Kadrinali Peter Turkson ambaye ni Mghana anatajwa kuwa miongoni mwa wanaoweza kumrithi Papa Benedikti wa 16 ambaye atajiuzulu mwisho wa mwezi huu. Iwapo Turkson atafanikiwa kuwa Papa, atakuwa mtu mweusi wa kwanza kushika nafasi hiyo ya ukuu wa Kanisa Katoliki.Moja ya mambo yanayozungumzwa kuhusu Kardinali huyo ni mtizamo wake kuhusu kukua kwa Uislamu duniani.Licha ya kuongea lugha yake ya asili ya Fante na lugha nyingine za asili za Ghana, Kadrinali Turkson anaongea pia Kiingereza, Kifaransa,Kitaliano,Kijerumani na Kiyahudi.Pia anafahamu Kigiriki na Kilatini.
'Papabili' (Mapapa watarajiwa) wengine ni kama ifuatavyo
Kardinali Luis Tagle wa Ufilipino
Kardinali Angelo Scola wa Italia
Kardinali Christoph Schoenborn wa Austria
Kardinali Odilo Pedro Scherer wa Brazili
Kardinali Leonardo Sandri wa Ajentina
Kardinali Ginafranco Ravasi wa Italia
Kardinali Marc Ouellet wa Kanada
Kardinali Timothy Dolan wa Marekani
Kardinali Joao Braz de Aviz wa Brazil
Kardinali Peter Erdo wa Hungary
Mwafrika mwingine anayetajwa kuwa anaweza kuwa mrithi wa Papa Benedikti wa 16 ni Kardinali Francis Arinze wa Nigeria (pichani chini)
0 comments:
Post a Comment