Naamini wengi wenu mnakikumbuka kibao cha "Ingekuwa Vipi" cha wasanii Jay-Mo na Mwanafalsafa.Nakipenda,sio kwa beats zake pekee,bali pia kimebeba ujumbe mzito wenye maswali mazito.Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la Raia Mwema imeanza kwa kunukuu verse moja ya wimbo huo,lengo likiwa sio uchambuzi wa muziki bali kufanya tafakuri kuhusu mwelekeo wa mambo katika nchi yetu.Tangu nifike hapa nyumbani takriban wiki tatu zilizopita,nimekutana na watu kadhaa ambao wamekuwa wakidai BORA MKOLONI ARUDI KUTUTAWALA.Aliyenisukuma zaidi kujadili suala hili ni abiria mwenzangu niliyesafiri nae katika chumba cha "daraja la kwanza" cha TAZARA,ambaye nae alidai kwamba "Bora Mkoloni arudi" baada ya adha lukuki zilizotupata katika safari yetu.Mie nadhani bora Wachina warejeshewe TAZARA kwani sie Waswahili imetushinda.Hilo la Mkoloni kurudi sina hakika nalo sana,ila ni dhahiri kwamba kuna wanaharamu wanaotutesa mara 100 zaidi ya walivyofanya wakoloni.By the way,wakoloni hawakuwa Watanzania wenzetu,lakini hawa washenzi wanaotufisadi na kulimbikiza fedha (wenyewe wanaita vijisenti) huko nje ni watu tuliozaliwa nao nchi moja iitwayo Tanzania.Makala yangu hiyo imehitimishwa kwa onyo kwa CCM kwamba ikiendeleza porojo zake za Maisha Bora kwa kila Mtanzania (or did they mean "kwa kila fisadi"?) basi wasishangae wakikutana na yaliyowakuta KANU huko Kenya.Ukisikia wananchi wanatamani Mkoloni arudi basi hizo ni dalili kuwa wamechoshwa na porojo za watawala.Pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti la Raia Mwema,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA
Pia kuna picha kadhaa kutoka maeneo mbalimbali ya Bongo.
Nadhani kuna wanaoikumbuka joint moja ya maeneo ya Namanga kuelekea Msasani iliyokuwa ikijulikana kwa jina la Studi Becker.Sasa hivi inaitwa New Angel.Pengine kwa vile ni ya "Malaika Mpya" ndio maana toilets zao ziko kizani kama inavyoonekana (au isivyoonekana?) katika picha.
Picha hizi nzuri (hapo juu na zinazofuata chini) zimepigwa na dada mmoja mrembo wa Hoteli ya Kempinski (ameomba jina na sura yake vihifadhiwe) kutoka ghorofa ya sita ya hoteli hiyo.Dada huyo mdau wa blogu hii anadai amepatwa na wazo la kupiga na kunitumia picha hizo baada ya kuona kile "kimbembe cha zule" cha picha za matope ya barabara ya Ifakara.Picha zote zinaonyesha mandhari ya bandari ya Dar es Salaam,minus ufisadi wa Mamlaka ya Bandari na TICTS.