Timu nzima ya TanzMED inayo furaha kukutaarifu kuwa tumefanya maboresho kwenye wavuti yako kipenzi ya afya, Tanzmed.com. Katika awamu hii, mambo mengi yamezingatiwa ili kukuwezesha wewe mtumiaji kuitumia TanzMED bila tatizo toka mahala popote kwa kutumia kifaa chochote.
Muonekano mpya wa TanzMED ukiwa na feature nyingi mno, kama;
1. Muonekano bomba usiochosha
2. Kuboreshwa kwa lugha ya kiswahili iliyotumika kwenye wavuti
3. Wavuti za kwenye simu, watumiaji wa simu sasa wataweza kuperuzi bila utata, nenda http://m.tanzmed.com
4. Kuimarika mambo ya usalama wa wavuti, hivyo upo salama pindi unapotembelea TanzMED
5. Kuongeza spidi kwa kupunguza vitu visivyo na ulazima, pia kutumia tekinolojia mpya zaidi.
6. Kuunganisha Facebook na TanzMED moja kwa moja, hivyo kuwawezesha watumiaji kupata mlisho wa makala toka Facebook.
7. Kuanzishwa kwa profile mpya ya waandishi wa TanzMED, hii itasaidia wana TanzMED kuweza kupata mawasiliano ya Daktari husika moja kwa moja na kuwafahamu zaidi wana timu wa TanzMED
Na mengine meeengi ...
Tembelea http://tanzmed.com/ kwa Afya njema.
TanzMED - Afya kwa Wote!
0 comments:
Post a Comment