Saturday, 23 June 2012

MNYIKA HAKUKOSEA

Mara ya kwanza niliona mnyika amekosea sana kumwita rais Dhaifu, hii ni kutokana na ukweli kuwa kanuni za bunge hazimruhusu, lakini pia ameyasema yale mbele ya watanzania wote ambao wapo wenye mapenzi thabit kwa rais. Lakini kumbe rais amemruhusu mnyika aseme maneno yale

Hivi ni nani hajawahi ona watoto wa darasa la kwanza wanafunga barabara kwa kuwa mwenzao amegongwa mpaka matuta yawekwe, na siku hiyo hiyo matuta yanawekwa? Tumemfundisha nini mtoto huyu? Tumemfundisha serikali yako ni dhaifu lakini ukiishikia kiboko inatekeleza hapo hapo

Wakati wa mkapa wanafunzi udsm waligoma, mkapa akafunga chuo mwaka mzima, hatukusikia tena mgomo mpaka 2007 wakati wa kikwete, tuliposikilizwa tulichogomea, tuligoma kwa kila kitu hata kama hatukustahili

Kitendo cha mtu kusimama mbele ya bunge akapata courage ya kusema rais dhaifu, akarudia na kurudia peke yake inaprove kama rais ni dhaifu

USHAURI WA BURE KWA RAIS: 
Haiwezekani sovereign country tunaambiwa kuna muwekezaji ana passport tano, serikali imemshindwa, KWELI? Serikali ya watu mil 40, jeshi, police, na TISS, inaandikwa gazetini imemshindwa mtu mmoja? Vaa mkono wa chuma baba


Hakuna uhuru usio na mipaka mheshimiwa kikwete. He who wishes to be obeyed must know how to command, uhuru ukizidi sana tunaharibu nchi. Unatuachia saaaana mpaka tunaanza kukukosea heshima

Madaktari wamegoma, tukaambiwa rudini kazini haraka au tutawafukuza wote tutaleta wanajeshi wafanye kazi, then kesho tunawaita tunakaa nao mezani, baba watakupanda kichwani washajua una udhaifu, unawaogopa..

Machiavelli anasema If an injury has to be done to a man it should be so severe that his vengeance need not be feared..
Kwa mfano watoto wanagoma lazma matuta yawekwe, waagize walimu wao wawatandike viboko watoto warudi darasani, then baada ya mwezi weka tuta kuzuia ajali kwa kuwa hapo mwanzo walikaa miaka bila tu.
Tunagomagoma kila kitu kwa sababu unaturuhusu, lakini pia haujali.. Wanafunzi wagome, madokta wagome, walimu wagome, hivi nani anawapa kiburi? Hawa madokta nani anawapa kiburi cha kugomea serikali?

Men are so simple and so much inclined to obey immediate needs that a deceiver will never lack victims for his deceptions
Mtembelee Slimcony katika blogu yake inayopatikana HAPA

1 comment:

  1. Well said, ila lakini pia naomba uangalie na upande wa pili! kundi moja kugoma mara moja haina tatizo, makundi kadhaa kugoma mara kwa mara inaonyesha kuna tatizo! Serikali inatakiwa kuanza kuwa serious na maamuzi yake na sio kutuchezea kiduku!

    Unadhani ni kwanini sikuhizi watu wanapuuzia maamuzi ya serikali, sio kama zamani?

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget