Padre Privatus Karugendo amekuwa akisimulia mkasa ulisababisha yeye kusimamishwa,na hatimaye kuvuliwa,daraja la upadre.Kma nilivyoeleza katikapost hii,japo sifahamiani personally na Mtumishi huyu wa Bwana,alikuwa columnist mwenzangu katika jarida laRaia Mwemahadi nilipolazimika kuchukua "sabbatical leave" ya uandishi wa makala.Pia,maandiko mbalimbali ya Padre Karugendo yalinipa changamoto kubwa hadi nikaamua kujiingiza katika anga za uandishi wa makala kwenye magazeti mbalimbali huko nyumbani.
Unaweza kusoma SIMULIZI kuhusu chanzo cha mkasa uliopelekea Padre huyo kusimamishwa na hatimaye kuvuliwa upadre kwaKUBONYEZA HAPA(Sehemu ya Kwanza) naHAPA(Sehemu ya Pili) na HAPA (latest).Blogu hii itaendelea kuwaletea simulizi hizo kadri zinavyochapishwa gazetini.Mkasa uliomkumba Padre huyu unanigusa sio tu kwa vile napenda makala zake au kwa sababu tuliwahi kuandikia gazeti moja,bali pia kwa vile kwa namna flani yeye,kama mie,ni majiruhi wa mfumo uliozowea kupongezwa na kunyenyekewa lakini usiotaka kusikia criticism au mawazo mbadala.
Dah!! Haya. Mimi ntasoma tuu na wenyewe watamalizana. Kali kwelikweli.
ReplyDeleteAsante Kaka Evarist
kak Evarist, nimepita kukusabahi.
ReplyDeleteAhsante kwa kunitembelea na kunipa changamoto.
Najifunza mengi kupitia kwenu wanblog wenzangu.
Hii ni habari ya kusikitisha sana.
ReplyDeleteNimesoma maoni ya wasomaji mbali mbali katika blog ya kaka Bwaya, imenisikitisha sana.
kwa leo sitasema mengi lakini napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza kwa ujasiri wake.
Ahsante sana kaka Evarist kwa kutuhabarisha.