Monday, 21 October 2013



Hatimaye BBM imewasili kwa watumiaji wa simu za Android na iPhone. Hiyo ni habari njema sana hasa baada ya uamuzi wa Blackberry kuiondoa BBM kwa simu hizo maara baada ya kuizindua takriban mwezi uliopita.

Lakini kwa bahati mbaya, si kila mtu anaweza kuanza kuitumia huduma ya BBM mara baada ya ku-download. Kwa mujibu wa maelezo ya BlackBerry, kuna foleni kubwa ya watu wanaosubiri huduma hiyo, ikimaanisha kwamba hata uki-download bado utapaswa kusubiri kwa muda flani.

Kwa bahati nzuri, nimefanikiwa kukutana na makala moja inayoeleza jinsi ya kukwepa foleni hiyo. Naomba nitahadharishe kuwa mie sijaijaribu trick hiyo kwa vile tayari nina BBM. Kimsingi, BlackBerry walitoa maelekezo kwamba wanaohitaji BBM wajiandikishe kwa kutumia e-mail zao, kisha watafahamishwa BBM itapokuwa tayari.Nilifanya hivyo, na ndio maana nimekuwa mingoni mwa watu wa kwanza kupata huduma hiyo.

Anyway, twende kwenye maelekezo.

Baada ya ku-download BBM app utakutana na picha hii 


Kama ulijiandikisha kama mie, basi ingiza e-mail address yako kisha bonyeza 'Next' halafu chagua "I got the email." Uwezekano mkubwa ni kwamba baada ya hatua hiyo utapata maelekezo ya kuanza kutumia BBM kwenye simu yako.

Tatizo ni kama hukuwahi kujiandikisha, kwani utatakiwa kuwa kwenye foleni hadi BlackBerry watakapokutumia e-mail ya 'mwaliko.'

Lakini habari njema ni hii 'njia ya mkato' inayokuwezesha kukwepa foleni hiyo ya BlackBerry. Fuata hatua zifuatazo:

Kwanza, download BBM app kwenye simu yako ya Android au iPhone. Kwa watumiaji wa Android, nenda hapa Kwa watumiaji wa iPhone nenda hapa

Pili, fungua BBM app uliyoi-download, ingiza e-mail address yako, kisha 'lazimisha kuifunga app hiyo' (force-close). Kama unatumia iPhone, unaweza ku-force-close kwa ku-double click 'Home  button' kisha 'isukume' (sway away) BBM app.

Kwa Android, nenda kwenye 'Setting' kisha 'Apps' halafu BBM kisha bonyeza 'Force close'

Hatua inayofuata ni kuifungua tena BBM app ambapo sasa utapewa fursa ya kufungua akaunti ya BBM na hatimaye kupewa BBM PIN number ambayo utawapatia watu unaohitaji kuwasiliana nao kwa huduma hiyo.

Nifahamishe kama trick hii imefanya kazi

Nakutakia majaribio mema

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget