Wednesday, 4 February 2009


Wafanyakazi wote wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wameachishwa kazi na kulipwa mafao yao kuanzia jana ili kupisha mpango wa kuliboresha shirika hilo litoe huduma kwa ufanisi.

Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya NIC, Dk. Hamis Kibola jana, ilisema kuwa shirika hilo litaajiri wafanyakazi wapya kulingana na mahitaji ya shirika. Dk. Kibola alisema leo na kesho shirika hilo halitatoa huduma ili kupisha kazi ya kuajiri upya na huduma itarejea tena Jumatatu ijayo wakati mchakato wa kuajiri utakapokuwa umekamilika.

Inakadiriwa wafanyakazi 500 wataachishwa kazi na shirika hilo litaajiri wafanyakazi wachache wenye ufanisi na wanaoweza kuleta changamoto mpya ya kulifanya shirika hilo liwe na tija na kuhimili ushindani wa biashara ya bima.

Dk. Kibola alisema mpango huo wa kuwaachisha kazi ni kwa mujibu wa makubaliano kati ya wafanyakazi kupitia chama chao TUICO –NIC, Serikali na Shirika la Kusimamia Mali za Serikali (CHC).

Alisema hadi jana taratibu za kuajiri upya zilikuwa zimekamilika, lakini hakusema ni kiasi gani kilichotumika kuwalipa wafanyakazi, lakini taarifa za NIC kwa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi mwaka jana zilionyesha shirika hilo limetenga Sh bilioni 5.2 kwa ajili ya malipo ya wafanyakazi. Mwaka jana, Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo alisema serikali itauza hisa nyingi za NIC kwa wananchi pindi shirika hilo litakapoweza kusimama lenyewe miaka michache ijayo.

Akizungumza baada ya mkutano wa 12 wa Siku ya Bima, Novemba mwaka jana, Mkulo alisema serikali itapeleka bungeni mabadiliko ya sheria mbalimbali ili kuibadilisha NIC kutoka kwenye shirika kuwa kampuni na serikali iongeze fedha zaidi kuliokoa ili baadaye hisa zake ziuzwe kwa wananchi na lijiendeshe kwa faida. “Tayari mchakato wote umeshakamilika wa kuliboresha shirika hili ambapo lengo la serikali si kuliuza, bali kuliendeleza,” alisema Mkulo.

Related Posts:

  • SHRIKA LA BIMA LAACHISHA KAZI WAFANYAKAZI WOTEWafanyakazi wote wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) wameachishwa kazi na kulipwa mafao yao kuanzia jana ili kupisha mpango wa kuliboresha shirika hilo litoe huduma kwa ufanisi.Taarifa iliyotolewa na Mwenyekiti wa Bodi ya NIC, … Read More
  • HE! MAKUBWA HAYA: BARABARA NAZO MBIONI KUBINAFSISHWA!?MSIMU WA MVUA,BARABARA YA KWENDA KWETU IFAKARA NI MITHILI YA SWIMMING POOL YA MATOPE.SIJUI NA HII NAYO WAWEKEZAJI WATATAKA IBINAFSISHWE.HOFU YANGU WANAWEZA WAKAICHUKUA KISHA WAKAIGEUZA SHAMBA LA MPUNGA,SASA SIJUI AKINA SIE TU… Read More
  • SAUDI INVESTORS EYEING LEASING TZ FARMLANDRiyadh, April 16 - Saudi investors have asked Tanzania if they can lease 500,000 hectares of farmland mainly for rice and wheat farming as part of a plan to secure food supplies for the desert kingdom, officials said.Senior o… Read More

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget