Mambo mengine huku Ughaibuni ni vituko vitupu.Kuna watu wanafuga majoka makubwa na kuyalea kama watoto wao,kuna wanaofuga panya mithili ya paka,na wengine wamegeuza tumbili kuwa watoto wa kambo.Na matunzo wanayopewa mbwa na paka hayatofautiani sana na anasa wanazofaidi watoto wa wabaka-uchumi wetu (mafisadi).
Kuna vijibwa flani vimekuwa kwenye chati kwa muda mrefu kutokana na kushebedukiwa na watu maarufu.Nadhani ushakiona ki-chihuahua cha Paris Hilton,kijibwa kidogo mithili ya paka.Sasa imeibuka fasheni mpya ya “kitimoto pimbi”,yaani nguruwe wadogo kupindukia.
Jioni hii kipindi cha Live From Studio Five katika kituo cha runinga cha Channel Five kimezungumzia fasheni hiyo mpya ambayo kwa hakika inaweza kuzua songombingo na maustaadhi pindi ikitua Bongo,almaaruf kwa ku-copy na ku-paste mengi ya yanayojiri anga hizi.
0 comments:
Post a Comment