Pichani ni shoga maarufu Bilali Mashauzi ambaye ni nadra kukosekana kwenye sherehe za akinadada maarufu Tanzania |
SUNDAY, JUNE 10, 2012
MSIMAMO WANGU KUHUSU USHOGA
umeibuka mjadala mkubwa leo twitter kuhusiana na group la facebook la kudai haki za mashoga tanzania. i saw this coming, Mashoga wapo, walikuwepo na wataendelea kuwepo regardless tumewakubali au tumewakataa.
kwanza niseme Imani yangu ya dini, mwenendo wangu wa maisha na jamii ninayoishi nayo hainiruhusu kukubali ushoga. Natamka kuwa siukubali ushoga kwa kuwa kiimani ya dini yangu ni dhambi, lakini pia katika mfumo wa maumbile ya mwanadamu ni kinyume.
Lakini pia Sikubali uzinzi, uasherati, ushirikina, wizi pamoja na dhambi nyengine ambazo kwa utamaduni wa mtanzania ni makosa na dini zote tunazoamini Tanzania ni makosa hali kadhalika.
jambo linalonifanya niandike makala hii ni kuweka wazi kama hata Leo mashoga wakiandamana barabarani kudai Haki zao au nikisikia serikali imeruhusu ndoa za jinsia moja, nitaumia moyoni kwa kuwa kwa imani yangu si sahihi lakini sitatoka kuungana na WANAFIKI kupinga haki za mashoga
Nimetumia neno wa WANAFIKI kwa kuwa watanzania wengi ni WANAFIKI. kati yenu, nani dini yake inaamini uasherati na uzinzi ni sahihi? kipo kitabu cha dini kinaruhusu Uzinzi? je utamaduni wa Mtanzania unaruhusu Uzinzi? na je wewe mwenyewe unaamini Uasherati na Uzinzi ni sahihi?
kama dini yako hairuhusu uzinzi, wewe mwenyewe unaamini uzinzi na uasherati si sahihi, na utamaduni wako unakataa uzinzi na uasherati, UMEFANYA NINI KUHUSU SHERIA YA TANZANIA KAMA UKIKAA NA MWANAMKE/MWANAUME ZAIDI YA MIAKA MIWILI INAITWA NDOA? nguruwe huli ila mchuzi wake unakunywa?
Sisi wenyewe, ndugu zetu, jamaa na marafiki tunasifiana uzinzi, tunafanya uzinzi, tuna facebook groups za uzinzi, kitu ambacho kitamaduni na kidini si sahihi, lakini tukisikia shoga tunapiga kelele.. huo ni unafiki
Wapo waislamu wenzangu ambao ni walevi wa pombe lakini Nguruwe hawali kwa kuwa ni Haramu, pombe ni halali? mlevi ataingia peponi kwa imani yako? Baba Yangu ana msemo "ukiamua kula nguruwe, chagua aliyenona" meaning ukiamua fanya dhambi wewe fanya tu kwa kuwa kwa mungu hakuna dhambi ndogo
Niwakumbushe kwa mungu kuna njia mbili, Ama PEPONI au MOTONI. naamini kutokana na Mafundisho yangu kwamba Shoga, Mzinzi, Mwizi, Muasherati, Muuaji pamoja na dhambi nyengine wataingia moto mmoja hivyo basi ukiamua kataza maovu, acha kwanza wewe na kemea maovu yote bila kubagua kwa kuwa hata usipofanya ushoga ukafanya wizi, utakuwa hujajinasua na moto
sikatazi watu kupinga USHOGA na hata nikikataza mimi sio Mtume wala Rais na wala neno langu sio Sheria ila nasema Siungani na nyie Kwenye kupinga haki ya Mashoga kuoana wakati mmekalia kimya uzinzi, uasherati, na ushirikina ambavyo vyote havikubaliki kwa utamaduni wa mtanzania wala kwa dini tuanzoamini watanzania
*********HAYO NI MAONI YANGU NA NDIO MSIMAMO WANGU*****
CHANZO: Slimcony On Change Tanzania
Hapo ni ukweli kabisa. Wengi wetu ni wanafiki....
ReplyDeleteMoja kati ya haya mawili ni sahihi, makala yako haieleweki au mimi sijaelewa. Alokwambia wanaopinga ushoga hawapingi dhambi nyingine nani? haujaona wezi wakichoimwa moto au hiyo ndo si kupinga wizi? hujaona matangazo yote yanayoelimisha na kukataza ngono? hujashuhudia ndoa za mkeka wewe au za mafungu ikiwa ni katika kukataa zinaa? ashukuriwe MUNGU hata walarushwa twawaona wakipelekwa mahakamani?ulitaka vipingweje labda?hao ulowaita wanafiki ulitaka wafanyaje uone wanakemea vyote?sitaki kuamini kwamba wewe ndo mnafiki ila nadhani yabidi kufikiri na kuwa na msimamo kama baridi ni baridi na joto ni joto. Hakuna dhambi ndogo wala kubwa ila afanyaye zinaa afanya dhambi juu ya mwili wake tofauti na zingine, ukiamua kula nguruwe kula alonona hivyo wamaanisha ukiamua kuzini ufanye na jinsia yako? sodoma na gomora siamini kama ziliangamizwa shauri ya wivu. HAYO NI MAONI YANGU NA NDIO MSIMAMO WANGU
ReplyDelete1. Swala ni mazoea ya kupokea kila kitokacho majuu. Tulianza na kupokea dini hapo zamani na kuacha dini zetu, hadi leo tunapokea vitu, tamaduni na ustaarabu toka huko huko. Kinachofanyika majuu hata kama ni kibaya iko siku wakati utafika tutakubari kama tulivyokubali hayo mengine na mashoga wataoana.
ReplyDelete2. Wanafiki ni wale walio na mahusianao na mashoga (bila mashoga, mabasha au wasagaji mashoga wasingekuwepo)na wengine wako serikalini na wengine ni watunga sheria wanapojidai nao kupinga ndoa hizo.
3. Au ni kwa maumbile aliyopewa na Mungu au kwa kujifunza na hatimaye akazoea, shoga anavyojisikia hatuwezi kumusemea na hasa yule aliyezaliwa akajikuta yuko hivyo nae anahaki ya kuishi kwa tendo la ndoa bahati mbaya ni tofauti na dini inavyotaka. Lakini ni dini hiyohiyo inasema kazi ya Mungu haina makosa. Hakujiumba na hakupenda awe hivyo aliumbwa kama ulivyoumbwa wewe ukiwa mtimilifu kijinsia.
HEHEHEHE USHOGA HAUKUANZIA MAJUU UPO DUNIANI KOTE KABLA NA HATA YA WAARABU NA WAZUNGU KUJA AFRICA:
ReplyDeleteUSHOGA NI HISIA NA UJONGWA