Saturday, 26 November 2011


MKUU NIMEFURAHISHWA NA LOWASSA KUANZA KUANIKA UKWELI KUHUSU RICHMOND KWA KWELI NAONA ANAFANYA KILE NILICHOWAHI KUTABIRI KWENYE MAKALA YANGU YA "LOWASSA SEMA NENO MOJA TU" SASA KWA KULIONA HILO NIMEAMUA KUMTUNGIA SHAIRI HILO HAPO CHINI NAOMBA LITUNDIKE KWENYE BLOG YAKO WADAU WALISOME......


Kalamu yangu nashika, shairi nakutungia
Kamanda umeongea, kiwingu umeondoa
Hukutaka kusinzia,makosa kuyarudia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mwananchi nimesoma, la jana nilinunua
Machoya yakatuama, dukuduku umetoa
Uliyosema Dodoma, Kwakweli yanavutia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Richmond kupasua, mapema uligundua
Kikwete ukamwambia, mkataba kuondoa
Rais akakataa, nini alitegemea?
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Nape akashikilia, lile asilolijua
Mikoani kaambaa, uzushi kang’ang’ania
Jinalo kulichafua, wewe ukavumilia
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Mapema nilitabiri, falsafa nikapinga
Magamba sikukariri, kuvuana sikuunga
Ukweli niliukiri, mantiki iso kunga
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa

Beti sita nakomea, kalamu naweka chini
Mengi nimeongelea, soma tena kwa makini
Yatazidi kutokea,kusini kaskazini
Jibu umetupatia, viva kamanda Lowassa.

Shairi limetungwa na Nova Kambota Mwanaharakati,
+255717 709618
Tanzania, East Africa
Jumamosi, November 26, 2011


2 comments:

  1. Chahali umenisononesha. Umeingiwa na nini hadi unampamba huyu fisadi wa kunuka? Sikuamini kuona naweka shairi langu la kumjibu huyu mtoto changudoa wa maadili wa Lowassa na ukalifuta. Kweli binadamu si viumbe wa kuamini. Hata hii futa kwa maslahi yako. Ila jua legacy uliyokwisha ijenga ina thamani kuliko hiyo hongo ya mabaki ya ufisadi.
    Nkwazi Mhango

    ReplyDelete
  2. Kambota nitakubota, hata kama kiroboto,
    Yote unayolumbata, si chochote ni kokoto,
    Huna mpaka na kata, nijuacho u limpyoto,
    Kambota acha unywanywa, naona unatumiwa.

    Lowassa bado fisadi, hata mmpambe vipi,
    Kambota wewe hasidi, watumika kama nepi,
    wajiona wafaidi, kumbe kesho ni makapi,
    Kambota acha unywanywa, Lowassa akutumia.

    Wauliza nalipwaje, Nani huyo anilipe?
    Sijalipwa hata punje, mie mwezio si kupe,
    Shurti mi nijikunje, niishi si kwa mahepe,
    Kabota acha ushamba, Lowassa atakuponza.

    Naijua Richmond, Richmond ni Lowassa,
    Kikwete ni Richmond, Richmond ni mkasa,
    Kambota nawe ni bundi, Richmond takutesa,
    Japo wachumia tumbo, Kambota acha ujuha.

    Utajaliwa ja ng’oda, Siku yako ikifika
    Ja ng’oda utakonda, Lowassa akikutoka
    Ukuuishie ukuda, ubaki kulalamika
    Fisadi hana rafiki, Jifunze kwake Lowassa

    Mambo yalipombana, Kikwete kaumuumbua,
    Hawa marafiki sana, Itakuwa wewe bua,
    Leo sana wajiona, ujinga wakusumbua,
    Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.

    Huna mpaka na nune, Kambota wala jaani,
    Leo wewe ujivune, kumbe wenda majilini,
    Sema sana utukane, itafika arobaini,
    Kambota acha ujuha, Lowassa hasafishiki.

    Kaditamati natua, mbele sitaendelea,
    Kwa hapa naomba dua, wadudi anisikia,
    Ninamuomba mulua, Kambota aone jua,
    Kambota chumia tumbo, hebu tumia ubongo.

    Nkwazi Mhango

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget