Tuesday, 13 May 2008

Niliposikia mara ya kwanza nilidhani ni stori tu za mjini.Jana nimesikia tena,na safari hii ni kutoka kwa mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita hivi majuzi.Ishu yenyewe iko hivi:eti wanafunzi wa kidato cha sita waliletewa mashuleni fomu za kuomba udhamini wa Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu.Hadi hapo hakuna tatizo,Bodi inawajali wanafunzi hai inawaletea fomu shuleni.Mgogoro unaanzia kwenye taratibu za kurejesha fomu hizo ambapo kila mwanafunzi alipaswa kulipia shs 10,000/= ambazo ni non-refundable.Mgogoro zaidi ni ukweli kwamba zoezi zima la kujaza na kurejesha fomu hizo lilifanyika hata kabla wanafunzi hao hawajafahamu matokeo yao.Kwa maana hiyo,mwenye kufaulu na kufanikiwa kupata admission ya chuo anakuwa amenufaika lakini kwa aliyepata maksi zisizomruhusu kuendelea na masomo ndio ameliwa.This is what we call daylight robbery.Kwanini wasingechukua hiyo elfu 10 baada ya matokeo ili wale wasio na sifa wasiliwe fedha zao bure?Deadline ya kurejesha fomu hizo ilikuwa tarehe 30/04 na matokeo ndio yametoka majuzi.Sipendi kuona mikopo ya wanafunzi inageuzwa kuwa kama bahati nasibu flani,or to be more precise,ujambazi wa mchana kweupe.

Related Posts:

  • THE PITFALLS OF OPPOSITION POLITICS IN TANZANIASome political analysts argue that ruling parties in Africa never lose elections,and if they do,which is rarely,it is likely not because they failed to deliver to the people who put the parties in power but rather either due … Read More
  • LOTTO YA MIKOPO YA ELIMU YA JUUNiliposikia mara ya kwanza nilidhani ni stori tu za mjini.Jana nimesikia tena,na safari hii ni kutoka kwa mwanafunzi aliyehitimu kidato cha sita hivi majuzi.Ishu yenyewe iko hivi:eti wanafunzi wa kidato cha sita waliletewa ma… Read More
  • NAPE: NCHI KWANZA CHAMA BAADAYE (HABARI NDANI YA GAZETI LA RAIA MWEMA)Chama cha siasa huzaliwa,hukua na kinaweza kufa pengine hata kabla hakijakua.Tofauti nachama nchi ikishazaliwa ni lazima iishi milele,tena kwa gharama yoyote ile.Lakini kuna wenzetu wengine hawataki kuelewa ukweli huo.Kwao,ch… Read More
  • WALIMU WACHARUKAWALIMU wa Mkoa wa Dar es Salaam jana walimshambulia kwa kumrushia mawe, chupa za maji, viti na meza, Rais wa Chama cha Walimu Tanzania nchini (CWT), Gratian Mukoba, kwa madai kuwa amewasaliti kwa kukubali kuahirisha mgomo wao… Read More
  • HII NDIO TANZANIA YETU:MITIHANI YA FORM FOUR YAVUJA KWA KASIMitihani zaidi kidato cha nne yavuja Necta iko njia pandaBARAZA la Mitihani Tanzania (Necta) bado liko njia panda kuhusu hatua za kuchukua baada ya mtihani mwingine wa kuhitimu kidato cha nne mwaka huu kuthibitika kuwa umevuj… Read More

2 comments:

  1. comment nzuri,i like that,hawa jamaa ni wezi sana,nakumbuka kipindi nahangaika kutafuta chuo pale bongo,nilikwendda mzumbe university,nakumbuka katika ujazaji wa zile loan form kuna mstari mmoja nakumbuka nilijaza kwa herufi ndogo na sikuwa na wino wa kufuta,then naambiwa hiyo form haitangaliwa na inabidi nitoe tena elfu kumi(10000)ili form nyingine mpya!!!!!!mmhhh kweli hamna elimu ilio bora kama ile ya mtaani.........bongo 'we acha tu'

    ReplyDelete
  2. mnh jamani kwa kweli hata mie nilipata shock pale niliposikia wadogo zangu wanasema eti tunajaza form za HELSB kabla ya matokeo, jamani jamani mbona visa vinazidi? Hivi huyu mtanzania anayeibiwa kwa EPA, RICHMOND, KIWIRA, BOT, NDEGE YA RAIS, RADA FEKI, KODI KUBWA, MSHAHARA MDOGO, NJAA, UMEME BEI JUU, NA BADO form za HELSB nazo zinakuwa bahati nasibu, jamani jamani mbona machozi yanantoka mie. Hivi ina maana tuna makosa ya kuwaweka hawa jamaa zetu kutuendeshea nchi? Au nao HELSB wameona bora na wao wachukue chao mapema ili wapate visenti vya kuweka offshore accounts? Kilio kilio kwa mtanzania jamani

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget