Saturday, 8 December 2012

Nilizaliwa tarehe kama ya leo, miaka makumi kadhaa yaliyopita. Siku yangu ya kuzaliwa 'inagongana' na siku ya kuzaliwa kwa taifa letu la Tanzania (au Tanganyika?) tulipopata uhuru tarehe 9 Disemba mwaka 1961.

Tofauti na wengineo ambao haudhimisha siku za kuzaliwa kwa pati, mie hutilia mkazo zaidi katika sala (kumshukuru Mungu kwa kunijalia miaka yote hiyo,na kumwomba anibariki nipate miaka zaidi) na kufanya tafakuri ya wapi nimetoka,nilipo na ninakoelekea.

Kwa 'somo' wangu Tanzania, yeye birthday yake ni tofauti kabisa na yangu japo tuna-share tarehe moja (ila miaka tofauti). Mwenzangu huadhimishiwa siku yake kwa gwaride na hotuba mbalimbali.Lakini pia kwa vile birthday ya Tanzania inamgusa kila Mtanzania, sikuhii inakuwa na umuhimu wa kipekee kufanya tathmini ya taifa limetoka wapi, lipo wapi na linaelekea  wapi.

Kwabahati mbaya (au pengine kwa makusudi ya wenzetu wachache) kila inapojiri birthday ya Tanzania tunajikuta na maswali mengi zaidi kuliko majibu.Wengi wanajiuliza kwanini tuendelee kuwa masikini wa kutupa ilhali tuna kila aina ya utajiri.Kwamtizamo wangu, wa kulaumiwa zaidi si viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza bali 'uzembe' wetu wakuchagua viongozi pasi kuzingatia kama wataweza kututumikia kwa dhati na uadilifu.

Enewei, hii sio siku ya kuandika makala ndefu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kumaliza na kuanza mwaka mwingine huku nikitarajia baraka zaidi kutoka Kwake. Nwashukuru pia wazazi wangu, Baba  Mzee Philemon Chahali na marehemu mama Adelina Mapango kwa kunizaa. Pasi mapenzi ya Mungu na wazazi wangu hao leo nisingekuwepo kuadhimisha siku hii ya kuzaliwa.Nawashukuru piawanafamilia wenzangu,ndugu,jamaa na marafiki kwa kuniwezesha kufika hapa nikiwa hai.

Nawashukuru pia ninyi mnaotembelea blogu hii kwani mmekuwa sehemu ya familia yangu ya kijamii tangu mwaka 2006. Baadhi yenu tunafahamiana,baadhi yenu hatufahamiani lakini kwa umoja wenu mmenifanya kuwa mwenzenu na kupita eneo hilimara kwa mara.

Shukrani pia kwa watu mbalimbali niliofahamiana nao aidha kupitia uandihi wa makala au kwa kukutana kwenye mitandao ya kijamii, hususan Twitter na Facebook.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI 

3 comments:

  1. HONGERA SANA KWA SIKU YA KUZALIWA KAKA EVARIST..MWENYEZI MUNGU NA AKUJALIA MIAKA MINGI ILI UWEZE SIKU MOJA KUSEMA NA WAJUKUU WAKO.UWE NA SIKU NJEMA SANA..

    ReplyDelete
  2. hongera sana;
    naomba mungu aendelee kukupa maisha marefu kwani bado una deni la kunielimisha zaid na kuwaelimisha wa tz kwa ujumla wetu.
    2010 tulijitaidi kuleta mabadiliko ya uongoz kwa kiwango kikubwa nimatumaini ya wengi 2015 tutapata uongoz (viongozi) wenye wajibu wao kwa wa Tz na wenye uchungu na nchi yao na watakao weza kututumikia kwa dhati na uadilifu

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget