Sunday, 30 September 2012
Thursday, 27 September 2012
- 02:20
- Unknown
- RAIA MWEMA
- No comments
NINAAMINI takriban kila msomaji wa magazeti ameshawahi kukumbana na sentensi hii inayokera ya “jina linahifadhiwa kwa sasa.”
Kinachokera si tu kuhifadhiwa kwa jina la mhusika mkuu katika habari bali ukweli kwamba mara nyingi habari husika hugeuka kuwa mithili ya mtihani uliojaa mafumbo, na pasipo msomaji “kujumlisha 2 na 2 kupata 4” hakuna uwezekano wa habari hiyo kuleta maana yoyote.
Mifano ni mingi lakini mfano mwafaka ni katika habari ambayo nitaizungumzia pia kwenye makala hii. Kwa siku kadhaa, magazeti mbalimbali yalikuwa yakiripoti taarifa kuhusu mke wa kigogo wa Jeshi la Polisi, ambapo utambulisho wa kigogo huyo na mkewe umebaki kuwa “umehifadhiwa,” akihusishwa na utapeli wa mamilioni ya shilingi kwa ahadi ya kuwapatia watu ajira kwenye vyombo vya dola.
Kabla ya kujadili tukio hilo la utapeli wa aina yake, tuendelee na mjadala wa tabia inayozidi kuota mizizi kwenye magazeti yetu ya “jina limehifadhiwa.” Japo uelewa wangu wa sheria ya kumkashifu mtu/taasisi (Defamation Law) ni wa wastani, siku zote kama mwandishi wa blogu na makala nimekuwa makini kuhakikisha kuwa ninapotaja jina la mtu au taasisi kwenye habari husika, nina uhakika na ushahidi ninao.
Kwa msingi huo, sioni haja ya kutumia sentensi “jina linahifadhiwa kwa sasa” (na mara nyingi hiyo ‘sasa’ hugeuka kuwa ‘milele’) kwa sababu iwapo mtajwa katika andiko husika ataamua kunipeleka mahakamani kwa madai ya kumkashifu, nitapambana naye vilivyo.
Nadhani sababu kubwa ya waandishi wetu kusaka hifadhi ya “jina linahifadhiwa kwa sasa” kwenye kuficha majina ya wahusika katika maandiko yao ni uoga wa kuburuzwa mahakamani kwa madai ya kashfa dhidi ya mtajwa. Na sababu pekee inavyoweza kusababisha uoga huo ni ukosefu wa facts au ushahidi kamili.
Ni wazi kwamba sheria ipo upande wa mwandishi pindi anapoandika habari ambayo imejitosheleza, kwa maana ya kuwa na ushahidi usiopingika kuhusu mtajwa katika habari husika.
Kimsingi, taaluma ya uandishi wa habari inashabihiana kwa kiasi kikubwa na ushushushu katika namna habari inayotafutwa. Katika taaluma zote lengo ni kupata habari kwa minajili ya kuziwasilisha sehemu fulani: kwa msomaji kwa upande wa wanahabari, na kwa mwajiri kwa upande wa mashushushu.
Tofauti za msingi katika utafutaji na matumizi ya habari ni kwamba wakati mara nyingi wanahabari wanapaswa kuwa ‘wazi’ wanaposaka habari (kupata habari kwa udanganyifu kunaweza kuwa kosa la jinai), takriban mara zote mashushushu husaka habari kwa kificho (na kwa mujibu wa sheria, shushushu kujiweka wazi-au kujiumbua-ni kosa).
Kwa upande wa matumizi ya habari zilizopatikana, wanahabari wanatarajiwa kuziwasilisha kwa msomaji (tukiweka kando taratibu za kiuhariri ndani ya chombo habari husika) ilhali kwa mashushushu habari, ambayo wakati huo hugeuka kuwa taarifa, huwasilishwa kwa chombo husika kwa hatua nyinginezo.
Kwa hiyo, tofauti ya kimsingi ya mwanahabari na shushushu ipo zaidi kwenye ‘habari’ na ‘taarifa.’ Wakati habari ni kitu cha wazi na kwa ajili ya matumizi ya umma, taarifa ni kitu cha siri na ni kwa ajili ya matumizi ya taasisi ya kishushushu tu.
Sasa tunachoshuhudia katika uandishi wetu wa “jina limehifadhiwa kwa sasa” ni mithili ya ‘mchanyato wa habari na taarifa,’ kwa maana ya ‘kuwasilisha habari nusu kama mwanahabari lakini pia nusu kama shushushu - nusu wazi nusu siri.’
Ni adhabu kubwa kwa msomaji anapokutana na habari iliyoandikwa kwa mfumo huu “kigogo mmoja (jina linahifadhiwa) wa taasisi moja (jina linahifadhiwa) anadaiwa kulimbikiza fedha zilizopatikana kifisadi katika nchi moja (jina linahifadhiwa).” Kimsingi, habari hii haina umuhimu zaidi ya kuuza gazeti husika na kusumbua ubongo wa msomaji.
Kwa nini mwandishi husika asihakikishe anapata facts zote kuhusu mhusika katika habari hiyo kabla ya kukurupuka kuiripoti nusu nusu? Ninatambua kuwa baadhi ya wanahabari wanaweza kujitetea kuwa wanafanya hivyo kwa minajili ya ‘kumshtua mhusika’ kwamba matendo yake yanafahamika lakini kimsingi hilo si jukumu la chombo cha habari. Kama kuna maovu yasiyoandikika gazetini basi yawasilishwe kwa taasisi za dola badala ya kuwachosa wasomaji na ‘habari za kificho.’
Turejee kwenye sakata la utapeli unaodaiwa kufanywa na mke wa kigogo wa polisi ambao kwa pamoja “majina yao yameendelea kuhifadhiwa” na vyombo vya habari vilivyokuwa vinaripoti habari hiyo.
Awali iliripotiwa kuwa mke wa kigogo huyo alijipatia mamilioni ya shilingi kwa ahadi ya kuwapatia ajira vijana 120 kwenye Jeshi la Polisi, Idara ya Usalama wa Taifa na Taasisi ya Kuzuia na Kudhibiti Rushwa (TAKUKURU).
Habari zaidi zilizeleza kuwa Jeshi la Polisi lilikuwa likimlinda mke huyo wa kigogo (na hii si ajabu kwani yeyote anayefahamu utendaji kazi wa vyombo vyetu vya dola anatambua kuwa viongozi wake na watu wanaowahusu ni miungu-watu wasiopaswa kusumbuliwa kwa aina yoyote ile).
Kwa mantiki hiyo, Polisi kumlinda mke wa kigogo wa jeshi hilo ni jambo la kutarajiwa japo si sahihi.
Baadaye ikaripotiwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Usalama wa Taifa Othman Rashid amelitaka Jeshi la Polisi kumkamata na kumchukulia hatua mwanamke huyo. Katika hatua ya nadra mno, Othman alisema (ninanukuu) “Nimewasiliana na IGP (Said) Mwema ili aweze kunipa ufafanuzi kuhusu mke wa kigogo huyo, lakini nashukuru amenipa ushirikiano na kuniambia kuwa suala hilo wanalishughulikia kisheria zaidi. Watanipa taarifa pindi watakapokuwa wamekamilisha.”
Lakini katika kile unachoweza kudhani ni tamthiliya isiyopendeza machoni, habari hiyo ikageuka sarakasi na kugeuka kuwa (ninanukuu) “Wakazi wawili wa jijini Dar es Salaam, wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, wakikabiliwa na makosa 12 ya kujipatia sh milioni 102 kwa njia ya udanganyifu wa kuwatafutia vijana kazi katika Idara ya Usalama wa Taifa na Jeshi la Polisi.”
Miongoni mwa wanaotajwa ‘kutapeliwa’ ni mke wa Mkuu wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi, Kamishna Paul Chagonja, aliyatajwa kwa jina moja tu la Happyphania, ambaye inadaiwa alitapeliwa shilingi milioni 5 “kwa madai kuwa ni malipo ya maombi ya usajili wa mafunzo ya POLISI (herufi kubwa kwa sababu maalumu), TAKUKURU na Idara ya Usalama wa Taifa.
Swali la kwanza, hivi kweli inaingia mke wa Kamishna wa Mafunzo na Operesheni wa Jeshi la Polisi atoe fedha kwa ‘matapeli’ ili kumpatia nafasi ya usajili wa mafunzo ya Jeshi la Polisi ambako mumewe si tu ni mmoja wa vigogo wa ngazi za juu bali pia ndiye mwenye dhamana ya MAFUNZO kwa wanaojiunga na jeshi hilo?
Swali la pili, tukiamini kuwa watu hao wawili waliokamatwa na kufungulia mashtaka (wote si wanawake), kwanini basi Mkurugenzi Mkuu wa Usalama wa Taifa alimtaka IGP kushughulikia suala la “mke wa kigogo wa polisi”? Hivi kweli inaingia akilini “mke wa kigogo wa polisi” awe “hao washtakiwa wawili wa kiume”?
Maswali ni mengi, ikiwa ni pamoja na kitendo cha mke wa Kamanda Chagonja kutoa fedha kwa matapeli hao. Pasi kuuma maneno, hivi kutoa fedha kwa ajili ya kupata huduma inayotolewa bure si rushwa? Kwanini basi waliopokea fedha hizo washtakiwe lakini waliotoa fedha wasishtakiwe kwa kutoa rushwa?
Ninatambua uwezekano wa utetezi wa “waliotoa fedha hizo ni victims (majeruhi) wa utapeli.” Hiyo inaweza kuwa kweli tu kwa watu wasiofahamu utaratibu wa kujiunga na taasisi hizo. Sitaki kabisa kuamini kuwa mke wa Kamishna Chagonja hafahamu utaratibu huo hadi kushawishika kutoa fedha kwa washtakiwe hao.
Katika moja ya habari inayomnukuu kigogo wa polisi ambaye kama kawaida jina lake lilihifadhiwa, alisema “…Hata mke wangu ni mmoja wa waliotapeliwa. Alikusudia kuwapeleka wanafamilia watatu akiwemo mtoto wake, mke wa kaka yake na wifi yake ambaye tunamlea.” Mke wa kigogo wa polisi anatapeliwa kuingiza nduguze kwenye jeshi hilohilo analofanya kazi muwewe? Huu ni utani mbaya kabisa.
Kama ilivyo desturi, habari hiyo ndio imeishiwa hapo. Magazeti yaliyokuwa yakiripoti kuhusu mke (jina limehifadhiwa) wa kigogo wa polisi (jina limehifadhiwa) yamemaliza kazi yao na kumwachia kazi msomaji kujumlisha 2 na 2 apate 4.
Na tabia hii ya kukera ya “jina limehifadhiwa” inachangia kuonyesha ubaguzi wa wazi wa kimatabaka. Sijawahi kuona sentensi ya “jina linahifadhiwa” ikitumika kwa tuhuma zinazowahusu walalahoi bali ni kwa vigogo pekee.Ni kwa vile uwezekano wa walalahoi hao kwenda mahakamani kudai wamekashifiwa na gazeti husika ni mdogo au ni kupuuza tu haki zao za kibinadamu?
Mwisho, wakati nina uhakika kuwa majina ya kigogo wa polisi na mkewe anayedaiwa kutapeli yataendelea kuhifadhiwa ‘milele’ (habari yenyewe ni kama imeshakufa kifo cha asili), harakati za kupigania uhuru wa vyombo vya habari hazitozaa matokeo tarajiwa kama vyombo vya habari vitaendeleza kasumba ya “jina linahifadhiwa” ambayo inainyima jamii uhuru wa kuelewa habari husika.
Friday, 21 September 2012
- 14:45
- Unknown
- Muhongo, ZITTO KABWE
- No comments
Zitto Kabwe, Let Dr. Muhongo Do His Job
Energy sector has brought to a disgraceful ending some very promising careers. It has sent packing very powerful and prominent figures in the country’s upper echelons of power; Infarct, at one point, it almost brought down the entire government, when the country’s premiere at the time, faced grand corruption allegations, and was forced to resign. It is our economic sector, by far mired by grand corruptions and ineptness.Reason behind all these has been nothing more than the bogus contracts. There is therefore, a critical need to review and even terminate some of the existing contracts in the eyes of the public, in order to close the loopholes fleecing the country of its wealthThe Kigoma North Legislator, Zitto Kabwe, has unleashed in the past few days, some scathing attacks on the Minister of Energy Sospeter Muhongo, for proposing a thorough review of the Gas exploration contracts. Mr. Kabwe described Dr. Muhongo’s statements as irresponsible, publicity stunts and cowboy’s approach at the expense of transparency. What I found rather irresponsible, odd, flawed and vague, was the broad idea of “Transparency” in which Mr. Kabwe is attacking Dr. Muhongo’s premise without providing a practical solution under conventional wisdomI also found Mr. Kabwe’s idea of shelving gas exploration for ten years as logically, and economically naïve. At best I would describe the proposition as a theory that contravenes the basic and natural economic principles that cannot be implemented in a needy nation like ours. Implementing this thought would be nothing short of economic suicide for a nation whose economy is extremely fragile.Mr. Kabwe’s Transparency assertion reveals nothing short of tactical political, intimidation, representation and defense of the unknown interests. I would not go as far as describing the verbal assault as a self serving personal act of vengeance. However, the premise under which Mr. Kabwe’s argument is based, and his pattern of attack, points towards just that.Mr. Kabwe unambiguously failed to explain how making transparent shoddy contractual agreements, will benefit the country without identifying the loopholes and deficiencies through extensive review. Arguably, lack of legal and technical knowhow to intimately interpret word by word in the existing contracts to weed out the elements tilting the scale on the favor of investors and shadowy forces of corruption, would have lent Mr. Kabwe’s proposition of transparency, some flesh to stand the test in opposition Dr. Muhongo’s hypothesisMr. Zitto ought to understand that, major foreign companies operating in Africa have tremendous resources. They have access to some of the best lawyers, and subject matter experts with extensive experience in contractual review, interpretation, negotiations, and writing. A fact which has many a times, led to the creation of lopsided contracts that have benefited investors while fleecing the host country.Mr. Kabwe failed to provide a balanced approach to those deficiencies. In my opinion, Dr. Muhongo’s approach is heroic, and nationalistic. The public should, without reservation throw its absolute support behind this man for his position to temporarily suspend and review all the current contracts related to gas exploration and even electricity productionHaving worked in the Investment Banking –Capital Markets- Can affirm to the fact that, success or failure of an investment, primarily depends upon how crafty a contract is. Managers across all economic sectors assemble top legal minds and experienced subject matter experts that would pull off successful investments through favorable and well structured contracts. These contracts at the same time have in them, clauses and provisions that provide room for ongoing review and amendments contingent upon the prevailing conditions or circumstances and market situations.My only question is why Zitto is up in arms trying to block the review of questionable contacts in the public eyes, what is his fear? Singapore, India, Venezuela, Brazil etc. in recent years, radically modernized and even terminated some contracts with foreign investors in various sectors that were becoming economic liabilities or not equitably representative. This is how things work be it in municipalities, public or private companies, sovereign states and government agencies. Dr. Muhongo as a subject matter expert has suggested just that. Why should he face political interference?From my understanding, TPDC, a body tasked with the contractual review is not a political body. It is a professional entity made of subject matter experts –seasoned professionals -. If Mr. Zitto is dissatisfied with TPDC current formation or the capability, he should demand the overhaul of its management team for a more qualified one, which will execute the task –contractual review- diligently, impartially and independently for the interest of the nation. All findings thereafter be made public to satisfy his demand for transparencyPolitical meddling, intimidation and personal hostility are not doing the country any good considering the fact that, main victims of bad contracts in the energy sector are the country’s economy, and the public at large. Politics should be kept off professional undertakings. Mr. Kabwe should let Dr. Muhongo do his job. This man has been in the office for a very short period. He has taken bold and risky decisions no other minister has ever taken in the ministry and the energy sector in general. He is stepping on dangerous toes for the best interest of the country, and what he needs the most at this point is our support not interferenceDr. Muhongo’s success or failure is not going to be measured by how many politicians he pleased or displeased, but on what he delivered to the country at the time of need. Soon or later, the public will know whether he was a bluff or a HERO he painted himself to be. Dr. Muhongo’s approach is the right step in the right direction. Wrong step into the wrong direction is to politically interfere with his work in the name of transparency. Give him a chance to do his JobMungu Ibariki Tanzania
Forwarded by Dr Shaban Nzori. "Mzalendo Mtanzania" is Mr Mashaka John.
Wednesday, 19 September 2012
- 14:08
- Unknown
- RAIA MWEMA
- 1 comment
Uskochi
Toleo la 259
19 Sep 2012
NIANZE makala hii kwa kurejea simulizi moja ambayo nimeshawahi kusimulia katika makala zilizopita.
Kati ya mambo yaliyonishangaza sana baada ya kuwasili hapa Uingereza kwa mara ya kwanza, takriban muongo mmoja uliopita, ni jinsi Ukristo ulivyopoteza nguvu miongoni mwa Waingereza wengi.
Licha ya ‘kutolewa ushamba’ kwa kushuhudia vitu mbalimbali ambavyo kabla ya kuja hapa vilikuwa ni vya kufikirika tu kama si kuviona kwenye filamu na runinga, kilichoniacha mdomo wazi zaidi ni pale nilipoona jengo ambalo zamani lilikuwa kanisa limegeuzwa klabu ya anasa za usiku (night club).
Kwa Mndamba mie niliyezaliwa sehemu (Ifakara) ambayo ina historia ya karibu na umisionari, kuona ‘nyumba ya Bwana’ imegeuzwa ukumbi wa anasa lilikuwa jambo la kushangaza mno. Na kadri nilivyozidi kuielewa nchi hii ndivyo nilivyozidi kutambua kuwa idadi kubwa tu ya Waingereza haina muda na Mungu au dini kwa ujumla.
Kila nilipopata wasaa wa kudadisi sikusita kuuliza swali hili, “hivi imekuwaje ninyi mliotuletea Ukristo huko Afrika leo hii mnaonekana hamna habari na dini hiyo ilhali dini inazidi kupamba moto huko kwetu?”
Majibu ya swali hilo yalikuwa tofauti kati ya mtu mmoja na mwingine, lakini jibu lililojitokeza mara nyingi zaidi ni kuwa imani ya kiroho haina nafasi muhimu katika zama hizi za sayansi na teknolojia.
Kimsingi, katika Jumapili ya kawaida, makanisa mengi ya Uingereza hujaza ‘wageni’ (kwa maana ya wakazi wenye asili ya nje ya nchi hii, hususan Waafrika na Wakritso kutoka Ulaya ya Mashariki).
Katika siku za kati ya wiki, mengi ya makanisa hayo yamekuwa kama vivutio vya utalii hasa ikizingatiwa kuwa mengi ya majengo hayo ya ibada yana sehemu muhimu katika historia za sehemu yaliyopo.
Lakini ukidhani kufifia huko kwa ‘dini ya nchi hii’ (kimsingi Uingereza ni nchi ya Kikristo na Malkia anaendelea kuwa ‘mkuu wa heshima’ wa Kanisa la Anglikana duniani) kunawafanya Waingereza kutokuwa watu wa kufuata maadili, basi ukienda sehemu mbalimbali za huduma (kama vile kwenye benki, maduka makubwa nk) au ofisini utakumbana na picha tofauti kabisa.
Kwanza, kwa kiasi kikubwa hakuna njia za mkato za kupata fedha katika nchi hii pasipo kuwajibika. Pili, Waingereza wengi wanachukulia shughuli zao kwa uzito na umuhimu mkubwa. Lakini jingine kubwa ni jinsi serikali na taasisi za utawala zinavyojibidisha kutengeneza mazingira mazuri ya kumwezesha kila anayejituma ‘avune matunda ya jasho lake.’
Kuna suala la haki na wajibu. Kwa kiwango kikubwa, wengi wa Waingereza wanatambua wajibu wao wa kulipa kodi, na wajibu huo unawapatia haki ya kupatiwa huduma ambazo kwa kiasi kikubwa zinakidhi matakwa yao.
Kadhalika, taasisi mbalimbali za hapa zinatambua wajibu wao wa kutoa huduma zinazoendana na matakwa ya wahitaji huduma hizo.
Kwa hiyo, licha ya nafasi ya Mungu na Ukristo (au dini kwa ujumla) kufifia miongoni mwa Waingereza wengi, bado kwa kiasi kikubwa jamii hii inafanya ‘mema’ mengi zaidi ya akina sie huko nyumbani tusiokosekana kwenye nyumba za ibada.
Binafsi, licha ya kutopendezwa kuona watu waliotuletea Ukristo huko nyumbani ‘wakiupiga teke,’ wengi wa Waingereza wanaendelea kunivutia jinsi wanavyoendesha maisha na shughuli zao kwa uadilifu mkubwa.
Japo Waingereza wengi ni kama hawana dini lakini wengi wao hawapo tayari kuona mwanadamu mwingine ananyimwa haki zake za msingi, na ndiyo maana nchi hii imetokea kuwa kimbilio kubwa kwa mamilioni ya wakimbizi ambao miongoni mwao ni wale walionyanyaswa na kuteswa na nchi zao aidha kwa imani au itikadi zao, jinsia zao, kutetea wanyonge na kadhalika.
Kwa hali hii, yayumkinika kuhitimisha kuwa bora kuwa ‘mpagani’ mtenda mema kuliko mcha-Mungu fisadi. Ndiyo, dini imepoteza umuhimu wake kwa wengi wa wenzetu hawa lakini wengi wao wameendelea kuwa ‘watu wema’ kuliko mamilioni ya wacha-Mungu huko Afrika.
Yawezekana kabisa ‘wapagani’ hawa kwenda mbinguni kutokana na kumpendeza Mungu kwa matendo yao huku washika dini wetu wakigeuzwa kuni za kuchochea washiriki wao katika kukandamiza, kuibia, kunyanyaswa na kufanya kila baya kwa wanadamu wenzao.
Ni katika mazingira haya ya ‘Uingereza ninayoipenda licha ya wengi wa watu wake kumpa kisogo Mungu’ ndipo nilijikuta nikishtushwa na habari katika gazeti moja la huko nyumbani kuwa Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Diane Louise Corner, “amesifu serikali kwa kukuza demokrasia kutokana na uhuru unaovipa vyombo vya habari kuujuza umma kuhusu mambo mbalimbali yakiwamo matumizi ya umma yanayofanywa na serikali.”
Awali, naomba niseme bayana kuwa hadi muda huu bado nina wasiwasi iwapo Balozi Corner alinukuliwa sahihi (yaani, iwapo kweli alitoa kauli hiyo).
Sitaki kabisa kuamini kuwa Balozi huyo hana taarifa kuhusu unyanyasaji mkubwa unaofanywa na serikali dhidi ya vyombo vya habari binafsi huko nyumbani (ukiweka kando gazeti hilo la serikali liloandika habari hiyo).
Hivi inawezekana Balozi Corner hajawahi kusikia manyanyaso yaliyowakumba wamiliki wa jukwaa huru la mtandaoni la Jamii Forums ambalo kwa hakika limekuwa chanzo kikubwa cha kufichua maovu katika jamii?
Inawezekana Balozi huyo hajawahi kusikia tukio la kumwagiwa tindikali kwa mwandishi wa habari Said Kubenea ambaye serikali inayosifiwa na Balozi huyo imejipa jukumu la kudumu kumdhibiti mhariri huyo na gazeti lake ambalo kwa sasa limefungiwa kwa muda usiojulikana?
Ni demokrasia ipi anayozungumzia mwanadiplomasia huyo ambayo kwa upande mmoja inaruhusu mikutano ya chama tawala CCM katika kampeni za uchaguzi huko Zanzibar lakini si tu inapiga marufuku hata mikutano ya ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) lakini pia inapelekea Jeshi la Polisi kunyanyasa wananchi wasio na hatia ambao ‘kosa’ lao pekee ni kutumia haki yao ya kikatiba na kidemokrasia ya kukusanyika (freedom of association)?
Hivi kweli Balozi Corner hana taarifa kuwa Jeshi la Polisi limeshafanya unyanyasaji mkubwa dhidi ya wafuasi wa CHADEMA na kupelekea vifo vya wananchi wasio na hatia huko Arusha, Morogoro na kubwa zaidi ni kifo cha mwandishi wa habari Daudi Mwangosi huko Iringa hivi karibuni?
Ninasema sitaki kuamini kuwa uhuru wa vyombo vya habari au demokrasia ninayoshuhudia hapa Uingereza ina tafsiri tofauti na hiyo anayosifia Balozi huyo huko nyumbani.
Niwe mkweli, moja ya sababu ninazoona kuwa zinachangia sana ukosefu wa utawala bora katika nchi zinazoendelea (ikiwamo Tanzania) ni tabia ya nchi zilizoendelea kama Uingereza kuendeleza tabia ya kufumbia macho ukiukwaji wa haki za binadamu ambao hauna nafasi kabisa katika ‘jamii zao za kistaarabu.’
Hivi majuzi tu, serikali ya Uingereza kupitia Waziri Mkuu David Cameron imeomba msamaha kuhusiana na maafa ya Hillsborough yaliyotokea mwaka 1989 ambapo mashabiki kadhaa wa soka waliopoteza maisha.
Je, Balozi Corner anafahamu kuwa hadi leo serikali anayoisifia kwa kukuza demokrasia haijaomba msamaha kwa japo kifo cha mwandishi Mwangosi zaidi ya kuunda tume ambayo tayari imeanza kuhujumiwa huku baadhi ya wajumbe wake wakilalamikiwa kuwa na utendaji kazi wenye mushkeli?
Kama Mtanzania ninayeishi katika nchi ambayo huko nyuma ilitutawala kwa mabavu lakini ninaiheshimu na kuipenda kwa mengi inayofanya kwa utu wa mwanadamu pasi kujali ni Mwingereza au ‘mgeni,’ nimeshitushwa sana na kauli ya Balozi Corner ambayo kimsingi inaweza kutumika kama sababu tosha kwa watawala wetu kuendelea kukandamiza uhuru wa vyombo vya habari na haki za binadamu kwa ujumla kwa kigezo cha kupewa ‘seal of approval’ na mwakilishi wa taifa kubwa na linaloaminika kwa kuenzi haki hizo muhimu za binadamu.
Kuna nyakati ninapata shida sana kuyaelewa haya mataifa makubwa kama Uingereza katika uhusiano wao na nchi ‘zinazojikongoja.’ Wao ndio wafadhili wetu wakubwa, na asilimia ya kutosha ya fedha za walipakodi wao ndizo zinachangia uhai na ustawi wa nchi masikini (japo zina utajiri unaofilisiwa kila kukicha) kama Tanzania.
Lakini cha kushangaza, hakuna hatua za makusudi zinazochukuliwa nao angalau kuwabana mafisadi wanaokwiba fedha zao (ambazo kimsingi zinatolewa kwa minajili ya kumsaidia kila Mtanzania).
Sana sana ni utitiri wa sifa zinazomwagwa kwa watawala wetu (kama hizo za kukuza demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari), sifa ambazo zinawapa motisha mafisadi kuendelea kuitafuna nchi yetu.
Je, ‘upole’ huo wa wafadhili wetu unachangiwa na hisia kuwa fedha za mafisadi huishia kuhifadhiwa katika mabenki yaliyopo huku? Au inawezekana bado mentality ileile iliyoleta ukoloni (na hata Ukristo) kwamba sisi tulikuwa hatujastaarabika vya kutosha na ilikuwa muhimu kwa wakoloni kujipa jukumu hilo, hadi sasa tunapaswa kuwa na demokrasia na uhuru wa vyombo vya habari pungufu na tunayoshuhudia hapa Uingereza?
Nimalizie kwa kumkumbusha Balozi Corner kauli ya Waziri Mkuu wa zamani wa Uingereza Gordon Brown katika harakati zake za kuisaidia Afrika.
Alisema (namnukuu katika tafsiri hii isiyo rasmi) “pasipo kuongeza jitihada za kusaidia, itazigharimu baadhi ya nchi za Afrika zaidi ya miaka 150 kufikia tulipofikia sisi (Waingereza).”
Lakini kwa mwenendo huu wa ‘sifa tusizostahili’ basi yayumkinika kubashiri kuwa inaweza kutuchukua hata milele kufikia demokrasia ya kweli yenye kuruhusu uhuru wa kweli wa vyombo vya habari.
Tuesday, 11 September 2012
Iliwahi kuripotiwa kuwa Mkurugenzi wa Katiba na Haki za Binadamu wa Chadema, Tundu Lissu, aliipinga Tume iliyoundwa na Waziri wa Mambo ya Ndani Dkt Emmanuel Nchimbi kuchunguza mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, marehemu Daudi Mwangosi.Moja ya sababu alizotoa Lissu ni Tume hiyo kuwa chini ya uenyekiti wa Jaji Mstaafu Stephen Ihema,ambaye alimtuhumu kuwa na rekodi ya utendaji kazi yenye walakini.
Katika pitapita yangu mtandaoni, nimekutana na habari inayomhusu Jaji Mstaafu Ihema, ambapo alikuwa mjumbe wa Kamati ya Ushauri wa Ugawaji Vitalu vya Uwindaji wa Kitalii, na sasa kamati hiyo imevunjwa kutokana na kulalamikiwa mno kwa vitendo vya rushwa miongoni mwa wajumbe.
Binafsi nimeguswa sana na habari hii hasa kwa vile inahusu tuhuma za rushwa kwa kamati iliyokuwa inamjumuisha Jaji Mstaafu Ihema.Sasa tukiamini kuwa Jaji Ihema ameshindwa jukumu la ujumbe tu kwenye tume hiyo ya ushauri,kwanini tumwamini kwenye uenyekiti wa kamati ya uchunguzi wa kifo cha marehemu Mwangosi?
Wakati ninawapongeza wanahabari waliojitokeza jana kuifahamisha bayana Serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwa wanalaani vikali mauaji ya mwanahabari mwenzao yaliyofanywa na jeshi la polisi,ningependa kushauri kuwepo upinzani zaidi dhidi ya Tume hii ambayo kuna kila dalili kwamba itaishia kuwa kiini-macho tu.Awali,hofu yangu kuhusu Tume hiyo ilielemea zaidi Watanzania wameshashuhudia utitiri wa tume ambazo mara nyingi ripoti zake zimeishia kufungiwa maandazi na vitafunwa vingine badala ya kuwekwa hadharani//hatua kuchukuliwa.Wengi wetu tunakumbuka kuhusu tume ya milipuko ya mabomu huko Mbagala na Gongo la Mboto.Hadi leo hakuna kilichoelezwa kuhusu ripoti ya tume hiyo...and life goes on.
Je wewe ni mdau wa habari? Unapenda kuona uchunguzi wa kifo cha marehemu Mwangosi unafanywa independently na watu wasio na harufu ya utendaji kazi wenye walakini?Basi ungana na wanahabari kupiga kelele dhidi ya tume hiyo ya kisanii
Minister for Information, Youth, Culture and Sports, Dr Emmanul Nchimbi, embarrassingly leaving the vicinity after the demonstrating journalists rejected his request to address them CLICK HERE for more details on how the journalist was killed by the police |
Friday, 7 September 2012
- 15:23
- Unknown
- CCM, SOPHIA KESSY
- No comments
UCHAGUZI WA JUMUIYA ZA CCM
Moshi (v) chaguzi zilianza rasmi tarehe 3/09 /2012 - 4/09/2012
1. Uvccm ulfanyika terehe 29/08/2012 mwenyekiti wake aliechaguliw ani Gulaton Masiga.
2. Wazazi tarehe 03/09/2012 mwenyekiti wake ni sterwat lyatuu.
3. UWT tarehe 04/09/2012 mwenyekiti wake ni Grace Mzava
Aidha viongozi na wajumbe mbali mbali walichaguliwa na kupatikana chini ya uongozi wa chama wilaya ya moshi (V) Innocent Nzaba ambaye ni katibu wa ccm wilaya na mlezi wa jumuiya Gabriel Massenga ambaye ni mwenyekiti wa ccm wilaya.
Pia katika uchaguzi huo mtangazaji mahiri wa kituo cha Radio na TV Clouds Media Group cha jijini Dar es saalam Bi Sophia Kessy nae alijitosa katika uchaguzi huo kuwanaia nafasi ya uwakilishi wa UWT kwenda vijana wilaya na kuibuka mshindi kwa kura 415 dhidi ya kura zilizopigwa 416 ambapo kura 1tu iliharibika .
Bi Sophia Kessy amesema kuwa kwa sasa ni hatua ndogo kati ya zile kubwa ambazo amepanga kujitosa na kuwania ambapo matarajio yake ya baadae ni kuwa kiogozi wa ngazi ya juu zaidi .
BLOGU HII INATOA HONGERA NYINGI KWA SOPHIA..
Tuesday, 4 September 2012
Septemba 2, 2012: Pichani JUU: CCM inafanya mkutano wahadhara huko Bububu, Zanzibar licha ya Serikali "kusitisha shughuli zote za kisiasa ili kupisha sensa ya watu na makazi."
Septemba 2, 2012 Pichani CHINI,mwandishi wa habari wa kituo cha TV cha Channel Ten,Daudi Mwangosi akipata kipigo kutokakwa FFU kwa "kosa" la kufanya coverage ya KIKAO CHA NDANI cha Chadema huko Nyololo,Iringa,ambacho Polisi sio tu walikizuwia kwa SABABU ZILEZILE ZILIZORUHUSU MKUTANO WA HADHARA JIMBONI BUBUBU bali walipiga,kujeruhi wananchi wasio na hatia na HATIMAYE KUMUUA mwandishi Daudi Mwangosi ."
Mheshimiwa Rais, damu za wananchi wasio na hatia wanaouawa na polisi kwa "kosa la kutumia haki zao za kikatiba za freedom of association" hazitapotea bure. Polisi waliua Arusha,lakini hiyo haikuzuwia wanachama na wapenzi wa Chadema kukusanyika Morogoro ambapo polisi waliua tena.Hata hivyo,kifo hicho hakikuwatisha wana-Chadema kukusanyika tawini kwao huko Nyololo ambapo baada ya unyanyasaji wa hali ya juu,polisiwaliua tena.
Hivi Mheshimiwa Rais hujifunzi kitu kutoka kwenye JEURI hii? Labda umesahau kuwa hata tawala dhalimu kabisa za kikomunisti huko Ulaya Mashariki zilijidanganya kuwa ukatili na unyama wavyombo vya dola utazidumisha (tawala hizo) milele,lakini wakati ulipofika zilisambaratika.Na huko Afrika ya Kusini,makaburu walitawala kwa mtutu wa bunduki lakini hawakuweza kuzuwia kuanguka kwa mfumo wa kibaguzi.
Mwanafalsafa Karl Marx aliwahi kuusia kuwa "mnyonge hana cha kupoteza zaidi ya minyororo." Wakati mafisadi wanaishi kwa hofu ya kunyang'anywa walichotupora, wanyonge wasio na uhakika na mloujao wanaishi kwa matumaini tu.Lakini kuishi huko kwa matumaini kunaweza kuwa silaha yenye nguvu kuliko vipigo,risasi na unyama wa FFU.
Watu wameichoka CCM na ni wazi kuwa vitisho na mauaji ya raia yasiyo na hatia hayawezi kushusha chuki hiyo.Sana sana inawaongezea tu sababu ya kukichukia chama hicho. 2015 si mbali.CCM inaweza kung'olewa madarakani.Ni vema,Mheshimiwa Rais,ukaanza kutafakari hatmayako pindi hao wanyonge wanaonyanyaswa sasa wakishika madaraka.
Watanzania wana kila sababu ya kuichukia CCM lakini inaonekana kana kwamba chama hicho kinasaka sababu nzito zaidi.Sijui ni kuishiwa na uwezo wa kuongoza au ndio kimezeeka na kinasaka namna ya kujipeleka kaburini,lakini kilicho wazi ni kuwa kila tone la damu linalomwagika kutokana na unyama wa polisi wetu ni sawa na lita nyingi za petroli kuchochea moto wa mabadiliko.
- 00:20
- Unknown
- BONGOFLAVA, Witnesz
- No comments
Brooklyn Hip hop Festival
Wes Jackson, President and executive director of Brooklyn Hip hop festival in the middle Witnesz the Fitnes mkewe Ebonie Jackson ambaye yupo kwenye kitengo cha mahesabu ya shughuli kadhaa za mumewe ikiwemo Hip Hop Festival and Brooklyn Bodega
Brooklyn Bodega a complicated animal, creators of BHF, Top notch blogazine (blog meets magazine) cultural programmers, Hip Hop Advocacy Group.
The bodega was founded in 2006 by Wes Jackson as the online home of the BHF , under the guidance of Bodega’s initial creative director and administrator James Blagden and Alma Geddy-Romeo.
The bodega grew into one of the most respected online destinations in the Hip Hop community Editorially, the Bodega strives to add a more academic voice to the world of Hip Hop Journalism, It Derives deep into issue facing the Hip Hop community from music business to politics to technology and they offer a professional and intellectual voice.
Wes Jackson has over 15years experience as an entrepreneur and innovator in music business. His carrier began with producing concerts for Nas, The Roots, The Dave Mathews, band and de La Soul etc. He went on and started his own promotions company by the name seven Heads Promotions, seven Heads was instrumental in launching the career of MOs Def. ,Talib Kweli and others under Wes’ Leadership. Seven Heads expanded into a Record label and a management company, The record company that spun into the room Service Group (RSG) one of the leading digital marketing, RSG has worked with Def. Jam, Capitol, Warner Bros, Interscope, vivendi, and converse the list is endless.
In addition to his successful business ventures Wes also serves as lecture at city University of New York (CUNY) Wes’s entrepreneurship spirit endure as he continues to grow the BHF into a world class event also as the Brooklyn Bodega Brand with the pop-up store Bbeats at DeKalb market in Downtown Brooklyn,
Wes aliweza eleza kiurefu zaidi juu ya biashara mjini New York kama mmiliki halisi wa hiyo Festival iitwayo Brooklyn Bodega na record label na mengineyo ambayo yote yanahusika na harakati za kihip hop zenye mafanikio makubwa up to date na kufafanua kibiashara zaidi mambo mbali mbali ikiwemo ujasiriamali na sababu za festival hiyo kutohusisha sana au kabisa wasanii kutoka nje wa Hip Hop,alisema wes kuwa wasanii wa hip hop Nchini New York wapo wengi mno mfano wa mafuriko na wote ni wa kali na kusbabisha eneo hilo kuwa hapatoshi hata kwa wakazi wenyewe so mtu yeyote akitoka nje ya nchi akitaka kuingia kwenye soko hilo ni lazima awe extra special, multitalented, unique na awe ni mchapa kazi mara tatu ya wasanii wa New York na ndivyo ilivyo kwa wanawake wanao fanya Hip Hop pia the half to beat men ambao they are flooded with extra energy has to be used In order to stay on the top of the game.
Pia nilipata kujua maana ya neno Bodega kama ambapo iliwahi sikika kwenye moja ya nyimbo za Big punisher alipo sema my father’s Bodega kwenye intro na kufafanua ya kwamba neno Bodega ni la kispanish likimaanisha panapo tengenezwa wine, ama corner store mjini new york ambapo huuzwa wine,vilevi mbali mbali na vitu vyote vihusuvyo starehe ikiwemo urahisi wa kupata condoms hata nyakati za usiku huwa pako wazi masaa 24 siku saba za wiki 24/7 kwenye hiyo corner store wanapatania ya kuwa ni an organized mess place,nikmrahisishia kwa kusema an organized place in a disorganized manner? akasema thats whats up kwa kuwa ukienda kwenye a corner store kulikuwa kuna taka taka karibia za aina zote anazohitaji mtu kwa nyakati za usiku na mchana na hutumika kama maskani na kupanga kuhusu mitikasi pamoja na kupeana mistari ma dj,rappers watu wa aina zote kwenye harakati walikuwa wakitia maguuhapo hata mkiwa hampatani mtaani mkifika hapo kila mtu huwa peacefull ni kiduka kona ambacho watu wa jinsia zote na kutoka pande zote kupata huduma,kwa upande wangu nilipata picha ya gengeni ambapo mara nyingi vijana hukaa hapo ndani ya bong na kuganga njaa ama wakihesabu magari ama kwa kuwalaghai mabinti hahahahaa!
So a lot of things happening at a bodega store you name it as the aim of the Brooklyn Bodega ambapo ndiye mama wa Hip Hop festival tamasha ambalo hufanyika kila mwaka mjini New York tangu lianze limekwisha fanya matamasha nane mpaka sasa na mwaka huu limekwisha fanyika ,ambapo watumbuizaji wa kuu walikuwa Buster Rhymes na Tribe called Quest na host Mkuu wa tamasha hilo miaka nenda miaka rudi akiwa ni Uncle Ralph.
Heshima Zizidi Kuendelea
CHANZO: Ukurasa wa G+ wa Witnesz
Sunday, 2 September 2012
Subscribe to:
Posts (Atom)