Thursday, 24 February 2011


Katika harakati zake duni za kujinasua uhusika wake katika suala la ujambazi wa Dowans,Rais Jakaya Kikwete alijaribu kuwahadaa Watanzania kwa kudai,pamoja na mambo mengine,kuwa "hawajui wamiliki wa Dowans".

Na kwa bahati nzuri kwake,vyombo vyetu vya habari vikaishia kumnukuu tu.Lakini kwa minajili ya kufupisha makala hii(na kupunguza maumivu yanayotokanayo) tuweke kando kuangalia namna Kikwete alivyotengeneza mazingira ya ujio wa Dowans kupitia majambazi wengine wa Richmond.Hapa namaanisha kauli yake kuwa tatizo la umeme lingekuwa historia baada ya ujio wa mitambo ya kuzalisha umeme kutoka Marekani (na tukaishia kuletewa mitambo garasa)

Hatimaye mwarabu Adawi aliyekimbia ukombozi wa Mzanzibari,amediriki kuja na kutufanyia kila aina ya vituko (kukataa kupigwa picha,nk) na kutangaza hadharani kuwa yeye ndio mmiliki wa Dowans.Na kama kututukana Watanzania,akadai kuwa anaweza kuangalia uwezekano wa kupunguza FIDIA ANAYOPASWA KULIPWA KWA KUTUIBIA (yale yale ya vibaka wanaomkaba mtu kisha kumpigia ukelele wa "mwizi,mwizi...")

Adawi ambaye Kikwete anadai hamjui (japo anamjua sana kwani wana mahusiano ya "kifamilia")ameweza kutia mguu Ikulu na kuongea na Makamu wa Rais Gharib Bilali (anayekaimu urais katika kipindi hiki ambacho Kikwete yuko kwenye mizunguko yake).

Japo tunajua kuwa Ikulu yetu imegeuzwa kijiwe cha mafisadi ambao wana uhuru wa kutembelea mahala hapo patakatifu kila wanapojisikia lakini kwa Adawi kupewa nafasi ya kukutana na Rais (kwa maana ya anayekaimu nafasi hiyo),na mkutano huo kufanywa siri,inaashiria kuwa Kikwete na serikali yake sio tu anamjua Adawi bali pia anamtumikia.

Sintashangaa kusikia kuwa Kikwete aliamua kwenda Mauritania ili kumwezesha Adawi afanye uhuni wake kisha ahitimishe ziara yake kwa maongezi na kaimu wa Kikwete (Gharib Bilali).Na sintoshangaa kusikia kwamba kabla ya kurejea Tanzania,maswahiba hao wawili (Kikwete na Adawi) wakakutana faragha kujadili kuendeleza ujambazi wa Dowans.

Na hata tukiweka kando ujio wa Adawi,kauli ya Kikwete kuwa hawajui wamiliki wa Dowans ilhali majina ya wamiliki hao yapo BRELA (na Waziri Ngeleja alishayaweka hadharani kabla Kikwete hajatoa utetezi wake feki) inatosha kuwafahamisha Watanzania kuwa Rais wao ameshindwa kazi.How come Waziri ajue kile ambacho Rais hakijui?Je kama anashindwa kujua jambo dogo tu kama rekodi ndogo tu iliyopo BRELA atawezaje kujua na hatimaye kushughulikia matatizo ya Watanzania takriban milioni 50?

Tusipofumbuka macho kama wenzetu wa Tunisia,Misri,Libya na kwingineko wanakopambana na tawala dhalimu tunaweza kuishia kuwa koloni la Adawi,yaani mwarabu huyo kuongoza nchi yetu kwa kutumia remote control in the form of Kikwete.

Related Posts:

  • Hatimaye Serikali Yaruhusu Gazeti Lake la Habari Leo Kumchafua Dkt Slaa.Lamuita "Padri Msomi"Inaudhi na kukasirisha kuona gazeti la serikali,Habari Leo,likijipachika jukumu la kumuua kisiasa mgombea wa Chadema Dokta Wilbroad Slaa kama ambavyo imekuwa ikifanywa na magazeti ya Habari Corporation na Changamoto,na mengin… Read More
  • KULIKONI UGHAIBUNI-11KULIKONI UGHAIBUNI:Asalam aleykum wasomaji wapendwa wa gazeti hili.Leo tuzungumzie muziki.Muda mfupi uliopita nilikuwa nasoma makala flani kumhusu msanii wa kizazi kipya Albert Mangwea.Yalikuwa ni mahojiano kati ya msaanii hu… Read More
  • Kikwete Atuambie Uhuni Huu wa Mgao wa Umeme Hadi Lini?Majuzi,msomaji mmoja wa blogu hii alinitumia maoni ambapo pamoja na mambo mengine aliashiria kuwa nina chuki dhidi ya Rais Jakaya Kikwete.Msomaji huyo aliyejitambulisha kuwa mkazi wa hapa Glasgow alidai (namnukuu) "...I know … Read More
  • KULIKONI UGHAIBUNI-15KULIKONI UGHAIBUNI:Asalam aleykum,Mwaka juzi gazeti maarufu duniani la TIME lilimtangaza George W.Bush kuwa “mtu wa mwaka (2004)” –au “Person of the Year” kwa lugha ya kwa mama.Katika uchambuzi wake kuhusu Bush,gazeti hilo li… Read More
  • KULIKONI UGHAIBUNI-20KULIKONI UGHAIBUNI-21Asalam aleykum,Leo nina jambo muhimu sana kuhusiana na maslahi ya Taifa letu.Nawaomba wasomaji wapendwa tuwe pamoja kwa makini ili tusipoteane njiani na hatimaye kuleta tafsiri potofu ya ninachotaka kuzun… Read More

1 comment:

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget