Friday, 27 November 2009


Uwajibikaji uliotukuka au kupitiliza majukumu?Who cares as long as we are kept safe.Katika magazeti mbalimbali ya hapa Uingereza kuna habari kwamba Waziri wa Usalama,Lord West,amehenyeshwa na askari baada ya kusimamishwa na kusachiwa (stop and search) kwa mujibu wa sheria za kuzuia ugaidi.Uzuri wa hawa wenzetu ni ile tabia ya "hapendwi mtu",yaani kutekeleza majukumu kwa maadili badala ya kuangalia urembo au haiba.

Sidhani kama kuna haja ya kuwakumbusha madudu ya Waziri wetu mwenye jukumu la utawala bora (which includes mapambano dhidi ya ufisadi) alivyojitokeza kuwa mama mlezi wa mafisadi.Ni katika tawala ambazo mtu anaweza kuropoka chochote na akaendelea kuitwa mheshimiwa ndipo hadi muda huu Sophia Simba anaendelea na wadhifa unaohitaji uadilifu wa hali ya juu,including umakini katika kauli.

Sasa kama askari wanaweza kudili na bosi wao kama raia mwingine iweje basi waziri wetu mwenye dhamana ya kuhakikisha mafisadi "wananyea ndoo" gerezani awe mtetezi wao mkubwa?Jibu jepesi ni kwamba Waziri Simba anapata jeuri hiyo kutoka mahala flani.Na si yeye tu bali viongozi wetu wengi wametokea kuwa na jeuri ya ajabu kwa vile wanafahamu fika hakuna wa kuwaadhibu.Kama aliyekuteua haonekani kuerwa na madudu yako why would you care kurekebisha madudu hayo?

Unfortunately,lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa watendaji wabovu badala ya kumkalia kooni aliyewapa fursa ya kuweka hadharani udhaifu wao.Ni kama katika futiboli;kocha akipanga kikosi kibovu basi lawama zaidi zitaelekezwa kwake kwa vile kikosi alichopanga hakijichagua chenyewe.Na ndio maana hivi majuzi kocha wa timu ya taifa ya Scotland alijikuta akifungashiwa virago vyake baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye kampeni yake ya kushiriki Kombe la Dunia hapo mwakani.

Na ukidhani mie ni malalamishi nisiye na hoja basi SOMA HAPA uelewe chanzo cha tatizo kiko wapi.

Related Posts:

  • HATIMAYE WAZIRI CHIKAWE AKIRI: JK HAWEZI KUWABANA MAFISADIWaziri Chikawe asema Kikwete hawezi kuwabana mafisadi*Asema Rostam, Dk Hoseah hawakamatiki*Asikitika DPP, DK Hoseah kuparuanaNa Leon BahatiWAZIRI wa Katiba na Sheria, Mathias Chikawe amesema Rais Jakaya Kikwete hana uwezo kut… Read More
  • KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA 2010Ahadi za urais 2005 zamtesa Kikwete uchaguzi wa mwakaniRais Jakaya Kikwet, mzigo mzito wa ahadi zake za mwaka 2005 unamkabili uchaguzi ujao 2010.Na Mwandishi WetuMIEZI michache ikiwa imebaki kabla ya kuanza kwenda kwa wananch… Read More
  • WAZIRI CHIKAWE AZIDI KUTOA KAULI TATAWaziri wa Sheria adai Bunge la sasa halina ubavu kwa serikaliNa Leon BahatiWAZIRI wa Sheria na Katiba, Mathias Chikawe amezidi kutoa kauli tata baada ya kuligeukia Bunge la Jamhuri ya Muungano, akisema halina nguvu ya kuilazi… Read More
  • Utashi Unahitajika Ili Tuushinde UfisadiMkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia Rushwa TAKUKURU Dr. Edward Hosea akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua mkutano mkuu wa Mwaka wa taasisi hiyo.Picha kwa hisani ya MJENGWAHivi karibuni,uongozi wa kampuni ya maga… Read More
  • PROFESA SHIVJI AMPA DARASA WAZIRI CHIKAWEProf Shivji asema Rais Kikwete ana mamlaka kisheria kuwabana mafisadi*WENGINE WAMTAKA WAZIRI CHIKAWE AACHE KUKURUPUKANa Sadick MtulyaSIKU moja baada ya Waziri wa Sheria na Katiba Mathias Chikawe kusema Rais Jakaya Kikwete haw… Read More

2 comments:

  1. kuna haja ya kuanzisha shule ya kusomea uwaziri!

    ReplyDelete
  2. Kiburi inatoka wapi! Anayemwezesha huyu waziri kuwajibika kinyume na kanuni na taratibu zilizopo basi wote wawajibika, na iwapo kama hakuna wa kufanya hivyo watanzania wapiga kura waonyeshe hasira zao kupitia chaguzi za kisiasa kwa kuacha kupigia kura wavunja sheria na watenda uahalifu

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget