Nimekutana nayo huko Jamii Forums:
Kichuguu;Mimi kama mmoja wa wanachama waandamizi wa Jamii Forums ambapo nimekuwa mwanchama kwa karibu miaka mitano sasa tangu ikiwa Jambo Forums kabla ya kubadili jina na kuwa Jamiiforums nimekerwa sana na matamshi ya Makamu Mwenyekiti wa CCM kuwa forums hii ni ya vijana wa CHADEMA. Naona kuwa amenivunjia sana heshima yangu mbele ya wenzangu kwa kunipa image ya kuwa mimi ni mpiga propaganda wa CHADEMA.
Baada ya kutafakari kwa kina matamshi ya Pius Msekwa na jinsi yalivyoathiri image yangu kama mwanachama wa JamiiForums, nimeamua kumfungulia mashtaka ya defamation kwenye mahakama ya Douglas County hapa Omaha Nebraska nchini Marekani. Nimejadiliana na mwanasheria wangu ambaye amenipatia kifungu cha sheria kinachoniruhusu kumshitaki raia wa nchi ya nje kwenye mahakama hii, iwapo marekani ina uhusiano wa kibalozi na nchi ya mshitakiwa. Sasa hivi tuko katika hatua za mwisho mwisho za kukusanya ushahidi imara.
Nimeshapata nakala za magazeti ya kiswahili na kiingereza ila nimekuwa natafuta video clip yenye kumwonyesha Msekwa akiwa anasema maneno hayo. Vile vile bado tunashauriana kiwango cha malipo ya Punitive Damages na Compensatory Damages; mwanasheria anashauri kuwa viwango hivyo vipimiwe zaidi kwa kuangalia jinsi gani Msekwa binafsi na chama chake walivyofaidika au watakavyofaidika kutokana na matamshi yake hayo, na kwa kiasi kidogo jinsi gani yalivyoathiri image yangu binafsi kama mwanachama mwanadamizi ambaye hujitambulisha kwa wenzagu wote kuwa mimi ni Premium Member wa JamiiForums.
Tukikamailisha taratibu zote, nitawaarifuni au mtasikia kwenye vyombo vya habari Msekwa akiwa subpoenaed kwenye kesi hii ambayo pamoja na mambo mengine ninataka kuwadhibiti wanasiasa wasiwe wanaropoka mambo bila kuwa na uhakika nayo.
Ngoma inogile
That's commendable. Mara nyingi CCM wanajibu hoja nzito kwa majibu mepesi na rahisi au yasiyohusiana na hoja. Ni rahisi kuwaelewa kwa hilo, watawezaje kujibu hoja nzito zinazotolewa katika kurasa za JamiiForums kama sio kwa kupindisha hoja tu?. Hata kama JamiiForums ungekuwa mtandao wa CHADEMA, -eti hoja kama ya ufisadi haifai kujibiwa kwa vile tu imejitokeza katika mtandao wa CDM (assuming JF ni ya CDM)? Na pia tusisahau kuwa mtaji mkubwa wa CCM katika udhaifu huu ni ignorance ya Watz.
ReplyDeletehiyo move itakuwa fundisho kwa watawala wachovu wenye kuamini bila ya wao nchi haitosonga mbele.
ReplyDeleteHizo ni siasa za kijinga jamiiforum hata wawo imewasaidia sio chadema hio ni aibu yawo na ufisadi umewakumba!aibuuuuu......
ReplyDeleteKama na yeye haangalii na kuchangia kwenye JF alijuaje kama ina maeneo yanayokosoa CCM? Hao ndiyo members wenyewe wa JF wanajificha ili wasijulikane. Kasome JF, kasomeshwa kwenye JF na kajua Ukweli sasa kulinda ulaji wake kwa wanyamapori anainung'unikia JF. Acha hizo Msekwa!
ReplyDeleteni vizuri sana ashtakiwe tene itakuwa chachu kama anamengine mengi ambayo si yakufaa yaibuke ashtakiwe hata mara mia elfu! unajua hawa wazee hawana hoja kabisa ni kula tu wanangalia! msekwa amechoka sana angepumzika kisiasa! ccm imekwisha wangekubali hilo! na JK ndo kaimaliza kabisa maskini! wanabaki kusema ooh chadema wahuni, jamii ya chadema,lisiwaingie akilini kuwa watu wamefunguka macho!
ReplyDeleteCCM wanatumia technic kama ya wakoloni kutawala,wanatumia ignorance,angalia hata igunga wamepatia kula nyingi sehemu primitive,sehemu ambazo hazina umeme hazijui hata aza ya mgao wa umeme,mtu akisoma tu anawachukia.Wasomi wengi vyuoni wanawachukia.Hii inafanana na wakati wa ukoloni,Waafrika walipopata elimu walidai uhuru mfano Nkhuruma,nyerere,mandela etc.Nasisi wasomi tusaidie kuutoa ukabaira wa rushwa uliowekwa nchini na CCM.Nchi ya ten percent taifa litatushinda,tutakalia kuomba misaada hadi mwisho wa dunia huku mapato ya nchi yanaishia kwa wajanja,wao ndio vinara wa kwenda kuomba misaada.Kuomba misaada ni aibu,wao mbona hawatuombi.Mtu akiongea mambo mazuri kama JF wanachukulia unawasema,kwa hiyo watu wasiongee haki kisa CCM imefanya vibaya.
ReplyDeleteMimi naona kama nia ya forum hii ni kutoa nafasi kwa wabongo kutoa dukuduku zao hakuna haja ya kumfungulia huyu mzee mashitaka. Huyu ni mtu mchovu wa siasa. Ni part of the problem kwa usaliti wa VISION ya JKN. Kama unainsist kudai pesa bila shaka tutakuona na wewe ni mroho tu wa pesa kama hawa mafisadi wa CCM. Tuliza tu ball wacha mtandao ufanye kazi. kwamba ni mali ya nani sio hoja ndugu. Hapa tunabonga watu wote, wanachadema, wanaCCM asilia, kwa ujumla kila mtu mpambanaji.
ReplyDeletehayo ndio yale baba wa taifa aliita 'kansa ya uongozi', hila na vitisho imekuwa mbinu yao rahisi kujibu hoja za msingi, inatumika hoja ya nguvu badala ya nguvu ya hoja. Wana uvivu wa kufikiri na kutumia akili..! Precious is expensive.
ReplyDeleteNo! big NO, kama ikiwezekana akapanda kortin ni jambo jema ili kuongeza umakini kwenye kauli zinzo jumuisha Generalize mara nyingi hupelekea kupotosha Jamii nakuficha ukweli. Uponyaji utakuja Tanzania kwa kujadili uhalisia "Realities", inabidi kusukuma mpaka tufike hapo hata kama ikibidi kwenda mahakamanini, kesho na CHADEMA watatumia mbinu hoyo, watakuwa wamefundishwa na nani? CCM! Go ahead, if at all your not joking.
ReplyDeletendo wakti wa kufundisha adabu watu kama hao.Awe wa CHADEMA au wa CCM kama tu hoja zake zina mashiko ni ruksa kama Mwinyi kutu[pia JamiiF.Hii ndio maana ikaitwa JF maana yake wanajamii wote regardless chama gani.Hata kama wewe ni wa chadema as long as unachosema ni kweli acha useme bana.
ReplyDeletehii keshi haifiki tu huko mahakamani? yapelekwa na konokono nn? mbwe mbwe nyingine ......
ReplyDeleteJadilini na mambo mengine yenye manufaa zaidi kwa nchi kuliko hizi propaganda za vyama.
ReplyDeleteWananchi wanamatatizo mengi sana ya kutafutiwa ufumbuzi kuliko haya
POLITICS IN EVERYTHING, NOTHING NEW OF IMPORTANT IN THIS FORUM
ReplyDeletemsekwa ataisoma namba jaman
ReplyDelete