUCHAGUA VIONGOZI WABOVU KWA VILE TU WANATOKA KATIKA VYAMA TUNAVYOSHABIKIA.
HONGERA SANA MZEE RUKSA.YOU TRULY HAVE SHOWN THE RIGHT WAY.
Sunday, 4 January 2009

Ghana's peaceful presidential election was a rare example of a functioning democracy in Africa and should be a model for the continent, African leaders and voters have said. Skip related content
Much attention in Africa and elsewhere was focused on the Ghanaian vote after a year of political crises, many of them violent, tarnished Africa's democratic credentials.
Opposition candidate John Atta Mills was declared the winner on Saturday after the closely fought election was settled by a run-off.
Kenya's prime minister Raila Odinga said: "John Atta Mills' victory and the conduct of the people of Ghana provides a rare example of democracy at work in Africa."
While the contest raised tensions and some violent incidents were reported, international observers say the vote was mostly peaceful. The conduct of the election contrasted with many other African countries, where democracy was battered in 2008.
More than 1,000 people were killed in post-election violence in Kenya at the start of the year and in Zimbabwe President Robert Mugabe and opposition leader Morgan Tsvangirai have been deadlocked for months over a power-sharing agreement after disputed elections.
SOURCE: ITN
Friday, 2 January 2009
Maelfu ya waandamanaji wanatarajiwa kuandamana baadae leo jijini London kupinga mashambulizi ya Israel dhidi ya Wapalestina.Inakadiriwa takriban watu 20,000 watashiriki maandamano hayo yatakayowajumuisha watu maarufu kama Mbunge wa chama cha Respect,George Galloway na mwanamuziki mkongwe Annie Lennox.Picha ya mwanzo inaonyesha akinamama wa Kiislam walioandamana jana jijini Dar kupinga mashambulizi hayo,na picha za chini zinaonyesha hali ilivyo na uharibifu uliosababishwa na makombora ya Israel huko Gaza.




VYANZO:Sky News,Habari Leo ,The Washington Post na The Guardian.
Subscribe to:
Posts (Atom)