Saturday, 27 February 2010

Pinda(2)

na Mwandishi Wetu, Urambo

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda, amemmwagia sifa kemkem Spika wa Bunge, Samuel Sitta akisema amejenga Bunge lenye sifa na umakini.

Pinda ambaye majuzi alimmwagia sifa Mbunge wa Igunga, Rostam Azziz (CCM) akiwataka wananchi wake wampime kwa kazi yake ni si kwa maneno ya bungeni, alisema Sitta amekuwa anaongoza Bunge kwa nia nzuri, na kwamba wanaolalamikia kazi yake ni wapotoshaji.

Alikuwa akihutubia wananchi katika Uwanja wa Jamhuri mjini hapa juzi, akasema Sitta ambaye ni Mbunge wa Urambo, amelifanya Bunge lisifiwe hata nje ya nchi.

Katika kusisitiza hili, Pinda alisema: “Hata watu wa nje wanalisifu Bunge letu…wanasema naam, hili ndilo Bunge…Bunge likicharuka kuhusu ufisadi wanasema hata si bure, nani asiyejua ufisadi? Ufisadi si rushwa? Bunge linachofanya ni watu wawe waadilifu.”

Aliwataka Watanzania waungane katika vita dhidi ya rushwa, kwani imesemwa tangu zamani kwamba rushwa ni adui wa haki.

Kwa takribani miaka miwili, Sitta amekuwa na uhusiano mbaya na baadhi ya vigogo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wengi wakiwa wabunge wenzake, kuhusu anavyoliendesha Bunge.

Miongoni mwa walioathirika kwa “kazi nzuri ya Sitta” ni Rostam ambaye pamoja na rafiki yake Edward Lowassa (Monduli – CCM) walihusishwa kinamna na kashfa ya Richmond, ambayo ilisababisha Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa Waziri Mkuu.

Kutokana na msimamo wa Sitta na athari za Kamati ya Mwakyembe, CCM iligawanyika makundi mawili, moja upande wa Sitta jingine likiwa upande wa Lowassa na Rostam.

Uhasama wa makundi hayo uliongezeka na kujikita katika vikao vingine vikuu vya maamuzi vya CCM, kiasi kwamba mwaka jana, wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC) walimbana Sitta katika moja ya vikao vyao, wakapendekeza avuliwe uanachama na afukuzwe ubunge, kwa maelezo kuwa anatumia vibaya nafasi yake kwa kuiaibisha CCM.

Sitta aliponea chupuchupu baada ya Rais Jakaya Kikwete kuunda Kamati ya Mwinyi, ambayo kwa muda sasa imekuwa ikihaha kuwapatanisha mahasimu hao; na sasa imefanikiwa kupunguza uhasama wa wazi miongoni mwao.

Katika kikao cha 18 cha Bunge kilichomalizika siku chache zilizopita, Sitta aliwashangaza wananchi alipofunga mjadala wa Richmond, huku akitarajiwa atumie fursa hiyo kuibana serikali itekeleze maagizo 23 ya Bunge kuhusu watu waliojihusisha na kashfa hiyo.

Sitta pamoja na wabunge waliokuwa wamejipambanua kuwa ni wapiganaji vita dhidi ya ufisadi wamelazimika kunywea, licha ya kutambua kuwa maazimio muhimu yaliyomtaka Rais Kikwete kuwajibisha waliokumbwa na kashfa hiyo hayakutekelezwa.

Katika kikao cha NEC kilichoisha hivi karibuni, Sitta aligoma kusuluhishwa na Lowassa na kundi lake, akidai kwamba hana ugomvi binafsi, bali anapambana na ufisadi. Kamati ya Mwinyi imeongezewa muda ili iwapatanishe mahasimu hao.

Mara baada ya kikao cha NEC, Pinda alianza ziara ya wiki sita mkoani Tabora; na alipofika Igunga, alitoa kauli ya kumtetea na kumsafisha Rostam kwa kauli ambayo baadhi ya wachambuzi walidai inalidhalilisha Bunge, kwani ilionekana kana kwamba “maneno ya bungeni” si maneno ya maana kwa wananchi kuyatumia kumpima mbunge wao.

Aliwataka wananchi wa Igunga wampime Rostam kwa kazi zake jimboni, si kwa “maneno ya bungeni;” Bunge lile lile linaloongozwa na Sitta.

Jana Waziri Mkuu alitembelea Wilaya ya Sikonge. Ziara yake mkoani Tabora inatarajiwa kuhitimishwa leo.

CHANZO: Tanzania Daima

Related Posts:

  • MAKALA NDANI YA GAZETI LA RAIA MWEMAUkurasa wa mbele wa gazeti la RAIA MWEMAMakala kamili bonyeza hapa----------------------------------------------------------------------------------------------------------------SHUGHULI YA 50 CENT NDANI YA ABERDEENJana kulik… Read More
  • KULIKONI UGHAIBUNI-86Soma makala nyingine mbili hapaAsalam aleykum,Moja ya mambo nayopendelea kufanya pindi muda unaporuhusu ni kuangalia runinga.Lakini naweza kusema kwa kujiamini kabisa kwamba mahaba yangu kwa runinga yamekuwa ni sawa na mithil… Read More
  • KULIKONI UGHAIBUNI-83Asalam aleykum,Kwanza nianze kwa salamu za rambirambi kwa familia,ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu Salome Mbatia,aliyetutoka hivi majuzi kutokana na ajali ya gari.Sote ni wasafiri,mwenzetu ametutangulia tu,Bwana ametoa Bwa… Read More
  • MTANZANIA UGHAIBUNI-3Ama kweli ni rahisi kupanga sera na kutegemea ifanikiwe lakini ni habari nyingine kwa mpanga sera kuwa sehemu ya utekelezaji huo.Hilo limejihidhirisha katika taarifa kutoka nchini Marekani ambapo maafisa wa mambo ya nje wa nc… Read More
  • LEO MAKALA MBILI KWA MPIGONadhani sio wazo baya kuja na makala mbili kwa mpigo.Usichoke kusoma,au kama namna gani vipi soma moja halafu nyingine iweke kiporo uisome baadae.KULIKONI UGHAIBUNI-82Asalam aleykum,Siasa za kimataifa zina vituko vyake,na pen… Read More

0 comments:

Post a Comment

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget