RADIO MBAO: Ninaomba kuwafahamisha kuwa mie na mwenzangu @djkvelli mkongwe wa masuala ya entertainment kama dj nchini Marekani na mmiliki wa kituo maarufu cha radio mtandaoni, RADIOMBAO, tumeunganisha nguvu, na kwa pamoja tunawaletea uzinduzi RADIOMBAO katika sura mpya. Licha ya matangazo ya radio, RADIOMBAO sasa inakuletea habari mbalimbali katika namna tofauti (bringing you news not in your traditional way). Uzinduzi rasmi utakuwa LEO Jumamosi ya Februari 1 mwaka huu 2014.
Tunataka nawe uwe mshiriki kwa kututumia habari kwa email radiombao@gmail.com nasi tutataja jina lako kama utapenda tufanye hivyo. Hii pia ni fursa adimu kwa wasanii kutangaza kazi zenu DUNIANI kwani RADIOMBAO inasikika katika NCHI 138 DUNIANI. Tutatangaza kazi yako ya sanaa BURE. Kwa kuunganisha uzoefu na ujuzi wa muda mrefu wa @djkvelli katika masuala ya entertainment nchini Marekani, na uzoefu wangu wa takriban miaka 10 katika fani ya habari, tunawaahidi kuwaletea kitu kipya,tofauti na kitakachokidhi mahitaji yako ya habari,mahojiano,burudani na soka, maisha najamii, teknolojia na mengineyo mengi. Ombi letu kwako ni kuwa sehemu ya familia ya RADIOMBAO: Mfahamishe ndugu, jamaa na rafiki yako kuhudu ujio mpya wa RADIOMBAO. Karibuni sana kutembelea tovuti yetu inayopatikana katika anwani hii
Wasiliana nasi kwa email radiombao@gmail.com
0 comments:
Post a Comment