Tuesday, 31 January 2012
Rais Jakaya Kikwete amekiri kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza kufuatia kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa Rais ameridhiria nyongeza ya posho za Wabunge.Rais alisema hayo katika majadiliano kati yangu na yeye kupitia mtandao wa Twitter kama inavyoonyesha picha hapa juu na hapa chini
Awali,Rais Kikwete alifafanua kuwa ni kweli alitoa maelekezo kuhusu suala la posho hizo lakini maelekezo hayo hayakuwa kuridhia jambo hilo.Kadhalika,Rais alibainisha kwamba alikubali haja ya kuangalia upya posho za wabunge na aliwataka wabunge kutumia hekima na busara katika kutafakari.Vilevile aliwataka wabunge kutumia Kikao cha Februari cha Bunge kulizungumzia upya suala hili,na kusistiza ni muhimu.Picha ifuatayo inaonyesha maelezo hayo ya Rais Kikwete kwenye mtandao wa Twitter.
Jana,gazeti la Mwananchi lilikuwa na habari iliyobeba kichwa 'JK ABARIKI POSHO MPYA ZA WABUNGE' ambapo pamoja na mambo mengine habari hiyo ilieleza kuwa Waziri Mkuu Pinda amesema kuwa tayari Rais Kikwete amesaini kuridhia ongezeko la posho za vikao (sitting alllowances) kwa wabunge kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 200,000 kwa siku.Picha ifuatayo inaonyesha sehemu ya habari hiyo:
Hata hivyo,mapema leo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ilitoa taarifa ya maandishi kukanusha habari hizo, kama inavyosomeka hapa chini
Taarifa Ya Ikulu
Blogu hii inaendelea kufatilia kwa karibu kuhusu suala hilo.
Related Posts:
Kilio Kumwokoa tena Pinda?Anyway,yeye na Mawaziri Wake ni Dalili tu,Chanzo ni KikweteWaziri Mkuu Pinda akifanya usanii wa kulia bungeni katika sakata la maalbino.Je hatorejea tena mbinu hii?Tusiume maneno.Tanzania hivi sasa inayomba kwa vile Rais tuliye nae,Jakaya Kikwete,ni mithili ya mtu asiyejua kwanini Wa… Read More
Tafakuri ya Nova Kambota: Pinda Kubali Kufa Ili Uione PepoNa Nova Kambota,Namkumbuka mwanamuziki wa kizazi kipya Seleman Msindi maarufu kama Afande sele na kile kibao chake cha “Darubini kali” anapohoji “kama unapenda pepo kwanini uogope kifo?”Tungo hii kwa namna ya pekee inamgusa w… Read More
Pinda Kumfuata Lowassa?Pinda kumfuata Lowassa• HATMA YA MAWAZIRI WATANO MIKONONI MWA JKna Mwandishi wetuWAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda, sasa yuko katika hatari ya kuondolewa madarakani kwa kupigiwa kura ya kutokuwa na imani naye kufuatia tuhuma nzito … Read More
Familia ya PINDA Yahamia CHADEMA? (PICHA)A PICTURE COULD TELL A MILLION WORDS: Dogo anaonekana akitoa alama ya V (for victory over mafisadi) huku Mtoto wa Mkulima akionekana kupigwa na bumbuwazi! CHANZO: Jamii Forums… Read More
EXCLUSIVE TO KULIKONI UGHAIBUNI: Rais Kikwete Azungumzia Kauli ya Pinda Kuhusu Posho za WabungeRais Jakaya Kikwete amekiri kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza kufuatia kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa Rais ameridhiria nyongeza ya posho za Wabunge.Rais alisema hayo katika majadiliano kati yangu na yeye kupitia mt… Read More
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment