Thursday, 2 April 2009


Mahamaka Kuu ya Tanzania imesema uamuzi wa serikali wa kulifuta Baraza la Wanawake Tanzania (BAWATA) ulikiuka Katiba. Majaji Amir Manento (mstaafu), Laurian Kalegeya na Juxon Mlay, katika hukumu yao iliyotolewa Dar es Salaam jana, walisema uamuzi huo wa Msajili wa Vyama na wa aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Ali Ameir Mohamed wa Septemba 1996, haukuwa halali.

Walisema katika hukumu yao ya kurasa 77 kwamba vifungu namba 9(a), 9(d)(iii), 12 na 13 (2) vya Sheria ya Usajili wa Vyama (vifungu 2(2),8,14,17 na 19(2) vya sheria ya sasa), vilivyotumiwa na Serikali kufikia uamuzi huo vilikiuka Katiba. Majaji hao, hata hivyo, waliamua kuwa vifungu hivyo ambavyo wakati huo na sasa vinaonekana kukiuka sheria, havitaondolewa katika sheria za nchi...SOMA ZAIDI
CHANZO: HabariLeo

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget