Saturday, 11 December 2010



Majuzi kulifanyika uzinduzi wa kitabu kinachoelezea wasifu wa Rais Jakaya Kikwete.Tukio hilo linaelekea kuwa na uzito wa kipekee kwani baadhi ya picha zilionyesha sehemu kubwa ya familia ya mkuu huyo wa nchi ilihudhuria uzinduzi huo.Sina hakika kuhusu kilichomo kwenye kitabu hicho lakini yayumkinika kuamini kuwa laiti wasifu huo ungegusia masuala kama "Wanamtandao na mchango wao katika ushindi wa Kikwete 2005",au "Uswahiba kati ya Kikwete,Lowassa na Rostam Aziz na jinsi unavochangia kufilisika kwa Tanzania", au "wasifu wa wateuliwa mbalimbali wa Kikwete na namna wanavyohusiana nae",nk isingekuwa rahisi kwa Rais Kikwete kujitokeza kwenye uzinduzi huo.

Mwandishi wa kitabu hicho ni Profesa Julius Nyang'oro.Wakati mwingine najiuliza kama baadhi ya maprofesa wa aina hii wameishiwa na mada za muhimu kwa jamii na badala yake wanageukia kujikomba kwa watawala kwa kuandika wasifu mithili ya pambio.Unaweza kunilaumu kwa kutoa tuhuma kabla sijasoma kilichomo katika kitabu hicho.Hata hivyo,huhitaji upeo wa juu kubashiri yaliyomo katika kitabu hicho,maana laiti ingekuwa ni wasifu wa Kikwete huyu ambaye utawala wake umetuzalishia msamiati wa "ufisadi",sambamba na kugubikwa na ishu za Kagoda,EPA,Dowans,Richmond na uzururaji njeya nchi,basi si mkulu huyo wala wanafamilia yake wangetia mguu kwenye uzinduzi huo.

Sasa sijui Profesa Nyang'oro kajaza nini kwenye wasifu huo!Mamia ya ahadi za Kikwete na kisha kuichambua moja baada ya nyingine ( kwa mtizamo chanya usiomuudhi mtawala) au ni hadithi za namna Jakaya alivyozaliwa katika familia ya kawaida,akajiendeleza pasipo makeke,akashika hatamu za uongozi lakini akiendelea kuwa "mtu wa watu" na hatimaye akapata urais ( bila kutaja mchango wa wanamtandao) na ameendelea kuwa mwenye upendo na upole sio kwa walalahoi pekee bali hata mafisadi.

Huenda wasifu huo pia ukagusia udaktari wa falsafa (wa heshima) wa Rais Kikwete.Inawezekana atapomaliza miaka yake 10 hapo 2015 (na kama hatafanya mbinu za kutaka aongezewe muda madarakani) ataweka historia nyingine ( on top ya ile ya kumpiku Vasco da Gama kwa safari) ambapo atakuwa kiongozi pekee aliyezawadiwa shahada nyingi za uzamifu kuliko mwingine duniani.Sijui mpaka sasa ana PhD ngapi,ila nakumbuka ile ya Uturuki,nyingine sijui ya Uganda kama sio Kenya,hii ya juzijuzi Dodoma na Muhimbili nao wamemzawadi shahada ya Afya ya Jamii.


Na kwa vile utawala wa Kikwete umetawaliwa na usanii wa namna flani,yayumkinika kuhisi kuwa hizo PhDs zinatolewa baada ya wahusika "kupigwa somo" au "kupewa kilicho chao".Ungeweza kuhisi kuwa ilikuwa hivyo hata Profesa Nyang'oro,lakini "mnyonge mnyongeni haki yake mpeni" hapo itakuwa mtu tu kaamua kujikomba.

Na kama ilivyozoeleka,wanahabari wetu (pamoja na baadhi ya mabloga) walichokumbuka ni picha za tukio na maelezo ya picha hizo (captions) tu,utadhani kwa kuangalia picha hizo msomaji atapata summary ya jumla ya kilichomo katika kitabu hicho.Hapa "simpigi mtu dongo" ila natoa changamoto kwa wenzetu mliobobea kwenye picha,mkumbuke kuwa picha pekee si habari kamili.Hivyo,inapowezekana mtupatie habari zaidi ya picha husika.Ni ushauri tu,tena wa bure buleshi.

Nakumbuka mwaka 2005 kulikuwa na kitabu cha wasifu wa Kikwete.Nahisi hapa katikati kuna waliojipendekeza na kuja na wasifu mwingine.Sasa tuna wasifu huu "mpya" kutoka kwa Profesa Nyang'oro na huenda hapo 2015 kutakuwa na wasifu mwingine wa "miaka 10 ya mafanikio ya kihistoria chini ya utawala wa Jakaya Kikwete".Mtu mmoja wasifu kibao!

Enewei,hiyo ndio Tanzania yetu.Na ukiwa na kiongozi mpenda sifa basi wajanja hawachelewi kumpamba kwa sifa hii au ile.Na kwa vile hawagusii yale yatakayomfanya mtawala atambue kuwa "hajafunga zipu" basi kwa upande mmoja watoa sifa hao wanapata wanachotegemea kupata (sifa,hela,kupiga picha na rais,kualikwa ikulu,na pengine kuzawadiwa U-DC) na kiongozi mpenda sifa anaendelea kuamini yeye ni chaguo la Mungu ndio maana sifa zinaendelea kumiminika kumhusu yeye.

12 comments:

  1. hahah! Ati Mister Misifa..i still think hiki kitabu kingetoka after he finished his 2nd term

    ReplyDelete
  2. I think this is the weakest president so far in the history of Tanzania. That being said it may be necessary for "wapambe" to find all the necessary things that will make him look credible and raise his ability" The only way to do so is to give him all the free "PHD honors" without sweating for it, write a book about him etc. Labda tu tuwe wakweli: kiongozi gani ambaye anapenda knowledge/education, mwenye vision etc atakubali kupewa free honors na akatembea kifua mbele when people call him/her Doctor? Kuna waliopewa all kinds of honors lakini wamekataa kuitwa Doctor. I think it is OK to receive those honors, lakini haibadilishi jina/initial yako simply because elimu au uelewa wako bado upo palepale, hauwezi ku-improve baada yakutunikiwa shahada hiyo. That means JK Kikwete bado ni kiongozi mwenye low IQ we have ever had, weak (in-terms ya uelewa wake)/asieona mbali (no vision), and incompetent. In short he is just a ceremonial leader to most of Tanzanians. He brings nothing to the table apart from a smile.He simply does not know what critical thinking and competency is all about! Sad enough he seems to have lost touch with reality.

    ReplyDelete
  3. izo message unacomment mwenyewe pple see u az a fool kuwa unampondea vbaya baba wa watu ata kama unamchukia bt si kumuandika kama ivyo mr misifa n ol others we sijui ukoje bt waonekana wa ajabu we mkaka stp being a fool

    ReplyDelete
  4. Sasa ndugu yangu,kwani hatuwezi kutofautiana mitizamo pasipo kutumia matusi?Binafsi siafikiani nawe kuniita fool lakini kutoafikiana nawe hakuhalalishi nami nikuite stupid.Why?Because you're simply exercising your constitutional rights to express yourself.Ndio freedom of speech hiyo.Sasa kama ni ruksa kwako kutumia haki yako ya kikatiba kutoa mawazo yako,how come iwe foolishness kwangu kufanya hivyohivyo?

    Na unaposema naandika comment mie mwenyewe,mbona hujiulizi kipi kilikusukuma mpaka ukaja hapa kutoa comments?Je kwa busara zako hudhani kuwa kuna watu wengine kama wewe wanaoweza kufanya kama ulichofanya (kuja hapa bloguni) na kuunga mkono (au kupinga kama wewe)?

    Pamoja na lugha zako zisizo za kistaarabu,naomba kukushukuru kwa kufika hapa na kutoa mchango wako wa mawazo.Karibu tena

    ReplyDelete
  5. Chahali hafanyi kosa lolote.This is part of his service to the country he loves. Muda wakusifiana uongo umekwisha. Wewe unayesema "anampondea baba wa watu" niambie kama kila mtanzania ana maisha bora. Niambie kama wingi wa magari Dar unaonyesha wenzetu wa Mbeya, Makambako, Dodoma, Mbagala etc wanamaisha bora. Niambie kama mtu mwenye akili zake anaweza kutoa misaada ya vibabaji kwaajili yakubeba wamama wajawazito ili wawahi hospitali. Jamani it is a no brainer. Please acha kutetea vitu ambavyo havina maana this is 21st century, tunataka kuona vitendo sio kucheza ngoma tu na pilau. We have to put in place short and long-term strategies that can be implemented successfully and achieved, and if not achieved we have to find out why (evaluate) and take it from there.Please jaribu kufikiri kabla yakutoa maoni. Unapoutaka uongozi kubali kuwa critically challenged, kiongozi ni mtumishi wa wananchi na sio uwe mzigo kwa wananchi wako. Watanzania tuache tabia za utumwa, kuabudiana hakuna tija.Tunaelewa wazi tatizo la umaskini nchini kwetu sio resources bali ni Leadership lakini bado tunakumbatia uozo.

    ReplyDelete
  6. For the record My name is Sis N but I chose to be Anonymos and I am the one who posted the first comment. So no need to insult other peoples intelligence kwamba wanapost wenyewe. By the way watu wenye upeo mdogo sana ndio wanaweza ku-post message zao wenyewe. I like this blog, to me it the best blog simply because you can challenge other peoples ideas without using profanities.

    ReplyDelete
  7. hey tanzanian people achane kulalamika kwenye ma-blog,suluhu kama umeonewa si muandamane?mnalalamika kwenye blog nani anaejali?

    ReplyDelete
  8. Kwenye uzinduzi wa tabu hili mtungaji alikiri kuwa huu ni mradi. Kumbe ni mradi! Nitashangaa kitabu hiki kisipotoa majibu ya uhusika wa Kikwete kwenye EPA na Richmond kama ilivyodaiwa na asikanushe. Hata hivyo, uzoefu unanipa kuwa yataongelewa 'mazuri' ya Kikwete tu huku mabaya na mapungufu yake na utawala wake yakinyimwa fursa. Tuliona haya kwenye kitabu cha maisha ya mwizi na imla wa zamani wa Kenya Daniel arap Moi.
    Kama ni mradi mwandishi amekuwa mkweli ingawa uteuzi wake wa mradi unatia shaka baina ya maslahi binafsi na ya taifa. Kwanini Kikwete na si kuandika vitabu dhidi ya ufisadi, ubabaishaji, kujuana na jinai nyingine ambazo zimetamalaki?
    Je usomi wa namna hii unaojifungia kwenye watu maarufu huku ukiwapuuzia makapuku una faida kwa jamii inayowatengeneza wasomi hawa? Ukisikia mwisho wa usomi ndiyo huu. Prince Bagenda aliandika kitabu cha uongo mtupu akidhania angepewa ubalozi akaambulia kujidhalilisha. Hata huyu Nyang'oro amejizika kitaaluma na kujiumbua alivyo mbabaishaji anayeweza kutumiwa na kila fisadi. Kama ndicho kitabu chake pekee basi ajihesabu mtunzi bali mwimbaji wa sifa za mafisadi.
    Chahali, hawa wanaokutukana usiwajibu kwa vile walishajiishia. Wao hawana tofauti na kapu ambalo hubeba kila balaa liwekwamo ndanimwe.
    Kikwete angekuwa kama wanavyotaka aonekane angetunga lau kitabu kimoja ili umma ujue uoni wake. Lakini kwa vile hana guts atabaki kutungiwa kama maiti na matapeli wanaotaka kuwa karibu naye ili wapate makombo ya ufisadi.

    ReplyDelete
  9. Huyo jamaa naona ameamua kutunga kitabu kwa nia ya kujipendekeza. Hata hivyo mhariri wa kitabu hicho alimkosoa siku ya uzinduzi na kumwambia ameegemea kwenye upande mmoja zaidi wa kiurafiki badala ya kuangalia changamoto zilizopo. Huo nduo uandishi wa "Kikasuku"

    ReplyDelete
  10. @Anony wa kwanza: nashindwa kukuelewa kabisa kwa kuwa wewe unatupeleka kwenye kumjadili JK a.k.a mbayuwayu kama mtu binafsi wakati hoja ilotolewa na mtoaji ni juu ya ISSUES around taasisi anayoiongoza:URAIS!

    Hapo ndo tunashindwa kuwa waelewa na tunapojadili issues na mwingine anatupeleka kusiko inakuwa haipendezi.

    Kiukweli ukweli unauma...ndo sababu unaropoka na kulaumu!

    ReplyDelete
  11. Sasa haya machafufu na madudu yote ANAYOFANYA NA SERIKALI YAKE NINI CHA KUSIFIA..!!!!!!Certainly,We got right strongly to highlit all dirtiness issues going on this shame regime

    ReplyDelete
  12. Huyu mtunzi wa hiki kitabu anajikomba na kujipendekeza..hakuna mazuri yoyote ambayo amefanya ktk nchi yetu hu prezident! Halafu watu wamempa tena kipindi kingine "cha kula". Shame upon him! najua hasomi blogs lakini message zitamfikia anyway!

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget