Tuesday, 13 January 2009

Venance George, Morogoro
BARAZA Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) limesema kauli iliyotolewa juzi na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu kupinga oparesheni Sangara inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), si kauli ya waislamu wote.
Akizungumza mjini Morogoro kwa niaba ya Kaimu Mufti wa Tanzania,
Shekhe Suleiman Gorogosi, mratibu wa habari wa Bakwata, ustadhi Issa Mkalinga alisema kauli hiyo ni ya waislamu wachache ambao wamekuwa wakitumiwa na viongozi wa kisiasa kwa manufaa binafsi.
Ustadhi Mkalinga pamoja na Mkurugenzi wa Utawala, ustadhi Karim Mataliwa, aakizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya kaimu mufti huyo ya kutembelea mikoani kuhamasisha uhai wa baraza, alisema baraza halitambui kauli hiyo na wala halijihusishi na mambo ya siasa.
"Ujue tunaelekea kwenye uchaguzi mkuu hapo mwakani, hivyo wako baadhi ya wanasiasa wanatumia mwanya wa majukwaa ya dini kupeleka ujumbe wao," alisema.
Akizungumzia ziara ya kaimu mufti mkoani Morogoro, Mkurugenzi wa Utawala alisema kuwa ziara hiyo ni sehemu ya utaratibu aliyojiwekea kaimu mufti ya kutembelea baraza katika mikoa yote Tanzania na kwamba kaimu mufti ametembelea Dodoma na Morogoro na atatembelea mikoa mingine.
Ustadhi Mataliwa alisema lengo la ziara hizo ni kutaka kujua uhai wa baraza na matatizo yanayolikabili baraza katika ngazi hizo ikiwa ni pamoja na kuhimiza kufanya maandalizi ya uchaguzi wa viongozi kuanzia ngazi ya msikiti hadi taifa utakaoanza kufanyika mwezi April mwaka huu.
Wakati huo huo, katika mahojiano na baadhi ya waumini wa dhehebu hilo, mkoani Morogoro wameunga mkono kauli ya Bakwata na kudai kuwa viongozi wa dini ni vema wakafanya shughuli zao za kiroho na kuwaacha wanasiasa kufanya kazi zao za siasa.
Mmoja wa waumini hao, Ismael Rashid, alisema tamko lililotolewa na waislamu katika kongamano la jijini Dar es Salaam la kudai kuwa Chadema haina manufaa na msaada wowote kwa uislamu si maneno ya kiungwaana na si vema kukipakazia chama hicho kwamba ni kikabila na cha kibinafsi.
Rashid ambaye pia ni kiongozi wa chama cha Jahazi asilia mkoani Morogoro alisema hatua iliyochukuliwa na Chadema ya kuacha kuunga mkono vyama vya CUF na Sauti ya Umma (SAU) ilikuwa ni sahihi kwa sababu chadema walisimamisha mgombea ubunge katika jimbo la Mbeya vijijini lakini vyama hivyo vilimwekea pingamizi mgombea huyo na kuenguliwa.
"Pingamizi hilo lilisababisha mgombea ubunge wa Chadema akaenguliwa kugombea
nafasi hiyo, sasa iweje chadema iwaunge mkono?" alihoji Rashid .
Alisema chama cha Chadema hakiungi mkono kampeni za mgombea wa CUF kwa mdai kuwa chama hicho, mwakani inakusudia kusimamisha mgombea wake katika jimbo hilo kwa hiyo kama Chadema ikiunga mkono CUF itashindwa kusimamisha mgombea wake hapo mwakani.


CHANZO:Mwananchi

2 comments:

  1. kaka Evarist,

    Nimepita kibarazani kwako kuperuzi kidogo.

    Ahsante kwa kutuhabarisha.

    ReplyDelete
  2. Afadhali iwe ilivyosemwa kwamba lile lilikuwa tamko la waislamu wachache. Nilistuka kusoma habari ile ya mwanzo. Tumefika mahala dini zinatumika kamamtaji wa kisiasa. Huu unaweza kuwa mwanzo wa mparaganyiko.


    CHADEMA kuwagomea CUF mimi naona ulikuwa uamuzi sahihi kabisa. Haiwezekani mwuwaunge mkono watu ambao kule Tarime walionyesha dalili ya wazi kuwaharibia (iwe kwa kujua ama kutokujua) na kama vile haitoshi, wanampinga mgombea wenu!

    Nadhani ndoa ya upinzani ina mushukeli mkubwa. CHADEMA wakitaka kufanya vizuri bora wawe kivyao vyao. Vyama hivi vingine haviaminiki na hata nguvu yao piani suala la mjadala.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget