Wednesday, 8 December 2010
- 19:11
- Unknown
- BIRTHDAY
- 6 comments
Leo ni siku yangu ya kuzaliwa.Kwanza sina budi kumshukuru Muumba kwa kunileta duniani tarehe 9 Desemba miaka thelathini na kitu iliyopita (30 plus yrs ago).Pili,nawashukuru wazazi wangu wapendwa,Baba Mzee Philemon Chahali na Mama mpendwa Marehemu Adelina Mapango (Mungu Akulaze Mahali Pema Peponi Amen).Tatu,nawashukuru wanafamilia wenzangu katika familia yetu-kaka na dada na wadogo zangu.Na nne nawashukuru wale woote nilio/ninaofahamiana nao katika muda wote huo.
Makala hii sio kwa ajili ya kuzungumzia birthday yangu.Kwa bahati nzuri (au mbaya?) tarehe ya siku yangu ya kuzaliwa inarandana na tarehe ya Uhuru wa Tanzania.Inapendeza kusherehekea siku ya kuzaliwa inayoambatana na tukio jingine muhimu la kihistoria.Lakini historia pekee sio muhimu kama haina manufaa stahili kwa jamii husika.
Wakati tunaadhimisha miaka 49 ya uhuru wa Tanzania tunalazimika kujiuliza mara mbili mbili umuhimu wa uhuru huo.Je uhuru wetu uliishia tu kwenye kumwondoa mkoloni au ulipaswa kutuweka huru katika nyanja zote?Naamini hilo la pili ndilo dhamini na maana halisi ya uhuru: uhuru wa kupata huduma tunazostahili (elimu,afya,maji,barabara,umeme,maji,nk),uhuru wa kuchagua na kukataa viongozi kwa njia halali (sio uchakachuaji),uhuru wa habari pamoja na uhuru wa kutoa maoni hata kama habari na maoni hayo hayawapendezi watawala),uhuru wa kuabudu pasipo kuwa kikwazo kwa waumini wa imani tofauti,uhuru wa kuishi ikiwa ni pamoja na kuepusha vifo vinavyoepukika (ajali zinazochangiwa na ufisadi wa polisi trafiki,ukosefu wa madawa unaochangiwa na ufisadi kwenye misaada/manunuzi kwenye sekta ya afya),uhuru wa kuishi bila kubaguliwa (mafisadi vs walalahoi,vigogo vs makabwela,watawala vs watawaliwa,nk),na KILA UHURU ambao ni HAKI ya msingi kwa mwanadamu.
Japo haipendezi kuzungumizia,ukweli mchungu ni kwamba miaka 49 ya uhuru wetu inatuacha na maswali mengi kuliko majibu.Na kama mzaha mbaya,siku chache kabla ya kusherehekea umri huu tumeshuhudia namna uchaguzi mkuu uliojaa kasoro lukuki na uchakachuaji ukitupatia "serikali mpya" (denti yuleyule lakini katika yuniformu mpya...ni dhahiri kuwa kama denti huyo ni "kichwa panzi" yunifomu hizo mpya hazitomsaidia lolote kimasomo).Na siku chache zilizopita tumeshindiliwa msumari wenye kutu katika kidonda kibichi pale kampuni ya Dowans "iliposhinda" kesi dhidi ya Tanesco (serikali) na sasa inastahili kulipwa mabilioni ya shilingi.Hiyo ndio salamu ya happy birthday kutoka kwa mafisadi.Tukio hilo halina tofauti na vitendo vya vibaka (hususan mitaa ya Mwananyamala karibu na hospitali kama unatokea Mwananyamala Kwa Kopa) ambapo vibaka wanakupiga roba ya mbao kisha wanakupigia ukelele wa "mwiz,mwizi".Kuporwa uporwe,na kipigo ukipate.Naam,ndivyo Dowans na wamiliki wake mafisadi wanavyotutenda.Huu ni ubakaji wa hadharani tena mchana kweupe.
Anyway,mie nasherehekea birthday yangu kibinafsi.Kama kuna mafanikio au mapungufu yaliyojiri katika miaka thelatini na kitu tangu nizaliwe yanabaki kuwa masuala binafsi.Lakini kwa vile Tanzania ni yetu sote,hatuna budi kusherehekea birthday yake kwa kufanya tafakuri kuhusu mantiki nzima ya "kuzaliwa" na kuwepo kwake.Ni kwa namna hiyo tu ndipo tutaweza kuendelea kusherehekea siku kama ya leo kwa "amani na utulivu" (tukumbuke mwenye njaa hana amani kama ilivyo kwa mgonjwa asiyeweza kupewa tiba stahili,au msafiri asiyeweza kufika aendako kwa vile barabara hazipitiki,au mlipakodi anayekwamishwa kimaisha na mgao usioisha wa maji na umeme,au mlalahoi asiye na haki mbele ya matakwa ya vigogo na mafisadi).
Happy birthday to me.Happy birthday Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Isn't it awesome sharing your birthday with a country? lol! Jokes!
ReplyDeleteHappy birthday man! and many more to come, bless ya! x
Happy birthday to you and our beloved nation.
ReplyDeleteHappY Birthday Mkuu!
ReplyDeleteAsanteni sana wakuu,Melkiory na Simon.
ReplyDeleteHongera sana Mkuu kwa siku Yako ya Leo Mungu akujalie zaid na zidi afya njema na Maisha marefu zaidi
ReplyDeleteHappy Birth day Evarist. May God grant you more days to live as you successfully fulfill whatever you have dreamed about.
ReplyDelete