Friday, 4 February 2011


Kuna jitihada zinazofanyika huko nchini Misri katika jitihada za kumaliza machafuko yaliyodumu kwa zaidi ya siku 10 sasa kushinikiza kung'oka madarakani kwa Rais Hosni Mubarak.Jitihada hizo zinafanywa na kundi linalojumisha "Kamati ya Watu wa Busara" (ni kama Wazee wa Busara lakini sio kama wale walioimbwa na kundi la Wachuja Nafaka ).Watu hawa wenye heshima zao katika taifa hilo wanajaribu kuepusha maafa zaidi ambapo inaelezwa kuwa hadi sasa zaidi ya watu 300 wameshauawa.Kwa mfano,miongoni mwa mambo waliyojaribu kuishauri Serikali ya Mubarak ni kuangalia uwezekano wa Rais huyu kubaki na cheo cha heshima (figure head) lakini majukumu ya kuendesha nchi yakabidhiwe kwa Makamu wa Rais.Kadhalika,walidai kuwa wanaweza kushawishi kundi la Muslim Brotherhood lisisimamishe mgombea iwapo Serikali ya Mubarak itakubali kuitisha uchaguzi.

Ukiangalia mwenendo wa mambo huko nyumbani,ni dhahiri nasi tunahitaji Wazee wa Busara wa kukutana na Rais Jakaya Kikwete,angalau kumwamsha katika lindi la usingizi unaomkabili na kumfahamisha kuwa taifa letu linaelekea kusikostahili.Tunaweza kujidanganya kuwa yanayotokea Misri hayawezi kutokea kwetu lakini ukweli ni kwamba mazingira yaliyopelekea mbinde huko Misri,Tunisia,na sasa Yemen na Sudan (kwa kiasi flani) pia yapo huko nyumbani.Umasikini wa kupindukia ambao unapuuzwa na watawala wanaozidi kujirundikia utajiri,sambamba na kupora raslimali za umma;ukosefu wa ajira;utawala wa kibabe (rejea mauaji ya raia wasio na hatia huko Arusha na Mbeya,sambamba na nguvu kubwa kupita kiasi zinazotumiwa na vyombo vya dola kudhibiti maandamano ya amani),to mention but a few.

Unfortunately,wazee aliotuachia Baba wa Taifa ndio dizaini ya akina Kingunge-watetezi wakubwa wa ufisadi.Kuna watu kama Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi,Mawaziri Wakuu Wastaafu kama Warioba na Cleopa Msuya,na wanasiasa kama akina Joseph Butiku lakini hawa wote wanakwazwa na tatizo lilelile linaloikwamisha Tanzania yetu: kuweka maslahi ya kisiasa mbele ya maslahi ya taifa.Angalau Warioba amejaribu mara kadhaa kuzungumza "kwa niaba ya umma" lakini mafisadi wakaanza kumuundia zengwe.

Nalazimika kupigia mstari umuhimu wa kuwatumia Wazee wa Busara kumwamsha Kikwete kwa vile inaelekea Rais wetu anajifanya haelewi kinachoendelea kwenye maisha ya Watanzania wengi.Yoote aliyoahidi wakati wa kampeni zake za mwaka 2005,na kisha kuyarejea tena wakati za kampeni za mwaka jana yanaelekea kuwa yamesahaulika kama sio kupuuzwa.

Majuzi nilityumiwa comment na msomaji mmoja aliyenishutumu kwa kile alichoita "kuchochea vurugu" na kudai mie nahamasisha yanayotokea Misri na Tunisia yatokee Tanzania pia ilhali mie mwenyewe niko nje ya nchi.Mpuuzi huyu anajifanya haelewi kwamba kuwa nje ya nchi hakumaanishi Utanzania wangu unakuwa nusu.Afterall,nina ndugu,jamaa na marafiki wanaoteseka kutokana na hayo nayopigia kelele kila siku.

Na hata blogu hii ikikaa kimya,au wazalendo wa mtandao kama Jamii Forums nao wakinyamaza,ukweli unabaki kuwa siku moja Watanzania wanaweza kusema this is too much,liwalo na liwe.Mwanafalsafa Karl Marx aliwahi kutuasa kuwa masikini hana cha kupoteza (akiamua liwalo na liwe) except minyororo anayobebeshwa na watawala dhalimu.

Tuna uchaguzi mmoja tu: kubadilisha hali ya mambo kwa njia za amani ama sivyo yanayojiri mahala kwingineko yanaweza kutokea kwetu pia.Sio suala la kuombea au unabii wa maangamizi bali huo ni ukweli mchungu.Hakuna namna ya kumaliza ugonjwa pasipo tiba.

Na kwa Kikwete na jamaa zake,ni muhimu kujifunza katika yanayoendelea huko Tunisia,Misri,Jordan,Yemen na Sudan.Kuendelea kuwakumbatia mafisadi wanaokwangua uchumi wetu kila kukicha ni jambo lisilokubalika hata chembe.

TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA

6 comments:

  1. Mkuu Chahali, wewe endeleza mapambano, kwani kelele za chura haziwezi kumzuia ng'ombe kunywa maji. Binafsi nilishakumbana na shutuma za aina hiyo kwasababu tu ya kukemea ufisidi.

    ReplyDelete
  2. wengi wetu ,tunafikiri tunaijuwa tanzania vizuri,tunajuwa watanzania vizuri,tunajuwa matatizo ya watanzania vizuri,hata jinsi wanavyo fikiri wa tanzania tunajuwa.? nacho juwa mimi,mwananchi mtanzania,awe mkulima au mfanyakazi,anasemewa mengi tu ,na kundi la watu wachache na kugeuka ndiyo sauti ya mwanchi huyo.sasa siku atakapo amua kujisemea yeye mwenyewe kwa kinywa chake kile anacho kitaka,na kile anacho fikiria,tuta linganisha uamuzi huo nayale ambayo tumekwisha wasemea kabla ya wao kupaza sauti zao? niawazo yangu tu na kuchanganyikiwa kwangu.kaka s.

    ReplyDelete
  3. NYIE WASOMI WETU BWANA, HAYA BANA. BINAFSI NADHANI NI VIZURI KUTOFAUTISHA MACHUNGWA NA MALIMAU BADALA YA KUYACHANGANYA.
    -MUBARAK AMEKUWA MADARAKANI KWA MIAKA 30, WAKATI KIKWETE NDIO AMEIINGIA KUMALIZIA NGWE YAKE YA MWISHO
    -MUBARAK AMEKUWA TYRANT KWA TAKRIBANI MIAKA YOTE ALIYOTAWALA, SINA UHAKIKA KAMA HUYU WA KWETU AMEFIKIA SIFA HIYO.
    -ALIKUWA AUTHORITARIAN KULINGANISHA NA RAISI WETU.
    -KUTOKNA NA UROHO WA MADARAKA, MUBARAK ALIHAKIKISHA KWAMBA INSTITUIONS NYINGI KAMA VILE CIVIL SOCIETY NA UPINZANI HAVIIMARIKI, HAPA KWETU KAMA UNAVYOJUWA, UPINZANI UPO NA WA NGUVU.
    BWANA CHALALI, INAWEZEKANA KWAMBA WENGI HATUKUKUBALIANA NA MATOKEO YA UCHAGUZI ULIOPITA NCHINI MWETU, LAKINI KUMFANANISHA KIKWETE NA MUBARAK, AU HALIYA EGYPT NA TANZANA SIDHANI KWAMBA SAHIHI. INAWEZEKANA KWAMBA WENGINE TULIISHIA NGUMBARO, LAKINI ARICLE ZINGINE NI MORE THAN PROPAGANGA.

    ReplyDelete
  4. Naomba nipingane nawe Chahali. Wazee wenye busara tunao wengi na wamejitahidi kumuelimisha huyu jamaa asiye na masikio bila mafanikio. Wapo akina Joseph Warioba, Joseph Butiku, Issa Shivji, Jenerali Ulimwengu, Cleopa Msuya, Fredrick Sumaye na wengine wengi tu.
    Yeye anapenda ibada za wazee njaa wa Dar es salaam ambao wanaweza kumramba popote atakapo ilmradi awatupie sazo.
    Kinachotakiwa si wazee tena bali vijana shupavu na kuingia mitaani kuhakikisha Tanzania haitawaliki. This is the only smartest move that can kick this heck out of there.

    ReplyDelete
  5. Chahali unachosema ni ukweli mtupu. Hali iliyoibusha haya ya Tunisia na ya Misri kimsingi ni ile ile tuliyo nayo hapa Bongo. Kwa bahati mbaya, wale wanaonufaika na mfumo wa kifisadi hawawezi kuliona hilo.
    Naomba nimsaidie kidogo anony wa 05/02/2011 18:29. Misri imekuwa chini ya udikteta wa mtu mmoja, Mubarak. Tanzania imekuwa chini ya udikteta wa chama, CCM. Kwa hiyo hakuna anyeweza kumlaumu Rais JK kwa huo udikteta wa chama - ni mfumo ambao naye ameurithi na kama mambo yangeendelea kuwa yale yale ya 1947, basi ana haki ya kuulinda kwa nguvu zake zote. Lakini karne ya 21 inahitaji kiongozi mwenye maono na vision. Kwa madaraka aliyo nayo rais wa Tanzania kwa mujibu wa Katiba yetu choka-mbaya (yaani urais-ufalme), JK anayo nafasi nzuri sana (kama angekuwa na utashi au vision) ya kuongoza ama niseme ku-initiate mchahakato wa mabadiliko kama ambayo tunasikia waTunisia na waMisri wanadai. Hilo ndilo wazalendo na wanaharakati wanalizungumzia - sio kwa sababu wanamchukia JK (JK ni muungwana na mwenye kutabasamu kwa kila mtu na kila kitu, ni mtu mzuri sana)bali wanamwona ndiye aliyeshika husukani ambao akiumudu vyema anaweza kutuepusha na hayo ya Tusinia na Misri. Je, huo utashi, vision, nk anavyo?

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget