Tuesday, 13 May 2008

Niliposikia mara ya kwanza nilidhani ni stori tu za mjini.Jana nimesikia tena,na safari hii ni kutoka kwa mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita hivi majuzi.Ishu yenyewe iko hivi:eti wanafunzi wa kidato cha sita waliletewa mashuleni fomu za kuomba udhamini wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.Hadi hapo hakuna tatizo,Bodi inawajali wanafunzi hai inawaletea fomu shuleni.Mgogoro unaanzia kwenye taratibu za kurejesha fomu hizo ambapo kila mwanafunzi alipaswa kulipia shs 10,000/= ambazo ni non-refundable.Mgogoro zaidi ni ukweli kwamba zoezi zima la kujaza na kurejesha fomu hizo lilifanyika hata kabla wanafunzi hao hawajafahamu matokeo yao.Kwa maana hiyo,mwenye kufaulu na kufanikiwa kupata admission ya chuo anakuwa amenufaika lakini kwa aliyepata maksi zisizomruhusu kuendelea na masomo ndio ameliwa.This is what we call daylight robbery.Kwanini wasingechukua hiyo elfu 10 baada ya matokeo ili wale wasio na sifa wasiliwe fedha zao bure?Deadline ya kurejesha fomu hizo ilikuwa tarehe 30/04 na matokeo ndio yametoka majuzi.Sipendi kuona mikopo ya wanafunzi inageuzwa kuwa kama bahati nasibu flani,or to be more precise,ujambazi wa mchana kweupe.

Saturday, 10 May 2008

Hapa nilipo,mtandao unasumbua sana.Kwahiyo,nawaomba mniruhusu niwape tu LINK HII ya makala yangu katika toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema.

Saturday, 3 May 2008

Hivi karibuni,eneo la Mlimani (UDSM) liligeuka Baghdad kwa muda kufuatia ghasia kubwa kati ya wanafunzi na vyombo vya dola.Hali sasa ni shwari,na majuzi walifanya uchaguzi wa viongozi wapya wa DARUSO japo inasemekana kwamba turnout ilikuwa ndogo sana.Ni kutokana na ushwari huo ndipo nami nilibahatika kuwatembelea wanazuoni flani hapo,na kufanikiwa kunyaka picha hii inayoonyesha eneo la Ubungo kama sijakosea,japo halionekani vema sana.

Miongoni mwa maeneo ya hapa jijini yanayotuwezesha kuendeleza libeneke la bloggin-japo nyakati nyingine kwa kusuasua-ni cafe moja iliyopo Millennium Tower.Kuna jamaa kanidokeza kuwa yeye huwa mwenyeji sana eneo hili kwa ajili ya kuangalia MIGONGO!Well,inawezekana alikuwa anazungumzia mgongo wa Twiga huyu,jirani na mwanga wa taa,ambaye ni kivutio mwanana!

Sina budi kuwataka radhi wasomaji wapendwa kwa kutoweka chochote hapa kwa zaidi ya wiki sasa.Napenda sana ku-update blog hii lakini wakati mwingine mazingira ya hapa yanakuwa kikwazo.Hata hivyo,nadhani mtaburudika na makala yangu katika gazeti la Raia Mwema toleo la wiki inayoisha leo.Makala hiyo ni reaction dhidi ya wababaishaji flani ambao wanajaribu kuhoji usafi wa akina-sie tulioamua "liwalo na liwe" dhidi ya mafisadi.In fact sio kama wanahoji as such,wanachofanya ni kuwa servants wa mafisadi,nisicho na uhakika ni whether wanafanya hivyo kutokana na njaa zao au mfilisiko wa mawazo.Anyway,makala nzima inapatikana kwa kubonyeza hapa

Wednesday, 23 April 2008

Naamini wengi wenu mnakikumbuka kibao cha "Ingekuwa Vipi" cha wasanii Jay-Mo na Mwanafalsafa.Nakipenda,sio kwa beats zake pekee,bali pia kimebeba ujumbe mzito wenye maswali mazito.Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la Raia Mwema imeanza kwa kunukuu verse moja ya wimbo huo,lengo likiwa sio uchambuzi wa muziki bali kufanya tafakuri kuhusu mwelekeo wa mambo katika nchi yetu.Tangu nifike hapa nyumbani takriban wiki tatu zilizopita,nimekutana na watu kadhaa ambao wamekuwa wakidai BORA MKOLONI ARUDI KUTUTAWALA.Aliyenisukuma zaidi kujadili suala hili ni abiria mwenzangu niliyesafiri nae katika chumba cha "daraja la kwanza" cha TAZARA,ambaye nae alidai kwamba "Bora Mkoloni arudi" baada ya adha lukuki zilizotupata katika safari yetu.Mie nadhani bora Wachina warejeshewe TAZARA kwani sie Waswahili imetushinda.Hilo la Mkoloni kurudi sina hakika nalo sana,ila ni dhahiri kwamba kuna wanaharamu wanaotutesa mara 100 zaidi ya walivyofanya wakoloni.By the way,wakoloni hawakuwa Watanzania wenzetu,lakini hawa washenzi wanaotufisadi na kulimbikiza fedha (wenyewe wanaita vijisenti) huko nje ni watu tuliozaliwa nao nchi moja iitwayo Tanzania.Makala yangu hiyo imehitimishwa kwa onyo kwa CCM kwamba ikiendeleza porojo zake za Maisha Bora kwa kila Mtanzania (or did they mean "kwa kila fisadi"?) basi wasishangae wakikutana na yaliyowakuta KANU huko Kenya.Ukisikia wananchi wanatamani Mkoloni arudi basi hizo ni dalili kuwa wamechoshwa na porojo za watawala.Pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti la Raia Mwema,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA

Pia kuna picha kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Bongo.



















Nadhani kuna wanaoikumbuka joint moja ya maeneo ya Namanga kuelekea Msasani iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Studi Becker.Sasa hivi inaitwa New Angel.Pengine kwa vile ni ya "Malaika Mpya" ndio maana toilets zao ziko kizani kama inavyoonekana (au isivyoonekana?) katika picha.


















Picha hizi nzuri (hapo juu na zinazofuata chini) zimepigwa na dada mmoja mrembo wa Hoteli ya Kempinski (ameomba jina na sura yake vihifadhiwe) kutoka ghorofa ya sita ya hoteli hiyo.Dada huyo mdau wa blogu hii anadai amepatwa na wazo la kupiga na kunitumia picha hizo baada ya kuona kile "kimbembe cha zule" cha picha za matope ya barabara ya Ifakara.Picha zote zinaonyesha mandhari ya bandari ya Dar es Salaam,minus ufisadi wa Mamlaka ya Bandari na TICTS.







Tuesday, 22 April 2008

NINA LUNDO LA PICHA LAKINI LEO INTERNET IKO SLOW SANA.KEEP ON VISITING THE BLOG FOR MORE PICS.PICHA TATU ZA CHINI NI KUTOKA HOSPITALI YA MTAKATIFU FRANCIS IFAKARA (KUNA SANAMU YA MTAKATIFU HUYO KATIKA PICHA YA TATU).PICHA YA NNE NI MAHINDI YALIYOANIKWA KWENYE LAMI.SIJUI NDIO TEKNOLOJIA AU VIPI LAKINI THE IDEA IS SIMPLE:LAMI INAPATA JOTO UPESI NA KWA KUANIKA MAHINDI KWENYE LAMI BASI YANAKAUKA UPESI,NA MASUALA YA UGALI YANAWEZEKANA NDANI YA MUDA ULIOPANGWA.HIKI NI KIPINDI CHA MAVUNO,KWAHIYO NADHANI VIBAKA WA MAHINDI SIO WENGI.SIDHANI KAMA KATIKA KIPINDI CHA NJAA VIBAKA WATAYANUSURU MAHINDI YALIYOANIKWA BARABARANI.




Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget