Showing posts with label CHANGAMOTO YETU. Show all posts
Showing posts with label CHANGAMOTO YETU. Show all posts

Wednesday, 25 August 2010


Hongera nyingi kwako Mzee wa Changamoto Yetu kwa blogu yako kutimiza umri wa miaka miwili.Ama kwa hakika blogu yako ni miongoni mwa sehemu zinazofanya kuweko mtandaoni kuwa ni jambo la muhimu katika maisha yetu ya kila siku.Hekima na filosofia zako zinaamsha tafakuru kubwa,huku ukihakikisha tunamwayamwaya na burudani ya miziki mbalimbali.Kwa hakika,Changamoto Yetu ni miongoni mwa sababu zinazonifanya niendelee kupenda fani ya kublogu.

Kila andiko lililowekwa kwenye blogu yako katka kipindi hiki cha miaka miwili kimekuwa na manufaa makubwa kwa jamii.Ni dhahiri kuwa kila unapoandaa andiko la kuweka bloguni hapo unakuwa na picha ya sie wasomaji wako akilini na hivyo kufahamu maswali,kiu,mshawasha,na matamanio au mahitaji yetu mengine.

Kukupa sifa unazostahili inahitaji chapisho kubwa zaidi ya thesis ya PhD.Naomba pongezi hizi fupi ziwakilishe stahili zako zote kutokana na kazi mwanana unayoifanya kwa jamii.

Again,Hongera Sana na Happy Birthday.

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget