SOMA KAULI ZA BABU HUYU HAPA CHINI KISHA UELEWE KWANINI NATOA WITO AONEWE HURUMA KWA KUPUMZISHWA.
Na Keneth Goliama, Mbeya
MBUNGE wa kuteuliwa wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Kingunge Ngombale Mwiru, amewashutumu viongozi wanaounda makundi ndani ya chama hicho na kuwaita waliochanganyikiwa.
Mbunge huyo aliapa kuwa matajiri wasipewe kipaumbele katika uongozi, kwani watu wakishakuwa na fedha wanajiingiza katika siasa kufanikisha malengo yao ya kibiashara.
Kingunge ambaye pia ni Naibu Kamanda UVCCM Taifa,aliyasema jana wakati akiwaapisha Makamanda wa Mkoa wa Mbeya kwenye ukumbi wa Mkapa.
Aliwataka makamanda hao kufanya kazi ya kuwashauri vijana na sio kuwaingiza vijana katika makundi yaliyopo ndani ya chama hicho.
Kingunge alisema kauli za baadhi ya viongozi kuwa, wabunge wengi wa CCM hawatarudi katika ubunge mwaka 2010 ni kweli kwa sababu kunahitajika mabadiliko katika uongozi ndani ya chama.
Hata hivyo, alisema wabunge hao wapya ni faraja kwa CCM kwa sababu watakuwa ni wakutoka ndani ya chama hicho.
Aliongeza licha ya Mkoa wa Mbeya ni mingoni mwa mikoa ambayo ilitoa watu waliokuwa mstari wa mbele kugombea uhuru , lakini sifa hiyo imeharibiwa na viongozi wachache.
Kingunge alisema baadhi ya viongozi mkoani hapa wanauhasama wa kugombea madaraka na kwamba sasa ugomvi huo unakiharibia chama.
Akiunga mkono jitihada za vijana wa mkoa huo kupambana na mafisadi, Kingunge aliwataka wasiache kutetea haki yao kwa sababu vijana ndio wenye nguvu katika maendeleo ya jamii na siasa.
Kingunge aliwaasa wanachama hao kukataa kurubuniwa na watu wenye fedha kwani kukubali kufanya hivyo ni kuua chama.
Baadhi ya viongozi wamefanikiwa kuwarubuni vijana kwa fedha ili waweze kujinufaisha wenyewe na kuharibu siasa mkoani hapa, alisema Kingunge
Alikionya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuwa, hakijui siasa ndio maanakimejaa matatizo matupu na uchaguzi wao ni ovyo na kwamba hakina uwezo wa kupewa kuongoza dola.
CHANZO: Mwananchi
HIVI ALIYECHANGANYKIWA NI NANI KATI YA KINGUNGE NA HAO ANAOWAITA "WAMECHANGANYIKIWA."MAJUZI,MTETEZI MAHIRI WA MAFISADI,YUSUPH MAKAMBA NAE ALITOA TAMKO LINALOSHOBIHIANA NA HILI LA KINGUNGE,MWANASIASA ALIYETUZUGA ENZI ZA MWALIMU KUWA NI MFUASI MAHIRI WA UJAMAA ONLY KUIBUKA MTETEZI MAHIRI WA MAFISADI.LEO,MIEZI MICHACHE KABLA YA UCHAGUZI MKUU,NAE ANAJITUTUMUA KUKEMEA MAFISADI!?HUKU NI KUCHANGANYIKIWA KUNAKONASIBISHWA NA KUZEEKA VIBAYA.
0 comments:
Post a Comment