Saturday, 15 June 2013




Mara nyingi nimekuwa mtetezi wa mabloga wenzangu hasa katika dhana iliyotapakaa miongoni mwa Watanzania wenzetu kuwa mabloga wengi ni watu wa kukopi na kupesti, hawajibidiishi kupata ukweli wa wanachoandika...na kimsingi ni wadaku tu. Moja ya sababu zinazoifanya jamii iwaangalie mabloga wa Kitanzania kwa jicho baya ni huu UGONJWA WA BREAKING NEWS. Looks like, mabloga wengi wanahangaika sana kupata breaking news, na wengi wakidhani kuwa wao kuwa wa kwanza 'kuvunja' habari kutasaidia kuwapandisha chati.

Lakini Breaking News ni kitu kinachohitaji umakini mkubwa.Unaweza kuskia 'flani kafa' kumbe si kweli, na keshoyake ukaletewa mashtaka ya 'kumzushia mtu kifo.' Tmaa ya kuwa wa kwanza 'kuvunja habari' sharti iendane na umakini wa kuhakikisha kuwa habari husika ni sahihi.Ni muhimu kujihangaisha huko mtandaoni, kutafuta kwenye Google-kama ni habari ya kimataifa- au kumpigia simu mhusika au watu wanaomfahamu, kabla ya kukurupuka na 'BREAKING NEWS' kwa herufi kuubwa.

Nimekerwa sana na uzushi unaosambazwa na baadhi ya mabloga wa Kitanzania kuwa ziara ya Rais Barack Obama nchini Tanzania imefutwa. Chanzo cha uzushi huu ni kwa mabloga husika kutofahamu maana ya neno SAFARI.Akilini mwa mabloga hao, neno la Kiingereza SAFARI ni sawa kabisa na neno la Kiswahili safari.Wasicheoelewa ni kuwa SAFARI ya Kiingereza inamaanisha "kutembelea mbugani hasa kwa madhumuni ya uwindaji au kuangalia wanyama" Na hicho ndio kilichokuwa -cancelled katika ziara ya Obama.

Kwamba Rais Obama alipanga kutumia siku mbili nchini Tanzania katika SAFARI (kuzuru mbuga za wanyama) lakini inadaiwa kuwa gharama za kilojistiki zimepelekea wazo hilo kufutwa.Kilichofutwa ni WAZO LA KUFANYA SAFARI MBUGANI na sio WAZO LA ZIARA YA KUJA TANZANIA.

Na kimsingi habari hii (ya Obama kuahirisha SAFARI MBUGANI) ambayo chanzo chake ni gazeti la Washington Post (soma HAPA) BADO HAIJATHIBITISHWA,na kilichoandikwa na gazeti hilo ni taarifa tu ya kichunguzi

Sasa angalia mabloga wetu walivyokurupuka na BREAKING NEWS zao



Ndugu zangu mabloga, lugha ya Kiingereza ni tatizo la Kitaifa kwa Watanzania wengi japo kuna wanaojifanya 'kichwa ngumu' licha ya kutoimudu lugha hiyo. Sasa mnapokutana na habari iliyoandikwa kimombo, na hamna hakika nayo, basi ni vema kuomba msaada kwa wanaoimudu lugha hiyo badala ya kutuharibia sifa ambayo tayari ishaanza kuharibika.

TUTAKAO-MANTAIN HESHIMA YA KUBLOGU NI MABLOGA WENYEWE, NA TUNAKAOISHUSHA HADHI YA KUBLOGU NI MABLOGA WENYEWE PIA.

NATARAJI MABLOGA NILIOWATAJA HAPO JUU WATATUMIA UUNGWANA KWA KUHARIRI HABARI HIYO YA OBAMA, NA PENGINE WATATUMIA USTAARABU WA KUOMBA RADHI WASOMAJI WAO, BADALA YA KUENDELEA KUPOTOSHA UMMA.

PIA NATUMAINI HAWATOCHUKIZWA NA MIE KUWATAJA KATIKA POST HII KAMA MIFANO YA UBABAISHAJI KATIKA FANI YA KUBLOGU.

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget