Tuesday, 1 September 2009




Jana nilibahatika kuangalia kipindi flani cha kuvutia katika kituo cha runinga cha BBC2.Mada kuu ilikuwa ni namna makampuni makubwa, katika jina la utandawazi, yanavyosaka faida kupitia biashara ya ngono.Tangu mwanzo wa kipindi hicho ilionekana bayana kwamba kuna mahusiano ya karibu, japo yasiyo waziwazi, kati ya makampuni yanayotengetengeneza filamu za ngono na makampuni ya biashara nyingine katika nyanja zisizohusiana na ngono.

Kwa mfano, hoteli nyingi zina huduma ya idhaa (channels) za kulipia kadri inavyoangalia zinazoonyesha ngono kwa wateja wanaohitaji.Kwa namna utaratibu huo ulivyosambaa sehemu nyingi ulimwenguni ni dhahiri biashara hiyo ina faida nono.

Mfano mwingine ni kwa makampuni ya simu za mikononi.Japo jambo hilo linaweza kuonekana geni huko nyumbani, takriban makampuni yote makubwa ya simu za mikononi yana huduma zinazomwezesha mteja kuchungulia kile kinachojulikana kama ngono nyepesi (soft-core porn).

Lakini kama kuna mahala ambapo biashara ya filamu za ngono imeshamiri vilivyo basi ni kwenye mtandao wa kompyuta yaani intaneti.Ni kutokana na kushamiri kwa filamu za ngono kwenye intaneti, hususan huduma zinazowezesha watumiaji kuweka filamu (uploading) wao wenyewe,kumekuwapo hisia kwamba intaneti “itaua” makampuni ya filamu za ngono.

Watetezi wa hoja hiyo wanadai kuwa urahisi, kwa maana ya gharama na access, wa kuona filamu za ngono kwenye intaneti unaweza kabisa kupelekea wateja wazoefu wa filamu za ngono kuacha kununua filamu hizo madukani kwa vile zinapatikana (mara nyingi pasipo kulipia senti moja) mtandaoni.

Wapinzani wa hoja hiyo wanadai kuwa kama ambavyo watu hawaachi kwenda hotelini au migahawani kwa vile tu wanaweza kujipikia nyumbani ndivyo ambavyo filamu “halisi” za ngono madukani zitakavyoendelea kuvutia wateja licha ya upatikanaji wake kirahisi mtandaoni.

Kuna hoja ya ziada kwamba wakati filamu “halisi” za ngono hutengeneza kwa kuzingatia ubora wa hali ya juu katika studio zilizo tayari kwa shughuli ya aina hiyo, nyingi ya filamu za “ridhaa” kama hizo zilizotapakaa mtandaoni zina ubora duni. Lakini hoja hiyo inavutia upinzani mwingine (kutoka kwa watetezi) kwamba nyingi ya filamu za “ridhaa” mtandaoni zina uhalisia zaidi, kwa mfano pale wapenzi wanapoamua “kuweka mambo yao binafsi hadharani” mtandaoni. Watetezi hao wanakwenda mbali zaidi na kudai kuwa filamu za “ridhaa” mtandaoni zina ladha mithili ya “kupiga kozi” (u-peeping tom).

Mfano mwingine ulioonyeshwa kwenye kipindi hicho ni namna makampuni makubwa ya ku-process malipo ynanavyorahisisha upatikanaji wa huduma ya filamu za ngono.Na hili ni maarufu zaidi kwenye tovuti za ngono mtandaoni. Mara nyingi, ili mtumiaji aweze kulipia huduma hiyo analazimika kutumia credit au debit card yake katika tovuti maalumu za ku-process malipo. Kwa mara nyingine, ni dhahiri kwamba kushamiri kwa makampuni ya aina hiyo kunaashiria faida nono kwao kwani kinyume chake yasingekubali “fedha chafu”.

Kilichonigusa zaidi katika kipindi hicho ni namna filamu za ngono, whether zile halisi kutoka studio au hizo za “ridhaa” mtandaoni zinavyochangia kubadili sexual behaviours sehemu mbalimbali duniani.Na pasipo kutarajia, mtangazaji alitoa mfano wa athari za filamu hizo kwa sexual behaviours huko nyumbani. Guess what? Ni kile ambacho wengi wanakihusisha na u-Magharibi: tendo la ndoa kinyume cha maumbile! Kwa mujibu wa kipindi hicho, wataalam wetu wa sexual behaviours huko nyumbani wanaamini kwamba filamu za ngono zimechangia sana kulifanya tendo la ndoa kinyume cha maumbile kuwa mithili ya jambo la kawaida (mainstream).


Binafsi nadhani moja ya eneo lililopewa attention pungufu tunapoangalia athari za mageuzi mbalimbali yaliyojitokeza miaka ya 80 (1980s) ni mageuzi katika tabia za kujamiiana.Hivi ni mie pekee ninayeshtushwa na kukua “kwa ghafla” kwa interest kwenye umbile halisi la mwanamke wa Kiafrika? Na swali la nyongeza, je kwanini “ghafla”, ashakum si matusi, makalio ya mwanamke wa Kiafrika yaonekane kuwa na umuhimu wa kipekee katika ku-describe shepu yake? Wapo wanaohusisha interest hiyo na kukua kwa interest kwenye tendo la ndoa kinyume cha maumbile.

La kusikitisha ni kwamba hakuna namna tunavyoweza kukabiliana na nguvu kubwa ya utandawazi. Filamu za ngono zinazoendelea kuonyeshwa katika “Drive-Inn, Avalon na Empress za uswahilini” zinazidi kusambaza tabia ambazo kimsingi zinakinzana na maadili yetu. Kipindi nachokizungumzia kilionyesha namna vijana flani huko Ghana walivyoishia kuambukizwa ukimwi baada ya kujifunza “mbinu za kisasa za kufanya tendo la ndoa” mtandaoni.Ni dhahiri pia kuwa filamu za ngono zinazoonyeshwa kwenye “majumba yasiyo rasmi ya filamu za ngono” (tukiweka kando mfumuko wa kasi wa madanguro bubu) unazidi sio tu kubomoa mila na desturi zetu bali pia kutapakaza maambukizo ya gonjwa la ukimwi.

Pengine mahala mwafaka kubaini kuwa tendo la ngono kinyume cha maumbile limekamata kasi katika jamii yetu ni pale kwa Dada Dina.Lakini hiyo si kusema kwamba suala hili linajadiliwa kwa uwazi zaidi. Kama kawaida yetu, baadhi ya mambo yanaonekana kama mwiko kuyajadili hata kama yanaathiri jamii yetu. Yayumkinika kuhitimisha kuwa unafiki ni kikwazo kikubwa kwa mijadala ya aina hiyo. Wapo “waliobobea” kwenye matendo kama hayo lakini aidha wanakwazwa na “kuonekana wa ajabu” iwapo watadiriki kuzungumzia ishu ya namna hiyo au “wanaruka kimanga” pale wanapoulizwa licha ya umahiri wao.

TAFAKARI!

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget