Thursday, 22 January 2009

Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakifanya patrol hapo Mlimani (UDSM).Picha kwa hisani ya MICHUZI JR.

Nilimaliza ngwe yangu hapo Mlimani (UDSM) takriban miaka kumi iliyopita.Kuna yaliyobadilika kwa kipindi cha miaka mitatu niliyokuwa hapo,na kuna mengine yamebaki kama yalivyo.Kwa kifupi sana,katika miaka hiyo mitatu,sikumbuki kama kuna academic year iliyopita pasipo mbinde ya aina moja au nyingine kati ya wanafunzi na serikali.Na kila mara chanzo kilikuwa kilekile:FEDHA.

Binafsi nadhani chanzo cha matatizo ya migogoro kati ya wanavyuo na serikali ni mapungufu katika sera nzima ya uchangiaji gaharama za elimu ya juu.Kwa nchi masikini kama yetu,haihitaji busara kufahamu kwamba kuna wanafunzi lukuki wanaotoka katika familia ambazo kumudu gharama za maisha ya kila siku ni mgogoro,achilia uwezo wa kumudu gharama za kumsomesha mtoto chuo kikuu.Kwa mantiki hiyo,ajenda ya kulipa ada na gharama nyingine kwa silimia 100 ni suala lisilowezekana kwa wanafunzi wanaotoka familia za aina hii,ambao kwa hakika ni wengi zaidi.

Kinachohitajika ni usimamizi mzuri wa mikopo kwa wanafunzi wa aina hiyo.Hii ni investment nzuri kwa future ya taifa letu.Iwapo serikali itakuwa na nia ya dhati kuhakikisha kuwa wakopeshwaji wanarejesha fedha hizo,ni dhahiri itajitahidi kuwatengenezea mazingira mazuri ya ajira pindi watapohitimu masomo yao...kwa vile ajira hiyo ndio inayotarajiwa kuwawezesha kulipa mikopo hiyo ya serikali.

Kama tunaweza kuwakopesha wabunge mashangingi yenye thamani ya mamilioni ya shilingi,naamini kabisa kuwa kuwakopesha wanavyuo wetu ni swala linalowezekana pasipo kusababisha hizi mbinde za kila mwaka au muhula wa masomo.Tatizo sio sera ya uchangiaji gharama per se bali,kama ilivyo kwenye maeneo mengine mengi,ni utekelezaji wa sera hiyo.FFU wanaweza kutuliza ghasia chuoni hapo kwa muda lakini hawawezi kuwa ufumbuzi wa tatizo hilo.

Related Posts:

  • SARAH PALIN NI "KILAZA"?Kwa lugha za Mlimani (UDSM) kilaza ni mtu ambaye shule haipandi.Kwake siku ya seminar presentation ni kama kutoa ushahidi kwenye kesi mahakamani ambayo inaweza kumpelekea kunyongwa.Ratiba ya mtihani ikitoka basi kwake inakuwa… Read More
  • KULIKONI UGHAIBUNI-80Asalam aleykum,Katika makala yangu iliyopita,nilizungumzia kuhusu kile ambacho wachambuzi wa siasa za kimataifa wanakiona kama kurejea kwa kasi kwa mbio za silaha (arms race) zenye uwezo mkubwa na wa kisasa zaidi kuliko hapo … Read More
  • UBABE HAUWEZI KUTATUA MATATIZO YA MLIMANI (UDSM) Askari wa kikosi cha kutuliza ghasia wakifanya patrol hapo Mlimani (UDSM).Picha kwa hisani ya MICHUZI JR.Nilimaliza ngwe yangu hapo Mlimani (UDSM) takriban miaka kumi iliyopita.Kuna yaliyobadilika kwa kipindi cha miaka mitat… Read More
  • MAANDALIZI YA HARUSI YA GHETTO BOY (UDSM CLASS OF 99)The family of the late Hon. Richard Mwakasege (MP) of Mbeya Town would like to inform you:Hon./Rev./Prof./Mr 7Mrs./Mr./Miss................................................................................That their beloved son… Read More
  • R.I.P Profesa Mushi: Daima Tutakukumbuka kwa PS 100 Pale Mlimani (UDSM)Nimepokea kwa masikitiko kifo cha Mhadhiri wangu wa zamani Profesa Samuel Mushi.Nilikuwa mwanafunzi wa Profesa Mushi tangu nilipojiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Septemba 1996 hadi nilipomaliza mwaka wa kwanza July 1997… Read More

1 comment:

  1. Hili tatizo nahisi kama linapuuzwa kiaina kwa jinsi linavyojirudia:-(

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget