RAIS Jakaya Kikwete amesema ana majina ya watu wa kitengo cha maktaba cha Bandari ya Dar es salaam wanaofanya ufisadi unaolikosesha taifa mamilioni ya fedha na kuahidi kuyakabidhi kwa wahusika ili washughulikiwe. Kikwete alisema hayo jana baada ya kufanya ziara ya kushitukiza kwenye Bandari ya Dar es salaam kukagua utekelezaji wa maagizo aliyoyatoa Januari 15 mwaka huu kwa wakuu wa Mamlaka ya Bandari (TPA).
Alisema kitengo cha maktaba kimekuwa kikifanya mchezo mchafu bandarini hapo kwa kushirikiana na wasafirishaji na kwamba, vibarua vya watu wa kitengo hicho viko hatarini.
“Waambieni watu wa kitengo cha maktaba kuwa mchezo wao unajulikana na orodha ya majina yao inajulikana, lakini bado kuwaumbua tu,” alisema Kikwete baada ya kumaliza ziara yake.
“Ndugu zangu sitawataja hadharani wala kwenye magazeti, bali nitakachofanya nitawaletea orodha ya majina, muwafukuze kazi. Kama wameshindwa kazi tutaleta watu wengine ambao wako tayari kufanya kazi kwa uaminifu.”
Alisema watu hao wamekuwa wakiwasiliana na wasafirishaji na kufanya ujanja wakati wa kujaza fomu za makontena yanayoingia nchini kwa kuandika mizigo tofauti na ile iliyomo ndani ya makontena hayo, ili yasipitishwe katika mashine ya uchunguzi ...ENDELEA
CHANZO: Mwananchi
HIVI KAMA MAJINA YA MAFISADI YANAJULIKANA (NA KINACHOSUBIRIWA NI "KUWAUMBUA") KWANINI WASICHUKULIWE HATUA?WAZIRI MWENYE MAMLAKA NA BANDARI YUKO WAPI NA ANAFANYA NINI?MKURUGENZI NA BODI YA BANDARI WANAFANYA NINI?NA,HIVI HATUA MWAFAKA DHIDI YA MAFISADI NI KUWAUMBUA AU KUWAFIKISHA MBELE YA VYOMBO VYA SHERIA?
0 comments:
Post a Comment