Sunday, 8 April 2012



Mwasisi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mzee Edwin Mtei, amezungumzia uteuzi wa wajumbe wa Tume ya Kuratibu Maoni ya Katiba iliyotangazwa majuzi na Rais Jakaya Kikwete.Katika bandiko lake kwenye mtandao wa jamii wa Jamii Forums,Mzee Mtei amepongeza hatua ya Rais Kikwete kuteua Tume hiyo na hatua nzima ya kuanzisha mchakato wa mabadiliko ya Katiba tuliyonayo sasa.

Hata hivyo,mwanasisasa huyo mstaafu ambaye aliwahi kuwa Gavana wa Benki Kuu katika Serikali ya Awamu ya Kwanza,ameonyesha wasiwasi wake kuhusu muundo wa Tume hiyo huku akitafsiri kuwa muundo wa Tume hiyo unadhihirisha kuwa demokrasia ya kweli ni ndoto kwa Watanzania.

Katika bandiko hilo,Mzee Mtei amehoji mantiki ya kukosekana uwiano halisi kati ya wajumbe wa Tanzania Visiwani na wale wa Bara kwa kuzingatia kigezo cha idadi ya watu,na akagusia pia kukosekana kwa uwiano wa imani ya kidini miongoni mwa wajumbe (yaani Waislam na wasio Waislam).

Tayari kauli hiyo ya Mzee Mtei inaelekea kuzua mjadala hata ndani ya Chadema,ambapo Mbunge wa Kigoma Kaskazini kupitia chama hicho, Mheshimiwa Zitto Kabwe, amenukuliwa kwenye ukurasa wake wa Twitter akisema, "Yeyote anayeangalia #TumeyaKatiba kwa misingi ya #Dini za wajumbe amefilisika kimawazo, ni kirusi dhidi ya Utanzania wetu. Azomewe"


Bandiko halisi la Mzee Mtei ni hili hapa chini (BONYEZA PICHA KULIKUZA)




0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget