MWENYEKITI wa TLP, Augustine Mrema, ametinga Loliondo kwa Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri (KKKT), Ambilikile Mwasapile kunywa dawa na kutamba ni kwa ajili ya kuongeza nguvu ya mwili kupambana na ufisadi
Mrema, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC), alisema jukumu alilokabidhiwa kuzunguka nchi nzima ni kubwa linalohitaji kuimarisha afya yake.
“Kazi niliyokabidhiwa ni kubwa, kuzunguka nchi nzima kupambana na ufisadi kunahitaji kuimarisha afya yangu,” alisema Mrema na kuongeza:
“Bila kuimarisha afya huwezi kufanya kazi hii niliyokabidhiwa, waeleze Watanzania kuwa nimeimarisha afya sasa nikupambana na mafisadi kwenye halmashauri nchini kwa kwenda mbele.”
Alisema Watanzania wanatakiwa kumshukuru Mungu kwa ‘kuwashushia’ Mchungaji mstaafu Ambilikile Mwasapile (76), kwa sababu hawatumii gharama kubwa zaidi ya 500.
“Kama angekuwa Marekani tungeenda kwa Sh500? dawa yake haina kuchakachua unakunywa. Dawa nimekunywa na nimerudi na picha nimepiga naye ” alisema Mrema kwa kujiamini.
Hata hivyo, Mrema hakubainisha magonjwa yanayomsumbua hadi kwenda kwa Mchungaji Mwasapile, ingawa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari kwa muda mrefu. Siku za hivi karibuni vigogo wengi wa Serikali na CCM wamekuwa wakienda Loliondo kwa ajili ya tiba.
CHANZO:Mwananchi

Huyu jamaa kaisha na kuishiwa vibaya. Anakwenda mikoani kupigana na mafisadi wapi wakati yeye ndiye nepi ya mafisadi?
ReplyDeleteHeri kuanza vibaya na kumaliza vizuri kuliko kuanza vizuri na kuisha vibaya kama Mrema. Huyu anahitaji kuwaona wataalam wa akili.