Sunday, 4 August 2013

Timu nzima ya TanzMED inayo furaha kukutaarifu kuwa tumefanya maboresho kwenye wavuti yako kipenzi ya afya, Tanzmed.com. Katika awamu hii, mambo mengi  yamezingatiwa ili kukuwezesha wewe mtumiaji kuitumia TanzMED bila tatizo toka mahala popote kwa kutumia kifaa chochote.

tanzmed-mpya


Muonekano mpya wa TanzMED ukiwa na feature nyingi mno, kama;
1. Muonekano bomba usiochosha
2. Kuboreshwa kwa lugha ya kiswahili iliyotumika kwenye wavuti 
3. Wavuti za kwenye simu, watumiaji wa simu sasa wataweza kuperuzi bila utata, nenda http://m.tanzmed.com 
4. Kuimarika mambo ya usalama wa wavuti, hivyo upo salama pindi unapotembelea TanzMED
5. Kuongeza spidi kwa kupunguza vitu visivyo na ulazima, pia kutumia tekinolojia mpya zaidi.
6. Kuunganisha Facebook na TanzMED moja kwa moja, hivyo kuwawezesha watumiaji kupata mlisho wa makala toka Facebook.
7. Kuanzishwa kwa profile mpya ya waandishi wa TanzMED, hii itasaidia wana TanzMED kuweza kupata mawasiliano ya Daktari husika moja kwa moja na kuwafahamu zaidi wana timu wa TanzMED
Na mengine meeengi ...
Tembelea http://tanzmed.com/   kwa Afya njema.
TanzMED -  Afya kwa Wote!



.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
.
Picha kwa hisani ya MILLARD AYO

Friday, 2 August 2013

Thursday, 1 August 2013


HATIMAYE PINDA KUWA WA KWANZA KUBURUZWA MAHAKAMANI ...
Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kimemfungulia mashtaka Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kutokana na kauli yake aliyoitoa bungeni hivi karibuni kwamba wanaokaidi maagizo ya dola wapigwe.

Hatua hiyo ya LHRC imepingwa vikali na Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), Dk Elieza Feleshi akisema hakuna uhalali wa mashtaka yoyote dhidi ya kiongozi huyo sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.

Mkurugenzi wa LHRC, Dk Hellen Kijo Bisimba alifungua mashtaka hayo katika Mahakama Kuu jana akisema kuwa wanamshtaki Waziri Mkuu kwa maelezo kuwa amekiuka kifungu cha Katiba Ibara 13 (1). Pinda ametajwa kuwa ni mdaiwa wa kwanza katika kesi hiyo namba 24.

Mkurugenzi wa Maboresho na Utetezi wa LHRC, Harold Sungusia alisema jana kwamba, mwingine aliyeunganishwa katika kesi hiyo ya kikatiba iliyofunguliwa na LHRC na Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema.

Alisema katika kesi hiyo, kuna jopo la mawakili wasiopungua 20 na kwamba wamepata saini za wananchi 2,029 wanaopinga kauli hiyo ya Pinda na kuunga mkono kufunguliwa kwa kesi hiyo.

Mjumbe wa Bodi ya LHRC, Wakili Dk Ringo Tenga alisema katika kesi hiyo wameangalia zaidi sheria na hasa haki za msingi za binadamu na kwamba kauli hiyo ya Waziri Mkuu Pinda inahatarisha haki hizo.

Kauli yenyewe

Wakati wa Kipindi cha Maswali ya Papo kwa Papo kwa Waziri Mkuu bungeni, Juni 19, mwaka huu, Waziri Mkuu akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Kilwa Kaskazini (CCM), Murtaza Mangungu aliyeuliza: “Serikali ipo tayari kiasi gani kubainisha na kuchukua hatua stahiki, badala ya kusakama makundi fulani, tujue chanzo halisi cha vurugu hizi na matatizo haya na jinsi gani vyombo vya dola vinavyoshughulikia kwa sababu yapo malalamiko katika baadhi ya maeneo kama Mtwara kwamba wananchi wanapigwa na vyombo vya dola?”

Waziri Mkuu alijibu: “Ni lilelile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu... hamna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.

“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi... wewe ndiyo jeuri zaidi watakupiga tu.... Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine... maana tumechoka.” Kesi hiyo itakayosikilizwa na majaji watatu, haina uhusiano na kesi nyingine ambazo wajibu maombi hupewa siku 90 kujibu hoja zilizowasilishwa. Kesi hiyo imefunguliwa kwa mujibu wa Katiba Sura ya Tatu.

Akizungumza juzi kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma baada ya kufungwa kwa Warsha ya Wapelelezi na Waendesha Mashtaka wa Serikali ngazi ya mikoa, Dk Feleshi alisema hakuna uhalali wa mashtaka hayo kwa sababu kauli ya Pinda kuwa pigeni haikuwa piga ua.

“Hii haikuwa kuchochea apige watu, alichosema ni kupiga wale wasiotaka kutekeleza amri halali na zaidi alisema piga lakini si kupiga na kuua,” alisema.

Mkutano huo uliendeshwa chini ya ulinzi mkali huku kukiwa na udhibiti wa kuvuja siri kwa kiwango cha juu. Pamoja na mambo mengine, ulikuwa ukijadili mbinu za kisasa katika kuendesha kesi pamoja na kujiuliza sababu za Serikali kushindwa katika kesi nyingi.

“Kwa sababu lile neno kupiga ni lazima lipewe maana pana huwezi kumpiga tu mtu hivihivi ambaye hakuvunja sheria lakini nilivyoelewa, ilikuwa ni hivyo, ni sawa na mtu ambaye anamshambulia askari,” alisema Dk Feleshi.

Alisema kuna sheria ya kutumia nguvu pale ambako kuna mkusanyiko usiokuwa wa halali pindi raia wanapokaidi kutawanyika kwa hiari hivyo hakuna shaka kauli ya Waziri Mkuu ililenga hivyo.

Hata hivyo, alisema hajapata taarifa za LHRC kumshtaki Waziri Mkuu kimaandishi na kwamba akizipata atatoa ufafanuzi baada ya kuona lengo la mashtaka.

Msimamo

Akizungumza baada ya kufungua mashtaka hayo, Dk Bisimba alisema Waziri Mkuu anaweza kushtakiwa kwa kuwa alizungumza kwa nafasi yake ya Waziri Mkuu na si mbunge na kusisitiza kwamba hakuna aliye juu ya sheria na kudai kwamba kauli hiyo ni kinyume cha Katiba.

Alisema kuwa kila anayevunja Katiba lazima ashughulikiwe kisheria na kwamba mahali pake ni mahakamani tu. Alisema kwa mujibu wa hati hiyo ya madai, kauli na amri kama hizo zinapotolewa na kiongozi mwenye hadhi kama ya mdaiwa wa kwanza (Waziri Mkuu) huchukuliwa kama sheria inayopaswa kutekelezwa na wakala wa utekelezaji wa sheria kama vile polisi. Wadai hao wanadai kuwa kwa ufahamu wao polisi wanaweza kuchukulia kauli hiyo kama amri halali kutoka kwa mkubwa wao na hivyo kuwapiga na kuwatesa watu wasio na hatia, kinyume cha Katiba.

Pia wanadai wanatambua kuwa Ibara ya 100 (1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa kinga kwa wabunge na uhuru wa maoni bungeni. Hata hivyo, wanatambua kuwa Ibara ya 100 (2) ya Katiba hiyo inawawajibisha wabunge wote chini ya masharti ya Katiba na kwamba kauli aliyoitoa Waziri Mkuu Pinda inakiuka Ibara ya 12(12).

Hivyo wanaiomba Mahakama hiyo itamke kuwa kauli na amri hiyo aliyoitoa Pinda inavunja Katiba.

Mkurugenzi wa taasisi inayofuatilia Mwenendo wa Bunge (Watch), Marcos Albania alidai kwamba wamegundua kuwa kauli hiyo ya Pinda ni moja kati ya matamko makubwa yanayovunja Katiba.

Alisema mbali na shtaka hilo, kuna la pili dhidi ya Waziri Mkuu Pinda, ambalo hawajalifikisha mahakamani ambalo pia linatokana na kauli hiyo aliyoitoa bungeni kwamba: “Sasa wamechoka.”




TANGU niwasili kwa mara ya kwanza hapa Uingereza zaidi ya miaka 10 iliyopita, nimejijengea tabia moja ambayo ni mithili ya ‘ibada’ yangu kila asubuhi, kusoma habari za huko nyumbani katika vyanzo mbalimbali vya habari mtandaoni.
Na ni katika mwendelezo wa tabia hiyo, Oktoba 2006 nilikutana na habari moja iliyohusu ‘sakata la Richmond.’ Katika habari hiyo ndani ya gazeti moja la kila siku huko nyumbani (Tanzania), ilielezwa aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, alikuwa anafanya jitihada za kuhamasisha wabunge wa CCM wawe na msimamo mmoja katika mjadala bungeni kuhusu sakata hilo.
Wakati huo nilikuwa nikituma makala katika gazeti moja la kila wiki huko nyumbani (sio hili), na kutokana na kuguswa na habari hiyo ambayo iliashiria uwepo wa harakati za kukwaza mjadala wa maana kuhusu skandali ya Richmond, niliifanya habari hiyo kuwa mada kwenye makala ya wiki iliyofuatia.
Makala hiyo ilinisababishia matatizo makubwa. Kwanza, mwandishi wa habari wa Waziri Mkuu (wakati huo) aliandika makala kali ya kunijibu, pamoja na mambo mengine aliniita mpotoshaji, huku akikanusha kwa nguvu mtizamo wangu kuwa ‘Lowassa alikuwa anajaribu kuwafumba mdomo wabunge wa CCM wasijadili suala la Richmond bungeni kwa ufanisi.’
Siku chache baadaye, nilipata simu kutoka kwa kiongozi mmoja wa juu wa taasisi niliyokuwa nikiitumikia wakati huo. Katika simu hiyo, bosi huyo alihoji iwapo nipo hapa Uingereza kimasomo au kisiasa. Alikwenda mbali zaidi na kunituhumu kuwa huenda wakati huo nilikuwa nikiitumikia Serikali ya Uingereza, kosa ambalo kwa mujibu wa kanuni za sehemu niliyokuwa mtumishi wakati huo ni sawa na kosa la uhaini (treasonable offence).
Kadhalika, kiongozi huyo, alinishambulia kuwa makala zangu zilikuwa zikiwapa hoja wapinzani wa CCM, na kisha kuniamuru niache mara moja kuandika makala zinazohusu masuala ya siasa za huko nyumbani. Nilijaribu kutii amri hiyo kwa muda mrefu lakini baadaye nikashindwa baada ya kuja huko nyumbani mwaka 2008 na kushuhudia jinsi mafisadi walivyokuwa wakiitafuna nchi yetu.
Kosa lililosababisha bosi huyo kufikia hatua ya kinipigia simu ya karipio ni makala hiyo niliyobainisha hapo awali, ambayo kimsingi ililenga kushauri uwepo wa mjadala huru na wa wazi kuhusu sakata la Richmond. Katika makala hiyo nilitahadharisha kuwa jitihada zozote za ‘kulifunika suala hilo chini ya kapeti’ zinaweza kuzua madhara huko mbele.
Miaka miwili baadaye, nilichobashiri katika makala hiyo kikatokea. Hatimaye Lowassa alilazimika kujiuzulu kutokana na skandali hiyo ya Richmond. Kama nilivyoitarajia, yule bosi aliyenikaripia mwaka 2006 hakunipongeza, na sidhani kama hadi leo (bado yupo madarakani) anatambua umuhimu wa nilichoandika wakati huo.
Kimsingi, tukio hilo ndio lilikuwa mwanzo wa uhusiano mbaya na mwajiri wangu, na picha iliyozidi kujengeka ni ya mie kuonekana msaliti kwa ‘kuisema vibaya’ CCM na serikali yake. Japo kimsingi nyingi ya makala zangu kuhusu siasa ziliendana na wajibu wa taasisi hiyo kwa umma, vitisho na manyanyaso mfululizo hatimaye vilisababisha ajira yangu katika taasisi hiyo ‘kutowezekana.’
Lengo la makala hii sio kumlaumu mtu au taasisi fulani. Pamoja na misukosuko kadhaa niliyopitia kutokana na dhamira yangu kunituma kujadili masuala mbalimbali yanayokwaza maendeleo ya nchi yetu, hususan ufisadi, bado ninaamini kwa asilimia 100 kuwa ninafanya jambo stahili, hata kama limeshanigharimu katika maisha.
Nilichokuwa ninafanya nilipokuwa mwajiri wa taasisi hiyo ndicho hasa kilichopaswa na kinachopaswa kufanywa na kila mwajiriwa na kiongozi wa taasisi hiyo ya umma, sambamba na kila Mtanzania mwenye upendo wa kweli kwa nchi yetu. Hatuna nchi nyingine zaidi ya Tanzania, na tusipoilinda na kuienzi hatutokuwa na pa kukimbilia (hasa tukizingatia hivi sasa tuna uhusiano wa shaka na baadhi ya majirani zetu).
Kilichonisukuma kurejea mkasa huo ulionikumba miaka kadhaa iliyopita ni mawasiliano niliyofanya majuzi na mwalimu wangu mmoja wa zamani hapo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Binafsi, mwalimu huyo ni kama mzazi wangu kielimu kwani ameniongoza tangu nikiwa mwanafunzi wake hapo ‘Mlimani,’ na kuniunga mkono kitaaluma hadi nikamudu kupata shahada nyingine mbili (licha ya niliyoipata UDSM), na ameendelea kuwa nguzo yangu muhimu wakati huu ninaposaka shahada ya nne – ya uzamivu (licha ya vikwazo mbalimbali vya kimaisha nilivyokumbana navyo).
Mwalimu huyo (ambaye ninaomba nihifadhi jina lake) alinieleza kuwa amekuwa akizungushwa na serikali kuongezewa mkataba wake kama mhadhiri katika kitivo kimoja chuoni hapo. Pengine msomaji unaweza kudhani nimeguswa na suala hili kwa vile tu mhadhiri huyo amekuwa na msaada katika maisha yangu kitaaluma. Ukweli ni kwamba takriban kila mwanafunzi aliyefundishwa na mhadhiri huyo atakubaliana nami kuwa mwanataaluma huyo ni mfano wa kuigwa kwa jinsi anavyojibidiisha kuhakikisha wanafunzi wake wanafaulu.
Na kujibidiisha huko hakumaanishi kuwapatia wanafunzi njia za mkato bali ni pamoja na kutumia muda wake binafsi hata katika siku za mapumziko kuwafundisha wanafunzi wake, iwe ni katika majengo ya chuo au nyumbani kwake.
Uzuri mwingine wa mhadhiri huyo ni ukweli kwamba yeye si muumini wa hizi dini zetu za ‘mapokeo’ yaani Ukristo na Uislamu. Ninasema ni ‘uzuri’ kwa sababu pamoja na mazuri ya dini zetu, kuna aina fulani ya ‘ubaguzi uliofichika’ unaotokana na mafunzo ya dini hizo, hususan katika kipengele cha ‘imani yangu ndio sahihi kuliko nyinginezo.’ Asiye muumini wa Ukristo au Uislam, kama ilivyo kwa mhadhiri huyo, ana ‘faida’ ya kuelezea mambo pasi kukwazwa na ‘sheria kali za kiimani’ zinazotawala dini zetu.
Katika kubobea kwenye taaluma ya Sosholojia (elimu-jamii), mwongozo mkubwa wa kitaaluma na kimaisha kwa mwalimu huyo ni jamii. Na ndio maana, kama ilivyo katika masuala ya dini, yeye amekuwa ‘neutral’ (asiyefungamana na upande wowote) katika itikadi za kisiasa. Kwake, jamii ndio nyanja muhimu zaidi katika maisha ya mwanadamu.
Mhadhiri huyo anashangaa kwa nini serikali imekuwa ikisuasua kumwongezea mkataba wake hasa ukizingatia kuwa utendaji kazi wake ni wa hali ya juu hadi amefikia hatua ya kupata Uprofesa. Na kwa kila anayemfahamu, kusita kwa serikali kumwongezea mkataba mwanataaluma huyo kunaashiria jambo moja tu; kutothamini michango ya Watanzania wenzetu wanaojitolea kwa maslahi ya taifa letu.
Bahati nzuri amefanikiwa kupata chuo kikuu cha kufundisha katika nchi moja barani Afrika, lakini hata hivyo anajisikia uchungu kuona anakwenda kutoa mchango wa kielimu katika nchi nyingine ilhali taifa letu lina mahitaji makubwa ya wataalamu katika nyanja mbalimbali, hususan elimu ya juu.
Sitaki kujifananisha na mwanataaluma huyo mahiri, lakini kwa kiasi flani, yanayomsibu yanashabihiana na kilichonikumba huko nyuma. Unatumikia umma kwa nguvu na moyo wako wote lakini wenye mamlaka wanakuona kama surplus to requirements (ziada isiyohitajika)
Athari kubwa ya kutothamini wenzetu wanaojitolea kwa ajili ya taifa letu ni ile hisia kuwa “ah, bora ujali tu maisha yako...mbona fulani alijiweka kimbelembele na angalia yaliyomfika.” Kwa lugha nyingine, uzalendo unakwazwa na vitimbi vinavyowaandama wenzetu wanatanguliza maslahi ya umma mbele ya maslahi yao binafsi.

Kwa mwenendo huu, basi tutazidi kushuhudia wataalamu mbalimbali wakiamua aidha kukimbilia kwenye ‘ulaji’ katika siasa au, kama ilivyo kwa mhadhiri huyo, kwenda kutumia utaalamu wao nchi nyingine, na kuliongezea taifa letu uhaba wa wataalamu katika sekta mbalimbali.

- See more at: http://raiamwema.co.tz/imebaki-kazi-moja-tu-kuipigania-tanzania#sthash.QVeXmYgZ.dpuf




Ahadi za JK kwenye kampeni za kusakaurais 2010
1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora
2. Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
3. Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria- Igunga
4. Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
5. Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
6. Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
7. Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
8. Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
9. Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi- Kagera
10. Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba- Bukoba Mjini
11. Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
12. Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
13. Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
14. Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu- Kagera
15. Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
16. Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba- Kagera
17. Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
18. Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika- Mwanza
19. Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
20. Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
21. Kulinda muungano kwa nguvu zote- Pemba
22. Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
23. Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa- Mbeya mjini
24. Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
25. Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
26. Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
27. Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
28. Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
29. Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi - Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
30. Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
31. Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
32. Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
33. Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
34. Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)- Hydom Manyara
35. Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa-Musoma
36. Kulinda haki za walemavu- Makete
37. Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
38. Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
39. Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
40. Kujenga barabara ya lami Manyoni- Kigoma– Kaliua,Tabora
41. Kukarabati barabara ya Arusha Moshi- Arusha Mjini
42. Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
43. Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido
44.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
45. Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha – Arusha mjini
46. Kukopesha wavuvi zana za kilimo- Busekera, Wilaya ya Musoma, .
47. Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
48. Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
49. Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
50. Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
51. Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
52. Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
53. Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania- Iringa
54. Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
55. kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
56. kuwapa wanawake nafasi zaidi- Kilolo ,Iringa
57. ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
58. Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa- Kabandamaiti mjini Zanzibar
59. Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
60. Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
61. Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
62. kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
61. Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
62. Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
63. Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
64. Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
65. Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa- Kibaha66. Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget