KULIKONI UGHAIBUNI
Asalam aleykum waungwana.
Nadhani kabla ya kubwabwaja mengi ingekuwa ni vema tukatambuana. Lakini kabla ya hapo, ngoja nikunong’oneze kitu kimoja kuhusu gazeti hili mwanana la KULIKONI.Hili sio gazeti la kawaida. Japokuwa hili ni toleo la pili tu, lakini nimeshuhudia kwa macho na masikio yangu maelfu kwa maelfu ya wapenda habari wakisema kwamba gazeti hili tayari limeshakidhi kiu ya wasomaji japo ndio kwanza linaanza. Na nawahakikishia wenye mtizamo huo kuwa hawajakosea. Ama kwa hakika huu ni mwanzo wa tofauti na mazoea. Japokuwa yapo baadhi ya magazeti yanayotoka mara moja kwa wiki ambayo ukilikosa linapotoka usitarajie kulipata siku inayofuata, kwa KULIKONI ukilikosa Ijumaa basi uwezekano wa kulipata kesho yake ni finyu sana. Kwa kifupi, ni gazeti linalokidhi matakwa ya kila aina ya msomaji: mtu mzima kwa kijana, kinababa kwa kinamama, waliojiajiri kwa walioajiriwa, na kadhalika na kadhalika.
Nirejee kwenye kujitambulisha. Mimi ni Mtanzania mwenzenu, na hadi naandika makala haya nipo hapahapa nchini, lakini nitakuwa nikiwaletea makala kutoka huko Ughaibuni ninakoishi. Naamini kuna mengi yanayotokea huko Ughaibuni ambayo ninyi wasomaji watukufu mngependa kuyapata sio kwa mtizamo wa CNN, Newsweek au Times, bali kwa mwenzenu ambae anayaona katika macho ya ki-Tanzania. Labda nifafanue. Mara ya kwanza nilipoombwa sigara na Mzungu nilidhani ni utani. Nilipompatia alinishukuru nusura anilambe miguu.Kumbe yule Mzungu alikuwa ombaomba kama rafiki yangu Matonya (japo ile staili ya Matonya inaweza kuwa kali kuliko zote ulimwenguni).Nilipokutana kwa mara ya pili na jamaa yule alieniomba sigara ,ambapo safari hii aliniomba pauni moja,ndipo nilipogundua huenda akawa ni ombaomba kweli.Uthibitisho niliupata nilipokutana nae kwa mara ya tatu lakini safari hiyo nikiwa na rafiki yangu mmoja Mghana ambae alikuwa hapo Ughaibuni kabla yangu.Huyo muumuu wa Came Nkrumah die alienithibitishia kuwa hapo Uingereza kuna ombaomba lukuki.Niliposimulia hadithi hiyo kwa jamaa zangu hapa baadhi walinibishia.Na walikuwa na hoja.”Mbona tunaangalia BBC kila siku na tunaowaona ni wazungu wanaoonekana kuwa hawana shida hata kidogo”,ilikuwa hoja ya mmoja wao.Ukweli ni kwamba hawa wenzetu wanapenda zaidi kuonyesha yale wanayoyaona kuwa yanaleta picha nzuri ya nchi zao.Angalau balaa la Katrina lilisaidia kuwafumbua macho watu kwamba hata huko kwa George Bush kuna masikini kama hapa kwetu,na wamesahaulika.
Kwa hiyo basi,makala hii itawasaidia Watanzania wenzangu kujua mambo mbalimbali-mazuri kwa mabaya-yanayojiri huko Ughaibuni ambayo ni nadra kwa mtu wa kawaida kuyapata.Naahidi wasomaji watukufu kwamba kama ambavyo hamtopenda kukosa nakala za KULIKONI basi ndivyo hamtotaka kukosa uhondo nitakaokuwa nawaandalia kutoka huko nje.Kama azma ya gazeti hili ilivyo-kuupatia umma chakula cha kila wakati-nami nitahakikisha nawapatia mlo wa kila wakati.Labda tofauti itakuwa ni kwamba mlo huo unaandaliwa kutoka nje.Lakini ugali si ugali tu.Ukitoka Uingreza au ukipikwa Manzese si bado ni ugali.Cha msingi upikwe kwa kuzingatia kanuni za upishi wa ugali.Pengine kingine ni kwamba mapishi haya ya kutoka nje yatakuwa tofauti ni yale uliyoyazowea.Haya yatamlenga mlaji wa kawaida.Kwa ufafanuzi,ni kwamba utofauti wa makala hii ni kwamba kama lilivyo gazeti lenyewe,itakuwa tofauti ni makala mlizozizowea katika baadhi ya magazeti ya kila wiki.Na tofauti yenyewe ni kwamba kipaumbele kitawekwa kwa watu wa kawaida na mambo ya politiki yatakuja tu pale yanapowagusa watu wa kawaida.
Basi hadi Ijumma ijayo,nawaomba make mkao wa Kula ambapo makala motomoto zitaanza kuwajia kutoka Ughaibuni.Ahadi yangu na ya timu nzima ya KULIKONI ni kubeba sauti za watu wa kawaida,na kwahakika hilo linawezekana.
Alamsiki
Monday, 17 April 2006
11:19
Unknown
BBC, CNN
No comments
Related Posts:
MACHAFUKO NCHINI KWENYA: UKABILA AU MAPAMBANO YA KITABAKA (MAKALA NDANI YA GAZETI LA MTANZANIA) Makala yangu hii ilitoka katika toleo la jana la gazeti la MtanzaniaMiongoni mwa adha za kumiliki runinga hapa Uingereza ni kuilipia ada ya leseni (TV Licence Fee).Ada hiyo kwa kiasi kikubwa hutumika kuendesha BBC ambalo ni … Read More
KAMA UNA MUDA,CHEKI DOCUMENTARY HII KUHUSU MAISHA NDANI YA SAN QUENTIN PRISONMuda mfupi uliopita nilikuwa naangalia documentary moja ya Louis Theroux kuhusu maisha ndani ya San Quentin State Prison,one of the toughest and most dangerous in the U.S. of A.Katika documentary hiyo iliyoonyeshwa BBC2 Louis… Read More
"WAZUNGU" WALIZWA NA UPATU (PONZI SCHEME)Watanzania wengi wanapenda habari.Na siku hizi vyombo vya habari viko vya kumwaga.Hata hivyo,upatikanaji wa habari za uhakika bado ni tatizo.Kwanza,wanahabari wengi wa huko nyumbani wanapendelea zaidi kuripoti habari badala y… Read More
BBC RADIO HOST SACKED AFTER A CALL TO TAXI FIRM REQUESTING A NON-ASIAN DRIVERA BBC Radio presenter has been sacked following a 'racist' call to a taxi firm, in which she requested a 'non-Asian' driver.Sam Mason told the operator that 'a guy with a turban would freak her daughter out' insisting they … Read More
KULIKONI UGHAIBUNI 1KULIKONI UGHAIBUNIAsalam aleykum waungwana.Nadhani kabla ya kubwabwaja mengi ingekuwa ni vema tukatambuana. Lakini kabla ya hapo, ngoja nikunong’oneze kitu kimoja kuhusu gazeti hili mwanana la KULIKONI.Hili sio gazeti la kawa… Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment