Saturday, 30 October 2010



Ndugu Watanzania wenzangu wote kwa ujumla mtakaosoma ujumbe huu, Salaam toka Mbeya Vijijini, ndio tumeanza mikutano midogo ya kufunga kazi asubuhi hii na tutahitimisha baadaye.

Ninashukuru sana kwa maneno ya heri kwa siku yangu ya kuzaliwa hapo jana na ningekuwa sina shukrani kama ningeacha ipite bila kusema asante kwa maneno mema mliyonipatia humu na kwenye facebook na hata waliopata nafasi kwa njia ya simu. Ninawashukuru vile vile kwa mashauri mbalimbali, na pia kwa sala na dua zenu.

Ninashukuru sana na ninaona fahari kuwa ni mwanachama mwenzenu.

Kampeni zote zinaisha leo na kesho ni siku ya Uchaguzi Mkuu kama mnavyofahamu. Kwa upande wangu nimetembelea karibu maeneo yote ya nchi yetu kubwa, nimekutana na watu mbalimbali na nimeona mengi. Nimeona mengi yenye kutia matumaini na faraja na nimena mengine ya kuhuzunisha na kukatisha tamaa. Yote kwa ujumla yake yamenipa picha ya kuelewa zaidi Taifa letu hasa kuhusu mafanikio tuliyoyapata mpaka hivi sasa na changamoto tulizonazo.

Ninaelewa vizuri zaidi sasa kupitia mang’amuzi binafsi hali ya Taifa letu ilivyo na ya kwamba ni lazima tubadili mwendo na huko tunakokwenda maana tutafika mahali ambapo tutashindwa hata kujiuliza tulifikaje. Watu makini hawawezi kuendelea na njia ambayo wanajua wamepotea. Kuendelea kung’ang’ania kwenda wakati mnajua mmeshapotea ni kutukuza kiburi cha kujiona. Taifa letu limepotea njia na hata kama tukijitahidi kwa nyimbo na masimulizi mbalimbali kuhalalisha huko tunakokwenda bado tutakuwa tumepotea.

Ni kwa sababu hiyo nilipoombwa kugombea Urais nilitambua uzito wa mzigo huu mkubwa kwani utahusiana moja kwa moja na kubadilisha mwelekeo wa taifa letu na kuanza kutengeneza pale palihorabiwa, kuinua kilichoanguka na kumwagilia kilichoanza kunyauka. Hili linahitaji mawazo mapya, uthubutu wa kiuongozi na mtazamo mpya wa nini Taifa letu linahitaji. Ndugu zangu, Taifa letu linahitaji mabadiliko makubwa ili tuweze kujipa sisi wenyewe na watoto wetu nafasi ya kuweza kufanikiwa huko mbeleni.

Mabadiliko haya siyo mabadiliko ya mapambo yaani kuhamimisha maua na vitambaa sebuleni wakati nyumba inanuka na nichafu. Wote mliosikiliza au kumwangalia mgombea mwenzangu jana ni wazi hana ahadi ya mabadiliko yoyote makubwa isipokuwa mwendelezo wa yale yale yaliyotufikisha hapa. Ni kutokana na hilo natambua kuwa kura ya kesho siyo kura ya kawaida; siyo kura kama ya 2005 au ya miaka kabla yake.

Kura ya kesho ni kura ya kuchagua kuendelea na vile tulivyo kwa miaka mitano ijayo au kubadilika ili tuanze upya kwa njia sahihi na kwenda ambako sote tunakujua tunataka kwenda. Ninaamini tunachohitaji ni mabadiliko yatakayoanzisha mwamko wa kuanza kulijenga upya taifa letu. Hili ndilo lililonifanya nikubali pale Chama changu kiliponiomba ninyanyue bendera ya Chadema kwenye uchaguzi huu katika nafasi ya Urais.

Naweza kuwaahidi mengi na kwa maneno matamu ya kila aina. Hata hivyo ninawaahidi kitu kimoja kwa uhakika wa asilimia 100. Mkinichagua kuwa Rais wenu na mkiwashawishi ndugu, jamaa na marafiki zenu kufanya hivyo nami nikachaguliwa, nitawapatia uongozi ambao utaifanya miaka 49 iliyopita kuwa ni ya masimulizi ya njozi za jinamizi kwani nitaongoza timu ya watu ambao watakuwa wamejitokea muda, elimu, ujuzi na vipya vyao katika kujenga taifa letu upya. Katika miaka mitano ijayo tutafanya mambo ambayo CCM na utawala wake imeshindwa kufanya kwa karibu miaka hamsini.

Tutawapa nafasi Watanzania hatimaye nao wafurahia matunda ya uhuru wao na vile vile kuweza kuanza kujenga Taifa la kisasa ambalo litakuwa ni tamanio nakinara cha mabadiliko ya kiutawala, kiuchumi na kiutendaji katika Bara letu. Tuna uwezo, tuna sababu na tuko tayari kuwatumikia.

Naomba sana kura zenu hapo kesho ili niwe Rais wenu katika awamu ya tano. Kura yako ina nguvu ya kubadilisha mwelekeo wa taifa letu. Usiuze, usiache kuitumia na pale utakapoitumia itumie kwangu, kwa wagombea Ubunge Chadema na wagombea wetu wa Udiwani ili tuweze kuhakikisha yote tuliyowaahidi tutayatimiza na zaidi.

Msiwe na shaka, hata toka Ikulu nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu wa mitandao hii na kuwapa taarifa mbalimbali moja kwa moja na kujibu maswali mtakayokuwa nayo kuhusu serikali yenu pale inaponipasa mimi kutolea kauli. Asanteni!!


Mungu Ibariki Tanzania Mungu Ibariki Afrika.


DR W P SLAA - MGOMBEA WA URAISI CHADEMA

Tuesday, 26 October 2010


Nimetumiwa barua pepe yenye habari ifuatayo nami naiwasilisha kama ilivyo


Taarifa kutoka Tunduma, mpakani mwa Tanzania na Zambia mkoani Mbeya zinasema kuwa lori la kampuni ya Azam linalomilikiwa na mfanyabiasha maarufu Bakhresa leo hii tarehe 18 Oktoba, 2010, limekamatwa likiwa na shehena kubwa la karatasi za kupigia kura zitakazotumika uchaguzi mkuu Oktoba 31.
Maafisa wa TRA tunduma walishtuka baada ya kukuta karatasi hizo za kupigia kura zimefichwa kwenye shehena ya vipodozi. Inasemekana kuwa mzigo huo wa karatasi za kupiga kura ulitokea Afrika Kusini na ulipakiwa kwenye gari la Azam kutoka kwenye gari lililotoka na mzigo kutoka Afrika Kusini.
Taarifa zinasema kuwa lori hilo linashikiliwa na TRA na mzigo huo umekuwa sealed. Kuna hofu kuwa vigogo wenye njama za kuiba kura wanaweza kujaribu kufuta ushahidi kuhusu kukamatwa kwa karatasi hizi za kupiga kura.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, karatasi hizo za kupiga kura tayari zimewekewa tiki kumchagua Jakaya Kikwete wa CCM na lengo ni kuwa zisambazwe kwenye vituo mbalimbali vya kupigia kura nchini na zihesabiwe kama kura halali.
Tafadhali mwenye taarifa zaidi kutoka mpakani Tunduma atupatie ukweli wa jambo hili
" ........ Wadau huu ni ukweli mtupu magari mawili ya A.A.Bahresa (named Azam on board)T 501AEM na T 263 AJN yako hapa kituo kikuu cha polisi mkoa Mbeya,binafsi nimeona hizo karatasi za kura ambazo JK kapigiwa kura ya ndio na ziko kama karatasi milioni tano kwa haraka haraka hope police watatoa taarifa kamili,wametutoa nje sijui wanazichakachua "

Nawasilisha kwa taarifa na ushahidi

Add caption


WAINGEREZA WANA MSEMO "IF SOMEONE HAS SOMETHING BAD TO SAY ABOUT YOU,IT'S PROBABLY BECAUSE THEY HAVE DON'T HAVE NOTHING GOOD TO SAY ABOUT THEMSELVES",YAANI KWA KISWAHILI,UKIONA MTU ANA BAYA LA KUSEMA KUHUSU WEWE BASI PENGINE NI KWA VILE HANA JEMA LA KUSEMA KUHUSU YEYE MWENYEWE.

RAIS ALIYE MADARAKANI NI JAKAYA MRISHO KIKWETE.CHAMA KILICHO MADARAKANI NI CHAMA CHA MAPINDUZI.SASA CHA KUSHANGAZA,AJENDA KUBWA YA KIKWETE NA CCM IMEKUWA KUHUSU "KWANINI DAKTA SLAA HAFAI,KWANINI CHADEMA WAONGO,KWANINI AHADI ZA DKT SLAA/CHADEMA HAZITEKELEZEKI" NA UPUUZI MWINGINE KAMA HUO.HIVI RAIS ALIYEKUWA MADARAKANI MIAKA MITANO NA ANAYETOKA CHAMA AMBALO LIMETUTAWALA MIAKA NENDA MIAKA RUDI HAWANA LA KUTUELEZA KUHUSU WAO WENYEWE BALI KUMVALIA NJUGA DOKTA SLAA NA CHADEMA KANA KWAMBA AKINA LIPUMBA NA WAGOMBEA URAIS WENGINE WANAGOMBEA UBUNGE AU UDIWANI?

JIBU LIPO KWENYE HUO MSEMO WA WAINGEREZA.KIKWETE NA CCM HAWANA JIPYA AU ZURI LA KUWAELEZA WATANZANIA ZAIDI YA KUDURUFU AHADI ZA MWAKA 1995,2000 NA ZAIDI 2005.HAWANA JIPYA ZAIDI YA KUBAHATISHA MBINU YAO MAARUFU YA "TUPENI KURA TUMALIZIE TULIYOANZA AWAMU HII".YAANI TUWAPE TENA KURA WAMALIZIE KUMALIZA RASLIMALI ZA TAIFA? HELL NO!TUWAPE TENA MIAKA MITANO WAMALIZIE UBIA WAO NA MAFISADI KUSAFISHA KILA KILICHOPO.HAPANA,NO,NEVER!

WAMETUNYANYASA KIASI CHA KUTOSHA.
WAMETUDHARAU KIASI CHA KUTOSHA (NDIO MANA AHADI LEO HAWATAKI KUOMBA MSAMAHA KWA MAKOSA YA UFISADI)
WAMETUTESA KIASI CHA KUTOSHA.
UMEFIKA WAKATI WA KUWAAMBIA NOT ANY MORE. IMETOSHA.WAMETUIBIA VYA KUTOSHA LAKINI SASA TUKIWAREJESHA TENA MADARAKANI SIO TU WATATUFILISI BALI PIA TUTAONEKANA WAJINGA KWA KUWARUHUSU WATUFANYE WAJINGA.

CHAGUA DOKTA WILBROAD SLAA KWA TANZANIA MPYA YENYE NEEMA NA MAENDELEO
MSTAAFISHE KIKWETE KWA MANUFAA YA UMMA
WATIMUE MAFISADI TUREJESHE NCHI MIKONONI MWETU

INAWEZEKANA.TIMIZA WAJIBU WAKO KWA KUMPIGIA KURA DOKTA SLAA HAPO JUMAPILI



Sunday, 24 October 2010



Siku moja nilikuwa na mazungumzo na babu mmoja wa Kiskotish.Kwa vile ilikuwa ni safari ya masaa kadhaa kwenye treni kutoka mji mkuu wa Uingereza,London kuelekea mji wa kaskazini mashariki mwa Scotland,Aberdeen,tulipata wasaa wa kuongea mengi.Babu huyo ameshawahi kukaa Tanzania,na anajua maneno mawili matatu ya Kiswahili.Swali moja aliloniuliza,na ambalo limeendelea kuumiza kichwa changu hadi leo ni kwanini Tanzania ni masikini licha ya utajiri mwingi ilionao na watu wakarimu,wapenda amani na wenye kiu ya maendeleo.Sio siri,nilijiumauma kutoa jibu la kueleweka.

Uzuri kuhusu hawa wenzetu ni kwamba hawajui kumwonea mtu aibu.Babu huyo alinieleza waziwazi kuwa nimeshindwa kumpa jibu la kuridhisha sio kwa vile sifahamu kwanini Tanzania ni masikini bali nimeona aibu tu ya kutoa jibu sahihi.Na huo ni ukweli.Nilijua nikimwambia kwamba tatizo kubwa kwa maendeleo ya Tanzania ni uongozi,angeweza kuniuliza "kwani viongozi hao ni wakoloni au Watanzania wenzenu?"

Katika maongezi yetu babu huyo alinipa fundisho moja muhimu ambalo nadhani sote tunapaswa kulitilia maanani.Alinieleza kuwa zamani hizo wakati Uingereza inajengwa,Waingereza hawakuwa wanafikiria kuhusu mahitaji yao tu bali pia mahitaji ya vizazi vijavyo.Alifafanua kuwa kadri anavyoelewa,Waingereza wengi wanajibidiisha sio tu kwa ajili ya leo bali hata miaka 200 ijayo.Akanipa mfano wa namna walivyojenga treni za chini ya ardhi,hospitali zao kuubwa kama kijiji kizima,vyuo vilivyotapakaa sehemu kubwa za miji na maendeleo mengineyo.

Akatanabaisha kuwa wengi wa walioshiriki katika ujenzi huo wa Uingereza ya leo kwa sasa ni marehemu.Na akanikumbusha kuwa japo wakati wanajituma kujenga nchi yao walikuwa wanafahamun kuwa watafaidi matunda ya jitihada zao kwa muda mfupi tu kabla Mungu hajawachukua lakini hiyo haikuwakatisha tamaa kwa vile walifahamu kuwa vizazi vijavyo vingetaraji waliowatangulia wangetumia nafasi zilizokuwepo muda huo kuwaandalia mazingira mazuri ya kuishi.

Nifupishe stori.Jumapili ijayo tuna Uchaguzi Mkuu ambao binafsi nauona kama tukio muhimu kabisa kwa historia ya nchi yetu.Takriban miaka 50 baada ya uhuru kuna wenzetu wengi tu ambao wanaishi katika mazingira mabovu kuliko kabla ya ujio wa mkoloni.Lakini pia,kuna wachache ambao angalau wanamudu mahitaji ya msingi ya kila siku.Ni kundi hili ambalo ningependa kuelekeza rai yangu kwao.

Hebu tutafakari stori za huyo babu niliyekutana nae kwenye treni.Laiti kizazi chao kingeridhika na hali waliyokuwa nayo wakati huo basi huenda Uingereza ya leo isingekuwa imepiga hatua kama ilivyo sasa.Laiti wangekuwa wabinafsi wa kufikiria maslahi yao tu wasingejihangaisha na mipango ya maendeleo ambayo matunda yake yangeonekana baada ya vifo vyao.Lakini kwa vile waliweka mbele maslahi ya jamii badala ya maslahi binafsi,hawakusita kujenga msingi wa jamii ya Uingereza kwa wakati huo na karne kadhaa baadaye.

Tunaweza kuendelea kuwalaumu wakoloni kwa kukwaza maendeleo yetu.Lakini wakoloni walishaondoka takriban miaka 50 iliyopita.Sasa badala ya kupiga hatua,kuna nyakati tunajikuta tunarudi nyuma zaidi ya wakati wakoloni wanaondoka.

Na japo siwatetei wakoloni,lakini angalau wao walikuwa na excuse.Hawakuwa Watanzania wenzetu.Hawakuwa na uchungu na nchi yetu wala vizazi vijavyo.Vipi kuhusu viongozi wetu wa sasa?Hivi sio hawa waliosomeshwa bure buleshi lakini leo wanakataa katakata kuwa elimu ya bure haiwezekani?Kama iliwezekana wakati huo ambapo hatukuwa na maendeleo ya kutosha,kwanini ishindikane wakati huu ambapo tumeweza kugundua vyanzo mbalimbali vya mapato?

Tukiridhika na mishahara inayotuwezesha kwenda Twanga Pepeta kial wikiendi,au vikao vya bia kila jioni kisha tukasahau kuwa kuna wenzetu (na wengi wao ni ndugu zetu kabisa) huko vijijini hawana uhakika wa kifungua kinywa,wamesahau ladha ya chumvi kwenye mlo kwa vile chumvi imegeuka anasa japo iko kibwena huko Uvinza,sukari imegeuka muujiza hata huko Kilombero ambako wana kiwanda cha sukari na miwa inayozalisha sukari inaozeana mashambani.Kuna wenzetu ambao wali nyama au ugali nyama ni milo inayowezekana kwenye sherehe,misiba au wanapobahatika mara moja kwa mwaka kupelekwa hotelini licha ya maelfu kwa maelfu ya ng'ombe,mbuzi,kondoo na wanyama pori lukuki,sambamba na mchele,mahindi,mihogo,mtama,nk.

Sasa hali hii itaendelea hadi lini?Tunaweza kupuuza shida za wenzetu hawa ambao ni wengi kuliko sie lakini ni dhahiri kuwa ndani kabisa ya nafsi zetu tunateseka tunapokumbuka kuwa punje za wali tunazosafisha kwa minajili ya kuzitupa zinahitajika kwa udi na uvumba katika nyumba moja au nyingine.Hivi kama hawa "wazungu" na ubinafsi wao (hawa familia ni baba,mama na watoto.Habari za shangazi,binamu,mjomba,babu,bibi ni kama kachumbari kwenye mlo: inapendeza lakini sio muhimu). waliweza kuvikumbuka vizazi vijavyo na hivyo kujenga nchi zao hadi kufikia zilipo leo,wakni sie ambao familia ni zaidi ya mume,mke na watoto?

Kuna wenzetu wanaokumbatia mafisadi kwa vile tu wanahofia kuwa mafisadi hao wakiondoka basi nao hawatakuwa na namna ya kumudu maisha yao.Hiyo si kweli kwani hata nyakati za mkoloni kuna waliokuwa wanatumikia wakoloni na kuwakandamiza waafrika wenzao,lakini watu hao waliendelea kuwa hai,huru na kumudu maisha yao...tena kwa njia halali pasipo hofu ya kuonekana wasaliti.

Kura utakayopiga Jumapili ijayo ni zaidi ya kura yako binafsi.Ni kura kwa ajili ya memba wote wa ukoo wako (ambao katika mazingira ya kawaida kuna wengi tu wenye kuhangaika na maisha ya kila siku),rafiki zako wa zamani ambao baada ya kukosa nafasi ya kuendelea na masomo wakajaribu bahati zao kwenye kilimo lakini jitihada zao zinakwazwa na vyama vya ushirika vinavyojua kukopa zaidi kuliko kuuza mazao.Ni pamoja na wale ambao waliamua kufany kazi za wito kama ualimu au uuguzi lakini sasa wanajiuliza kama "wanafanya kazi ya Kanisa" kwani licha ya mshahara kuwa kijungujiko lakini pia hauna uhakika wa kufika katika muda stahili.Kuna wale jamaa zako walioamua kujiari lakini wanaandamwa na polisi na kubambikiwa kesi za bangi,uzururaji,nk kila wanaposhindwa kutoa rushwa kwa askari au mgambo.

Wafikirie hawa wakati unapiga kura.Weka kando mafanikio yako binafsi.

Na kwa wale wanaoteseka kwa vile watawala wamekuwa bize zaidi na kuongeza idadi ya magari yao ya kifahari,kuongeza idadi ya mahekalu yao,kuongeza idadi ya nyumba ndogo zao,na matumizi mengine ya anasa kama hayo,huu ndio wakati wenu wa kulipa kisasi.Kama mlibebwa kwa malori kwenda kwenye mkutano wa Kikwete au mgombea mwingine wa CCM,well,hakuwaomba bali walijipendekeza wenyewe.Hivi hamsangai ukarimu huu wa ghafla umetoka wapi?Hamjiulizi kuwa wakati mnahangaika kupeleka wagonjwa na akina mama wajawazito hospitalini kwa vile hakuna magari ya vimulimuli wao walikuwa wantembelea magari ya thamani huku wakiwatimulia vumbi,lakini ghafla leo wanawabeba kwenye malori mkawasikilize.MSIDANGANYIKE.Mkishawapa kura,hamtawaona tena mpaka mwaka 2015.

Japo nimesema kuwa uchaguzi huu una umuhimu wa kipekee,lakini ni muhimu kukumbuka kuwa tulikuwa na chaguzi kama hizi huko nyuma,na wa karibu zaidi ni wa mwaka 2005.Hivi hamkupata matumaini Kikwete alipoahidi maisha bora kwa kila mmoja wenu.Je mmeshayaona maisha hayo bora?Kama bado,kwanini mnataka kumwamwini tena safari hii japo amekaa madarakani miaka mitano na ameshindwa kutimiza ahadi aliyoweka mwenyewe bila kushikiwa mtutu wa bunduki (hakulazimishwa)?

Na yule mbunge aliyeahidi miujiza lakini akaishia kuongeza kitambi chake na idadi ya watoto kupitia hawara zake,kwanini umpe tena kura?Unataka aendelee kukusanifu?Maana ulifanya makosa mwaka 2005 ukiamini kuwa ahadi zake zilionyesha anakujali.Lakini miaka hii mitano iliyopita inatosha kukuthibitishia kuwa huyo ni tapeli wa kisiasa,na hakuna tapeli anayeaminika.Lakini sio yeye tu bali hata chama chake.

Hesabu umri wako.Halafu jiulize lini ulianza kuisikia CCM.Kumbuka magapi wameahidi katika miaka yote hiyo uliyokuwa unawafahamu.Linganisha maendeleo yako na hao wenye CCM halisi.Kwanini bado unaendelea kukiamini chama hiki?Kama waliahidi 1995 hawakufanya,lakini wakarejea tena kuahidi mwaka 2000,na hawakufanya.Na bila aibu wakarejea tena mwaka 2005,na safari hii wakiahidi kuwa wanajua matatizo yako na ya familia yako.Wakaahidi pia kuwa maisha yako yatakuwa bora kwa vile hilo linawezekana.Na wakaonyesha namna watakavyowezesha maisha bora kwa kila Mtanzania.Je wametimiza?

Lakini pengine wameshindwa kutimiza kwa sababu za kibinadamu.Sasa kwanini badala ya kukuomba msamaha na kueleza kwanini wameshindwa kukuletea maisha bora,wanakufanya mjinga kwa kukuahidi yaleyale waliyoahidi mwaka 2005 na kutoyatekeleza?Kumbuka: ukiwachagua tena hutokuwa na sababu ya kuwalaumu kwani wameshakuthibitishia kwa miaka kadhaa kuwa hawawezi kukusaidia lakini ukaendelea kuwaamini.Sasa,japo inakera kuona unaendela kuwaamini matapeli hawa,ni muhimu kukumbushana pale tunapokosea.Kufanya kosa si kosa bali kurejea kosa.Na umesharejea makosa hayo mara kadhaa.Sasa umefika wakati wa kusema IMETOSHA.

Nimalizie kwa kukumbusha kuwa katika uchaguzi huu tumebahatika kumpata Nyerere wa pili.Huyu ni Dokta Wilbroad Slaa.Kama ambavyo Nyerere alijitoa mhanga kuhakikisha mkoloni anaondoka,Dokta Slaa amethibitisha kuwa ni mzalendo mwadilifu ambaye ameamua kupambana na mafisadi hadi watokomee.Kama aliweza kuwakalia kooni mafisadi alipokuwa mbunge tu,jiulize atakayofanya atapokabidhiwa urais.Wakati akiwa mbunge silaha yake pekee ilikuwa ni maneno,lakini tukimkabidhi dola atakuwa na nyenzo mbalimbali za kuipeleka nchi yetu inapostahili kwenda.

Usihadaishwe na wasiwasi kuhusu wizi wa kura.Kuiba wataiba lakini ili waweze kuiba za kutosha kuwabakiza mafisadi madarakani itategemea zaidi idadi ya kura tutakazompa Dokta Slaa.Ni rahisi kuiba kura chache lakini ni vigumu kuiba maelfu au mamilioni ya kura.Wingi wa kura kwa Dokta Slaa utakuwa silaha muhimu ya kuwatia aibu mafisadi katika kujaribu kuchakachua kura au matokeo ya uchaguzi huo.

INAWEZEKANA.TIMIZA WAJIBU WAKO

Friday, 22 October 2010



Makala yangu katika jarida la Raia Mwema toleo la wiki iliyopita ililenga kuchokoza mjadala kuhusu "mashushushu".Nilijaribu kutengeneza mazingira ya kumwezesha msomaji kuhitimisha iwapo madai ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa,kuwa Serikali ya Rais Jakaya Kikwete imesambaza Maafisa Usalam wa Taifa nchi nzima ili wamsaidie Kikwete kurejea Ikulu (wachakachue kura).Katika toleo la wiki hii la jarida hilo,jamaa mmoja anayejiita Almas Kajia ametoa majibu kwa niaba ya Idara yab Usalama wa Taifa.Nasema "anayejiita" kwa vile ameshindwa japo kuweka barua pepe yake au namba ya simu just in case ningehitaji kumjibu one to one.

Anyway,naomba nichapishe makala yake nzima,japo unaweza pia kuisoma katika jarida la Raia Mwema.

Kazi ya mashushushu ni usalama si kuhujumu uchaguzi
Almasi Kajia
Oktoba 20, 2010
RAIA Mwema namba 155 la Oktoba 13-19, 2010 liliandika makala iliyokuwa ikiuliza kama mashushu hutumiwa kuhujumu uchaguzi.
Makala hiyo iliyochapishwa katika safu hii ya Raia Mwema Ughaibuni ya Evarist Chahali anayeishi Uskochi, ilikuwa na kichwa kidogo cha habari “Dk. Slaa aibua madai fikirishi”.
Mashushu ambao mwandishi anaulizia kama wanaweza kutumiwa kuhujumu uchaguzi ni maafisa Usalama wa Taifa wa Tanzania na uchaguzi anaozungumzia ni Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010.
Katika makala yake, mwandishi ameanza kwa kujisifu kwamba ana ufahamu wa kutosha juu ya Usalama wa Taifa au intelijensia, ameisomea fani ya Usalama wa Kimataifa na kwamba anaijua vizuri Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania.
Pamoja na sifa, tambo na majigambo yote haya, mwandishi anasema anachojaribu kuandika hakisemeki au hakizungumziki na anasema kwa kutekeleza kile anachotaka kukifanya lazima tujiulize maswali magumu na pengine ya kuogofya.
Napenda niseme kwamba kuanzia mwanzo kabisa katika kupitia makala yote ya mwandishi huyu hakuna chochote alichoandika ambacho hakizungumziki na hakuna swali lolote gumu wala la kuogofya ambalo amelidhihirisha katika makala yake.
Nilichogundua katika makala yake ni kuwa kama huo si mtindo wake wa kuwavutia wasomaji napenda kuamini kwamba yeye ni mshika bango wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) na ameendeleza tu yale yanayofanywa na chama hicho yasiyofurahisha kila mtu, ni mambo yanayorandana na afanyayo Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe na mgombea urais kupitia chama hicho, Dk. Willibrod Slaa.
Hata hivyo, ameeleza mambo ya msingi sana katika kuthibitisha kwamba amejifunza fani ya usalama wa kimataifa kwa kusema kwamba uimara wa taifa lolote duniani unategemea uimara wa idara yake ya usalama wa taifa na kulegalega kwa mambo katika nchi yoyote duniani kunaashiria upungufu wa idara hiyo.
Lakini katika hali ambayo sikutarajia, mwandishi anakiri kwamba kwa miaka mingi sasa, Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania ni miongoni mwa idara bora duniani. Hilo pengine lilitokana na maelezo yake kwamba anaifahamu vya kutosha Idara hiyo.
Wapo waandishi wengine ambao wamekuwa wakiandika habari kama hizo, lakini wakiwa na mitazamo inayotofautiana. Jambo ambalo linanishangaza au pengine linanitia shaka katika makala yake ni kama Idara anayoisifu hivyo imekwishakupoteza sifa hizo na kama ni hivyo je, hiyo ndiyo sababu ya yeye kuanza kuwa na shaka kama Idara hiyo sasa inaweza kutumika kuhujumu matokeo ya uchaguzi?
Amesema idara ya usalama wa taifa duniani kote hufanya kazi kwa siri kubwa kabisa na usiri huo ni sehemu ya utekelezaji wa kazi zake. Anasema usiri ni muhimu kabisa na wa lazima katika ukusanyaji wa taarifa nyeti.
Jambo ambalo wasomaji walitakiwa walijue kutoka kwa mwandishi ni ikiwa usiri wa Idara ya Usalama wa Taifa ndio utakaotumika kuhujumu matokeo ya uchaguzi na kama hilo ndio lengo ni kwa nini Idara hiyo ifanye hivyo, kwa kutumiwa na CCM au kwa utashi wake yenyewe?
Mwandishi amezitaja nchi za Uingereza na Marekani kama mifano kwamba mara chache wakuu wa vyombo vya intelijensia huitwa kutoa ufafanuzi kwa mambo yanayohusu usalama wa Taifa wa nchi hizo.
Kwamba aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Central Intelligence Agency (CIA) ya Marekani, George Tennet aliitwa kueleza juu ya ushahidi kwamba Iraki ilikuwa na mipango ya kutengeneza silaha za maangamizi.
Anasema katika nchi hizo mbali na kuondoa katika orodha baadhi ya mambo ambayo ni siri, mabunge yao yana kamati zinazoshughulikia masuala ya usalama na zinawaita viongozi wa idara hizo kutoa ufafanuzi katika masuala yanayohusu intelijensia pale inapokuwa lazima kufanya hivyo.
Suala hili halifanyiki kwa siri anayoizungumzia mwandishi na kama nia yake ingekuwa ni kulifahamu hilo angemuuliza Dk. Slaa ambaye amekuwa mbunge kwa miaka 15 na anafahamu kwamba ipo Kamati ya Bunge ambayo inafanya kazi kama zile zinazofanywa na mabunge ya Uingereza na Marekani.
Amerejea swali lake kama Idara ya Usalama wa Taifa inaweza kutumiwa na CCM kuhujumu uchaguzi na akaunganisha masuala mengine mawili kwamba; hakuna ofisa usalama atakayefurahi na tuhuma za Slaa zikibainika kama ni uongo na Watanzania watakuwa na hofu kama itabainika kwamba tuhuma hizo ni za kweli.
Swali kwamba Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa wapi wakati ukitokea ujambazi wa EPA na je, Idara hiyo ilikuwa ikifanya nini wakati mikataba ya kifisadi ikitokea. Mwandishi anajihami mapema kwa kusema kwamba maswali haya yatazua uhasama kati yake na idara hiyo.
Labda niseme tu kwamba si maofisa wa Idara ya Usalama tu watakaochukia bali Watanzania hawatafurahi kuona tuhuma hizi za Dk. Slaa ambazo ni za uongo zinazidi kuendelezwa na watu wenye hadhi za kisomi kama mwandishi mwenyewe kwa ahadi ambazo nina hakika hazitatimia.
Wananchi wa kawaida ambao wamekwishakuelewa kwamba Chadema ina tabia ya kuzua mambo na ambao wanaamini kwamba nchi hii ina ulinzi wa kutosha, hawawezi kuingiwa na hofu kwa kutegemea tu propaganda za askari wetu kutoka Uskochi.
Ninachotarajia mimi ni kwamba Idara ya Usalama wa Taifa haitamjibu mwandishi. Nililo na uhakika nalo ni kwamba itanyamaza bila kusema chochote kwa kuwa mwandishi mwenyewe amesema kuwa Idara hiyo inafanya kazi zake kwa siri kubwa kabisa.
Ninahisi kwamba mara zote Idara hii inaacha wajinga wajielimishe wenyewe. Swali kwamba Idara ya Usalama wa Taifa ilikuwa wapi wakati ufisadi wa EPA ukitokea sio la msingi bali jambo la muhimu ambalo Mtanzania wa kawaida anaweza kusema ni kwamba suala la EPA limeshughulikiwa sana na Serikali na baadhi ya wahusika wamefikishwa mahakamani.
Naamini kwamba ufisadi si sera ya Serikali wala ya Chama tawala-CCM- na ni vyema ikubalike kwamba, kwa sasa pengine tofauti na ilivyokuwa huko nyuma, ufisadi ni suala la mtizamo na hulka ya mtu kuliko kuonekana kama mtindo wa maisha wa baadhi ya Watanzania.
Serikali ya Tanzania inazingatia utawala wa sheria na tungejali sana suala la mtu kumiliki vitu kama gari, nyumba nzuri, vitu ambavyo wengine hawana, mtu huyu akaonekana kuwa fisadi, Watanzania wengi wangeishia jela.
Amezungumza mengi ikiwa ni pamoja na ikiwa Msajili wa Vyama vya Siasa ambaye shughuli zake si za siri anaonyesha wazi kuipendelea CCM kwa kuingilia majukumu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi, hali ikoje katika Idara ya Usalama wa Taifa.
Nilijaribu kuhoji pale mwanzo kama mwandishi alikuwa anahisi nini juu ya usiri aliousifia sana, usiri wa Idara ya Usalama wa Taifa, kama usiri huo ndio utatumika kuhujumu matokeo ya uchaguzi.
Kinachojidhihirisha hapa ni kwamba mwandishi anataka Watanzania waamini kwamba Idara ya Usalama wa Taifa kwa kutumia kigezo cha usiri, inaingilia Tume ya Taifa ya Uchaguzi kama alivyofanya Msajili wa Vyama vya siasa kwa nia ya kuhujumu matokeo ya uchaguzi (kama kweli alifanya hivyo).
Inaonekana anaamini kwamba usiri huu ndiyo utakaotumika kukipatia ushindi CCM kwa kuihujumu Chadema.
Lakini kila mtu anajua kwamba kazi ya Idara hiyo kama chombo cha usalama ni kuhakikisha Usalama wa Taifa ambao ni pamoja na uchaguzi kuendeshwa kwa amani, si kuuhujumu.
Inavyoonekana, mwandishi mara zote anaiangalia Idara ya Usalama wa Taifa kama chombo chenye uamuzi wa mwisho kwa kila kitu na anasema kwamba Idara hiyo inamfahamu mmiliki wa Kagoda, ama kwa njia zisizo rasmi au njia rasmi.
Hivi kama kweli kazi za Idara hiyo ni za siri ni vipi itathubutu kutekeleza au hata kama imetekeleza, ieleze wazi kwamba imefanya hivi na hivi kwa watuhumiwa wa aina yoyote, achilia mbali wa Kagoda.
Binafsi nina shaka juu ya uelewa wake wa usalama wa kimataifa na ufahamu wake juu ya Idara hii ambayo anadai ni moja ya idara bora duniani na inayotenda kazi zake kwa usiri.
Ni utaalamu gani anaozungumzia mwandishi unaoweza kutumika kushinikiza Serikali kwa njia zilizo rasmi na zisizo rasmi. Nimejaribu kudadisi kwa wajuzi wa masuala ya Usalama wa Taifa, nikaambiwa kwamba kazi ya idara hiyo duniani kote ni kutoa ushauri na si kushinikiza kama mwandishi anavyotaka tuamini.
Nilitaka kujua kama ameifahamu Idara hiyo vipi kwa kuhadithiwa au pengine alishawahi kuwa mtumishi kwenye chombo hicho nyeti? Kwa yote mawili nilipata jibu moja kwamba hata kama alihadithiwa au alifanya kwenye Idara hiyo, kulingana na kanuni za usiri ambao ameukiri yeye mwenyewe, hawezi kusimama hadharani na kusema kwamba amekuwa mtumishi wa chombo hicho.
Anasema pia kwamba idara ya usalama wa taifa kote duniani ni kama nusu jeshi (paramilitary) na viongozi wake wanaogopwa kupindukia na uamuzi wao hauhojiwi.
Katika udadisi wangu, niliambiwa mambo mawili kwamba kuogopwa kupindukia kunatokana na usiri wa idara zenyewe na nikaamini kwamba usichokijua ni sawa na usiku wa giza.
Kwamba wanaoiogopa idara ni wasioifahamu na anachotaka kusema mwandishi ni kwamba wasomaji waendelee kuiogopa Idara yao ya Usalama wa Taifa.
Nafikiri hilo si la lazima kwa sababu wananchi wana haki ya kukifahamu chombo ambacho kwanza kinahakikisha kuwa Taifa ni salama na kinatumia kodi za wananchi katika utendaji wake wa kazi wa kila siku. Hakuna sababu ya kukiogopa, ni chombo chao na ambacho kimewekwa kisheria.
Mwandishi ametaka pia wasomaji wake wapime madai fikirishi ya Dk. Slaa ambayo yametolewa kama tuhuma ikiwa hadithi au ni kitu kinachowezekana. Ukiyavulia nguo maji sharti uyakoge na kwa hilo mwandishi haamini kwamba anachosema Dk. Slaa ni hadithi tu, anaamini kwamba ni ukweli ingawa hoja yake imejengwa katika nadharia tu.

Ukisoma kwa makini utagundua kuwa Bwana Almasi Kajia (tukiamini kuwa hilo ndilo jina lake halisi) ameelemea zaidi kwenye kujadili wasifu wangu kama mwandishi badala ya kujibu maswali muhimu niliyotoa katika makala ya mwanzo.Lakini kwa vile sipendi malumbano,naweza kufupisha kwa kuhitimisha kuwa makala yake imeshindwa kuthibitisha kuwa HAIWEZEKANI IDARA YA USALAMA WA TAIFA KUTUMIWA NA SERIKALI YA KIKWETE KUCHAKACHUA KURA.Yah,anaweza kusema madai ya Dokta Slaa ni nadharia kwa vile hata fedha za EPA zilipoibiwa tuliambiwa kuwa huo ni uzushi tu (na wahusika wakatishia kumfikisha Dokta Slaa mahakamani).

Haihitaji taaluma ya usalama japo wa mgambo kutambua kuwa fedha za EPA ziliibiwa wakati taasisi zenye jukumu la kuzuwia zikiwa kazini.Mkataba wa kitapeli wa Richmond ulisainiwa wakati wenye jukumu la kuuzuwia wanakenua meno tu.Same story kuhusu Kiwira,IPTL,Buzwagi,Meremeta,Tangold na skandali nyingine za ufisadi.

Wakati naandaa makala hiyo sikutegemea pongezi kutoka kwa wahusika.Nafahamu kuwa hawapendi kukosolewa sio kwa vile wako sahihi bali wanatambua kuwa aina yoyote ile ya ukosoaji inawafumbua macho kuonyesha udhaifu na mapungufu yao.Na hawataki hilo lijulikane kwa vile linaweza kupelekea Nguvu ya Umma kudai majibu kwa nguvu.

Mafisadi wangependa sana kuona kila Mtanzania akiwa mbumbumbu.Wanasali kwa bidii kusijitokeza wahaini wa kuhoji maswali magumu.Si mmesikia tishio kwa gazeti la Mwananchi kwa vile tu haliandiki kile watawala wamezowea kusikia?Wameleweshwa na sifa kiasi kwamba ukiwakosoa ni sawa na kuwatukana.

Finally,naomba kuthibitisha kuwa nilipoandika kuwa naifahamu taasisi hiyo vizuri nilikuwa na sababu zangu za msingi.Sihitaji kufafanua kwa vile hayo ni mambo binafsi.Lakini they and I know very well kuwa hilo la kuifahamu vyema halina ubishi.Mambo mengine hayawezi kuzungumzwa hadharani.

Nilichofarijika ni kile alichowahi kutamka Rais wa zamani wa Marekani,George W.Bush kwamba "ukisema au kufanya jambo flani,kisha watu waka-react basi ujue ulichoongea kimewagusa" maana laiti ingekuwa upumbavu au uzushi tu,Bwana Almasi asingepoteza  muda wake kunijibu.

AJIKUNAYE UJUE KAWASHWA


Kama ilivyo ada,toleo la wiki hii la jarida la Raia Mwema limesheheni habari moto moto na makala zilizokwenda shule.

Makala yangu katika toleo hili inazungumzia kuhusu Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Jumapili wiki ijayo.Nimejaribu kujenga hoja kwanini miaka mingine mitano kwa Jakaya Kikwete ni hatari kwa ustawi wa taifa letu.

Nisikupunje uhondo bali bingirika na makala hiyo kwa KUOBONYEZA HAPA.

Thursday, 21 October 2010


Mke wa Balozi

Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe

Kushoto kwenda Kulia: Mariam Kilumanga (Mwenyekiti wa TAWA), Mama Balozi Joyce Kallaghe na Mariam Mungula (Katibu wa TAWA)























Picha zimeletwa na Miss Jestina

Wednesday, 20 October 2010



Serikali sasa yatishia kulifuta Mwananchi
Wednesday, 20 October 2010 07:52

Mwandishi Wetu
SERIKALI imetishia kulifunga au kulifutia usajili gazeti la Mwananchi kwa madai kwamba linaandika habari za uchochezi dhidi ya serikali ya awamu ya nne.Barua ya serikali yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/76 iliyoandikwa kwa mhariri mtendaji wa gazeti la Mwananchi, inaonya kwamba kama gazeti hili litaendelea kuandika habari ambazo imeziita za uchochezi dhidi yake, haitasita kuchukua hatua stahiki kwa mujibu wa sheria za nchi.

Hata hivyo, barua hiyo haijaweka bayana habari hizo ilizozielezea kuwa ni za mtazamo hasi dhidi ya serikali na ambazo imedai kuwa ni za uchochezi.

“Kwa barua hii unatakiwa kuacha mara moja tabia ya kuandika habari za uchochezi na kuidhalilisha nchi na serikali kwa kisingizio cha uhuru wa habari na uhuru wa kutoa mawazo ulioanishwa katika katiba ya nchi yetu," inaeleza barua hiyo ya Oktoba 11 iliyosainiwa na Raphael Hokororo kwa niaba ya Msajili wa Magazeti.

"Aidha ukiendeleza tabia hiyo, serikali haitasita kuchukua hatua stahiki za kulifungia gazeti lako au kulifutia usajili kwa mujibu wa sheria za nchi.”

Barua hiyo, ambayo imebeba kichwa cha habari kisemacho "Karipio kali kwa kuandika habari zenye mwelekeo wa uchochezi wa kudhalilisha", ni mwendelezo wa barua nyingine iliyoandikwa na mkurugenzi wa Idara ya Habari, Clement Mshana kwenda kwa mhariri wa gazeti hili Septemba 24, 2010.

Katika barua hiyo ya Mshana, serikali imedai kuwa gazeti la Mwananchi limekuwa na mtazamo hasi dhidi ya serikali na ikamtaka mhariri ajieleze.

Barua hiyo yenye kumbukumbu namba ISC/N.100/1/VOL.V/70, bila ya kutoa mifano, inadai kuwa Mwananchi imekuwa ikiandika habari hasi tu kana kwamba serikali haina zuri linalofanywa kwa wananchi wake na kutaka maelezo.

“Katika kipindi kirefu sasa, na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Habari hizo zimekuwa zikidhalilisha serikali iliyo madarakani ya awamu nne,” inasema sehemu ya barua hiyo.

Katika majibu ya barua hiyo ya kwanza, Mwananchi Communications Ltd (MCL), ilieleza kuwa baada ya kutafakari kwa kina ilishindwa kuelewa msingi wa tuhuma hizo ambazo hazina mifano yoyote ya habari inayodaiwa kuwa ni hasi kwa serikali.

“Baada ya kupitia barua yako na kuitafakari, imetuwia vigumu kuelewa msingi wa tuhuma zako kwa gazeti hili kuhusu mtazamo hasi dhidi ya serikali bila hata kutoa mifano ya habari ambazo zinabeba tuhuma zako kwa gazeti hili hasa unaposema kuwa kwa kipindi kirefu sasa, hasa wakati huu wa kampeni za uchaguzi,” inasema barua hiyo yenye kumbukumbu namba MCL/RN/09/VOL.1.27 iliyoandikwa na mhariri mtendaji wa MCL, Theophil Makunga.

Barua hiyo ya MCL inaeleza kuwa kimsingi habari za kampeni za uchaguzi katika kipindi hiki zinahusu vyama vya siasa na kuhoji sababu za serikali kujiona inaandikwa vibaya na Mwananchi wakati ni vyama ndivyo vinavyoshiriki kwenye kampeni.

Mhariri wa Mwananchi anaeleza katika barua hiyo kuwa kwa sasa gazeti lake linaandika habari za wagombea uongozi kutoka vyama mbalimbali na sera zao ili wananchi wafanye uamuzi siku ya kupiga kura na hakuna chama kilichoandika barua ya malalamiko.

“Kwa taarifa yako tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi Agosti 21, 2010, gazeti la Mwananchi halijawahi kupata malalamiko kutoka chama chochote cha siasa kinachoshiriki katika kampeni hizo juu ya kuandikwa vibaya. Kimsingi Mwananchi linachofanya ni kuripoti wanachosema wagombea wa vyama mbalimbali au kufanyiwa katika mikutano ya kampeni,” inasema barua hiyo ya MCL kwenda kwa Msajili wa Magazeti.

Katika barua hiyo, MCL inaiomba serikali kutoa ufafanuzi zaidi kuhusu kuhusika kwa serikali katika kampeni za uchaguzi hadi gazeti hili lionekane lina mtazamo hasi.

“Kwa msingi huo, tunaomba ufafanuzi zaidi hapa; serikali inahusika vipi katika kampeni mpaka Mwananchi ionekane ina mtazamo hasi kwa serikali wakati vinavyoshiriki katika kampeni ni vyama vya siasa na wagombea wake,” inasema barua hiyo.

Baada ya barua hiyo, Msajili wa Magazeti alijibu kwamba majibu yaliyotolewa na MCL hayaridhishi na hivyo ofisi yake haikuridhika na utetezi huo.

“Kama tulivyoeleza kwenye barua yetu kwako kuwa katika kipindi kirefu sasa na zaidi wakati huu wa kampeni za uchaguzi, gazeti lako limekuwa likiandika habari zenye mtazamo hasi dhidi ya serikali. Gazeti lako sasa limeamua kufanya ‘house style’ yake ya kuandika habari zenye uchochezi na kudhalilisha nchi na serikali iliyopo madarakani,” inasema barua hiyo.

Katika onyo lake, serikali inasema kwamba picha, habari zinazopewa kipaumbele katika ukurasa wa kwanza wa gazeti zinatiwa chumvi kwa lengo la kuchochea wananchi waione serikali yao haijafanya chochote kwa maendeleo yao.

Akiongelea hatua hiyo ya serikali, Makunga alisema kwamba MCL imeshtushwa na karipio hilo ambalo halikuonyesha ni habari ipi ambayo gazeti la Mwananchi limekosea.

“Msajili hakunukuu hata sheria moja ya vyombo vya habari kuonyesha jinsi gani gazeti limekosea wala habari au kichwa cha habari chenye mtazamo hasi kwa serikali,” alisema Makunga.

Alisema Mwananchi imechukulia hatua hiyo ya msajili kuwa inatishia uhuru wa vyombo vya habari hasa katika kipindi hiki cha kampeni za uchaguzi ambacho kinahitaji uvumulivu baina ya taasisi mbalimbali katika jamii.

Makunga alisema kwa kuwa Mwananchi na msajili inaonekana kutokubaliana katika suala hilo, wameamua kupeleka taarifa Baraza la Habari Tanzania (MCT) liweze kufanya uchunguzi kwa mujibu wa katiba yao.

Alisema msimamo wa sera ya uhariri ya MCL inasimamia kwenye ukweli na weledi pasipo kushurutishwa na vikundi vyovyote vya nje na ndani.Makunga alisema Mwananchi itaendelea kuandika habari za ukweli bila ya kumuonea mtu au taasisi yoyote kwa maslahi ya Tanzania.

CHANZO: Mwananchi


Baadhi ya wazazi wa watoto wanaugua ungonjwa wa malaria wakiwa nje ya Kituo cha Afya Nyamongo Wilayani Tarime

Anthony Mayunga, Tarime

KITUO cha Afya Nyamongo wilayani Tarime hakijapata dawa ya mseto inayotibu malaria kwa kipindi cha miezi mitatu hadi sasa.

Tatizo hilo linakwenda kinyume na kampeni za kupambana na malaria kwa kuwatibu wagonjwa ambayo inasisitiza kwamba Watanzania watapata vyandarua na dawa sahihi za kutibu malaria.

Uchunguzi wa uliofanywa na Mwananchi katika kituo hicho kilichoko katikati ya eneo la mgodi wa dhahabu wa North Mara ,ulibaini ukubwa wa tatizo hilo na wananchi kuonyesha kukata tamaa juu ya
mikakati inayonadiwa na viongozi kutokomeza malaria nchini. Marwa Ryoba mkazi wa Nyangoto alisema wanalazimika kutumia dawa za krolokwini,metakefilini na SP ambazo zilikwishapigwa marufuku na serikali kwa kushindwa kutibu ugonjwa huo.

“Tunashangaa ahadi na tambo nyingi za serikali kuwa watatokomeza malaria wakati hatupati dawa , hivi kupewa vyandarua na Wamarekani bila dawa inatusaidia?”alihoji kwa uchungu.

Mganga mfawidhi wa kituo hicho Dk George Marwa alikiri kuwa hawajapata
dawa mseto licha ya kutoa taarifa kwa zaidi ya miezi mitatu. “Hapa tunapambana na matatizo makubwa maana jamii haijui tatizo la Msd badala yake lawama zinaelekezwa kwetu,maana kama hakuna Alu unadhani huko wanatumia nini,”alisema. Kuhusu kadi za kiliniki hakuna na wajawazito na wenye watoto
wanalazimika kununua mitaani inadaiwa wananunua Sh2,000= maana hatuna,na hilo linawakatisha tamaa wasiokuwa na fedha kuhudhuria
kiliniki.
“Hapa tunahudumia zaidi ya watu laki moja kutoka kata zaidi ya nne za Tarime na Serengeti, glovu unapewa pc 50 kwa miezi mitatu ,wakati hizo ni kwa wiki moja,wanalazimika kununua, na ni tatizo la mfumo.

Awali mwanamke aliyekutwa katika kituo hicho akisubiri huduma jina tunao ,alisema kuwa wanachofanya ni kwenda kuandikiwa tu kisha wanakwenda kununua dawa kwenye maduka ya watu ambao pia si wataalam.
“Wengi tunatumia panadol wakati unaumwa malaria na hata kwa watoto
,matokeo yake panapotokea vifo inakuwa vigumu kujua nini tatizo ,maana wapo wanaoishiwa damu, lakini tunashindwa watibiwe na nini,”alisema.

Alikwenda mbali na kudai kuwa matatizo ya wananchi kwa huduma za afya yamegeuka kuwa mtaji kwa wanasiasa wanafiki,kwa kutoa ahadi ambazo hazitekelezeki,”suala la dawa limeshindikana sasa wanadai malaria
itakuwa historia kwa kuua ama nini?”alihoji kwa masikitiko.Baadhi ya wajawazito na wenye watoto waliokuwa hapo kituo
cha afya walisema mbali na dawa ya malaria pia wanalazimika kununua kadi na glovu kwa kuwa hazipatikani hapo kituoni .

“Pembeni wanasema huduma kwa wajawazito na watoto chini ya miaka mitano bure ,lakini hapa tunanunua dawa,mipira ya mikononi(Gloves)na kadi za kiliniki,wengi wanajifungulia majumbani na hawaleti watoto
kiliniki akiugua malaria wananunua panadol na dawa za kienyeji,”walisema.

CHANZO: Mwananchi

NAAMINI TATIZO LA KUDAIWA MALIPO KWA HUDUMA ZINAZOPASWA KUTOLEWA BURE NI KARIBU KILA MAHALI NCHINI.NDIO MAANA CCM HAWATAKI KUSIKIA AHADI YA CHADEMA KUHUSU  ELIMU BURE.

Sunday, 17 October 2010

Moja ya mambo yaliyokuwa yakiwaumiza vichwa wafuasi wa Barack Obama wakati wa kinyang'anyiro kati yake na Hillary Clinton kupata mgombea urais wa Marekani kwa tiketi ya chama cha Democrats mwaka 2008 ni theory inayofahamika kama Bradley Effect.Kwa kifupi kabisa,Bradley Effect (au Wilder Effect) ni hali inayoweza kutokea kwenye kura za maoni katika chaguzi nchini Marekani panapokuwa na mgombea Mweupe (White) na asiye mweupe (non-White).Pengine ili wasionekane wabaguzi wa rangi,wahojiwa Weupe katika kura za maoni hueleza kuwa chaguo lao ni mgombea asiye Mweupe au husema kuwa hawajafanya uamuzi kuhusu chaguo lao (Undecided).

Kwahiyo,matokeo ya kura ya maoni yanaweza kuonyesha mgombea asiye Mweupe anapendwa zaidi kuliko mgombea Mweupe lakini inapofika kwenye hatua ya kupiga kura (ambapo mpiga kura anakuwa peke yake),wapiga kura Weupe wanampigia Mweupe mwenzao.

Asili ya Bradley Effect ni katika kinyang'anyiro cha uchaguzi wa uchaguzi wa gavana wa jimbo la California mwaka 1982 ambapo licha ya mgombea Mweusi,Meya wa Jiji la Los Angeles Tom Bradley kuongoza kura za maoni,aliishia kushindwa uchaguzi huo kwa mgombea Mweupe George Deukmejian.

Baadhi ya wachambuzi wa chaguzi nchini Marekani wanaamini pia kuwa Bradley Effect ilijitokeza tena kwenye mchakato wa kumpata mgombea wa chama cha Democrats kwenye jimbo la New Hampshire ambapo licha ya Obama kuongoza katika kura za maoni,Hillary Clinton aliibuka mshindi kwenye jimbo hilo (japokuwa baadaye Obama alifanikiwa kuibuka mshindi wa jumla,na kupitishwa kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Democrats,na hatimaye kushinda nafasi ya urais).

Katika post hii najaribu kubashiri (hypothesize) namna Bradley Effect inavyoweza kuwa sababu ya mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,kuongoza katika tafiti za  taasisi za Redet na Synovate kuhusu nafasi za wagombea urais katika uchaguzi mkuu wa Tanzania hapo Oktoba 31.Hapa ntawazungumzia wagombea wawili tu,Kikwete na mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.

Japo Bradley Effect 'halisi' inahusu mgombea Mweupe na asiye Mweupe,sababu inayopelekea matokeo ya kura kutorandana na mwelekeo wa kura za maoni inaweza kutumika kuelezea kwanini kura za maoni za Redet na Synovate zilimpa Kikwete ushindi na sio Dokta Slaa.Kama ilivyo kwenye chambuzi mbalimbali,kuna mambo flani inabidi 'kupuuzwa' ili kufikia matokeo yanayokusudiwa.Katika uchambuzi huu,naomba 'nipuuze' urafiki kati ya taasisi hizo na CCM na badala yake nikazanie kwenye uwezekano wa Bradley Effect pekee.

Inawezekana kabisa kuwa wahojiwa kwenye tafiti za Redet na Synovate ni wananchi waliotoa majibu 'kuwaridhisha watafiti',yaani walisema wanampenda zaidi Kikwete kuliko Dokta Slaa.Moja ya sababu za kutoa majibu ya aina hiyo ni mazingira halisi ya Tanzania ambapo licha ya 'siasa za mkono wa chuma' za zama za chama kimoja kuonekana kama historia,ukweli unabaki kuwa baadhi ya wananchi wanaamini kuwa kusema lolote lisilowapendeza watawala ni kujitafutia matatizo.

Naomba kufafanua kidogo katika hilo.Nilipokwenda Tanzania mwaka 2005 kufanya fieldwork ya utafiti wangu wa shahada ya uzamifu (PhD) nilikumbana na wakati mgumu kuwahoji baadhi ya maustaadh (mada yangu inahusu masuala ya Waislam na Uislam nchini Tanzania) kwa vile baadhi yao walidhani mie ni wakala wa serikali niliyetumwa kuwachunguza ili 'serikali iweze kuwadhibiti zaidi'.Bahati mbaya,fieldwork hiyo ilifanyika wakati jeshi la polisi lilikuwa linamsaka mwanaharakati wa Kiislam,Sheikh Issa Ponda.Ilichukua kitambo kujenga uaminifu kati yangu na maustaadh hao.

Kuna wanaoilaumu Redet na Synovate kuhusu aina ya watu waliohojiwa wakidai kuwa huenda wahojiwa walikuwa watu walio karibu na CCM (kwa mfano mabalozi wa nyumba kumi).Uwezekano wa Bradley Effect  'yetu' (yaani isiyohusiana na ishu za ubaguzi wa rangi) ni mkubwa kwa vile wahojiwa wanaweza kutoa majibu yasiyoonyesha 'wanambagua mgombea wao' na hivyo kusema huyo ndio chaguo lao japo mioyoni wana dhamira na/au chaguo tofauti.

Of course,inawezekana tafiti hizo za Redet na Synovate 'zilipikwa' ili kuendana na matakwa ya CCM.Inawezekana pia kuwa aina ya watu waliohojiwa ni ambayo isingetoa majibu tofauti na 'ushindi kwa Kikwete'.Lakini,kama makala hii inavyojaribu kubashiri,inawezekana kabisa kuwa wahojiwa 'waliwazuga' jamaa wa Redet na Synivate 'ili isiwe shida'.Nani yuko tayari kuona genge lake au kibanda cha biashara kinabomolewa kwa vile tu amechoshwa na namna CCM inavyozidi kuahidi maisha bora lakini wanaonufaika ni mafisadi pekee?Mtu wa aina hii haoni shida 'kudanganya leo' kisha 'akaungama siku ya kupiga kura' kwa 'kumwadhibu Kikwete na CCM kwenye sanduku la kura ambapo hakutokuwa na wa kumtoa mimacho kwanini hajampigia kura Kikwete au CCM'.

Huu ni ubashiri tu.Unaweza kuwa sio sahihi lakini kama zilivyo bashiri nyingine-hususan zinazoambatana na mifano hai-unaweza kuwa na ukweli ndani yake.Kadhalika,Bradley Effect 'yetu' inaweza kutoa matokeo ya kuwashangaza wote wenye imani kuwa CCM na Kikwete watarudia kupata ushindi wa kishindo kama wa mwaka 2005.

Pengine kuna watakaohoji kwanini Bradley Effect 'yetu' haiwezi kutumika kwenye utafiti mwingine (wa TCIB) unaoonyesha kuwa Dokta Slaa anaongoza.Jibu langu ni kwamba watoa maoni hawana cha kupata (nothing to gain) kuwadanganya watafiti kuwa wanampenda Dokta Slaa wakati ukweli wanayempenda ni Kikwete.Likewise,kwenye tafiti za Redet na Synovate,inawezekana baadhi ya wahojiwa walikuwa na cha kupoteza laiti wangesema hawampendi Kikwete (si unajua kuhusu umoja na mshikamano ndani ya chama?).Vilevile,yawezekana wahojiwa hawakuwa na cha kupoteza (nothing to lose) kwa kudanganya kuwa wanampenda Kikwete (kwa minajili ya kuwaridhishwa watafiti na 'kulinda ugali wao') kisha wakamnyima kura katika usiri wa chumba cha kupigia kura.

Mwisho,naomba kusisitiza tena kuwa hypothesis hii imejaribu kupuuza sababu za 'wazi' kama vile upendeleo wa watafiti,uoga wa wahojiwa,na kubwa zaidi,UCHAKACHUAJI.

Saturday, 16 October 2010


Senegal welcomed 163 Haitian university students to Dakar Wednesday. Senegalese president Abdoulaye Wade, offered them free education after an earthquake devastated their island nation in January.

Sanogier Genevieve Julbertha arrived in Senegal Wednesday, less than a year after a catastrophic earthquake in her country killed about 200,000 people and caused widespread structural damage.

The 20-year-old law student is one of the more than 160 Haitians who will enroll in a Senegalese university this fall free of charge.

She says she does not have the words to describe how good it is to be in Senegal. She says we are the same people. We share the same roots. She says life is still difficult for many Haitians. Many universities collapsed, she says, and many families are still homeless.

The Senegalese government was swift to offer aid to Haiti in the earthquake's aftermath this January, committing $1 million in emergency relief as well as offering land to Haitians who wanted to relocate to Senegal.

Senegalese President Abdoulaye Wade addressed the students Wednesday at a ceremony at the foot of his recently-inaugurated Monument to the African Renaissance. He called the students' arrival an act of "panafrican solidarity."

Mr. Wade says today marks the return of young Haitians to the land of their ancestors and a resounding victory for Africa. Others before us have tried, he says, only to return to a land still dominated by outside forces, but these students are returning freely to an independent Africa in control of its destiny.

The students will attend one of three Senegalese universities on full scholarships from the Senegalese government.

Mardoche Fontilus, 20, says he will study psychology in Senegal. The opportunity is a "dream come true," he says, but it cannot erase the memories of this past year.

He says the earthquake impacted the lives of everyone in Haiti, and it was our brothers, sisters, aunts and cousins under the rubble. He says he is grateful for the international aid they have received, but January 12 was a sad day they will never be able to forget.

Fontilus said he hopes the education he receives in Senegal will allow him to return to Haiti and help rebuild his country.

SOURCE: VoA

Friday, 15 October 2010


Na Mwandishi wetu

Shirika lisilo la kiserikali linalojishughulisha na kutoa utafiti wa taarifa mbalimbali kwa lengo la kuwawezesha wananchi maamuzi kwa uelewa la Tanzania Citizens Information Bureau (TCIB) limetoa taarifa ya matokeo ya utafiti wa kura ya maoni kuhusu wagombea urais 2010.

Akizungumza na waadishi wa habari Mhadhiri Chuo Kikuu cha Dar es salaam idara ya Uchumi Dr. Vicent Leyaro amesma malengo ya TCIB ni kutoa msukumo kwa wananchi kushiriki katika harakati za kulinda na kendeleza misingi ya Demokrasia, Kutoa fursa kwa wananchi katika kutoa maoni yao juu ya mambo mbalimbali katika maisha na kujenga uwezo wa wananchi kwa njia ya tafiti na elimu katika nyanja za serikali, siasa, Mambo ya Kimataifa, ulinzi, elimu na maadili.
Kutoka kushoto ni Mhadhini kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Idara ya Uchumi Dr.Vicent Leyaro akizungumza na waandishi wa habari katika Hotel ya Courtyard juu ya utafiti wa (TCIB) akiwa na mwakilishi wa Mkurugenzi wa (TCIB) Bw. Steven Msechu.

Aidha Dr. Vicent Leyaro amesema washiriki katika kura hii ya maoni ni 3047 wenye wasifu wa aina mbalimbali ikiwa ni pamoja na watoto chini ya darasa la saba, elimu ya sekondari na elimu iliyo juu ya sekondari ambapo katika utafiti huo silimia kubwa ya vijana wamonekana kuunga mkono mgombea urais wa CHADEMA Wllbrod Slaa na asilimia kubwa ya wazee wameonyesha kumuunga mkono mgombea urais wa CCM Jakaya Kikwete.

Amesema Dr. Willbod Slaa ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa ya Kilimanjaro 71%, Arusha 60.4%, Manyara79.8%, Iringa58.2% na Dar es salaam 42% ambapo Jakaya Kikwete ameongoza kwa asilimia kubwa katika mikoa Dodoma 59.3%, Morogoro 56%, Mbeya50%, Rukwa 54.3% na Ruvuma 55%.

Akihitimisha wakati akijibu maswali kwaa waandishi wa habari Dr. Vicent Reyaro amesema utafiti haukuangalia wala kupendelea sehemu ambazo mtu anapendwa sana kuliko sehemu nyingine na uchambuzi wa matokea kimkoa yanaonyesha kuwa wagombea wawili Jakaya Kikwete na Dr. Willbrod Slaa wanachuana vikali baadhi ya mikoa na mikoa mingine kufanya vibaya.

Hata hivyo utafiti huu wa kura ya maoni kuhusu wagombea urais hauukufanyika kwa upande wa Zanzibar japokuwa wananchi wa Zanzibar wanashiriki katika kupiga kura ya kuchagua rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Chanzo: Changamoto

Habari kwa hisani ya Jamii Forums


Makala yangu katika toleo la wiki hii la jarida maridhawa la Raia Mwema inazungungumzia madai ya mgombea Urais kwa tiketi ya Chadema,Dkt Wilbroad Slaa,kuwa serikali ya Rais Jakaya Kikwete imesambaza maafisa usalama nchi nzima ili kuhujumu uchaguzi (kumsaidia Kikwete ashinde).Kwa kutumia taaluma na utaalam wa kutosha kuhusu masuala ya intelijensia,makala inajaribu kumpa mwangaza msomaji iwapo Idara yetu ya Usalama wa Taifa inaweza kutumiwa visivyo katika mazingira tuliyonayo sasa.

BONYEZA HAPA KUSOMA MAKALA HIYO Pamoja na habari na makala nyingine zilizokwenda shule katika jarida hili mahiri la Raia Mwema

Thursday, 14 October 2010


Mimi si mwanasheria japo nasaka uhitimu wa kiwango cha kati (katika Sheria) kwa njia ya masafa.Kwahiyo nina uelewa wa wastani kuhusu masuala ya jumla-jumla kuhusiana na taaluma ya Sheria.Na ni katika hilo ndipo nafahamu kuhusu CLASS ACTION.Kwa uelewa wangu wa wastani,Class Action ni aina ya kesi ya madai inayofunguliwa na kundi (mara nyingi kundi kubwa) dhidi ya taasisi au kundi flani.

Kwa mfano,kundi la wavuta sigara linaweza kufungua class action dhidi ya kiwanda cha tumbaku au cha sigara kulingana na madai yao dhidi ya wadaiwa.Aina hii ya kesi ni maarufu zaidi huko Marekani,na sina ufahamu kama imeshawahi kutokea huko nyumbani.

Naamini tuna Watanzania wazalendo katika kila fani.Naamini pia tuna Watanzania wazalendo wenye taaluma ya sheria hususan kesi za madai au kwenye sheria za mawasiliano.Lengo la makala hii ni kuuliza kama wazalendo hao hawawezi kutoa fundisho kwa makampuni mbalimbali ya simu huko nyumbani ambayo yayumkinika kuyatuhumu kuwa yanakiuka haki za usiri (privacy) wa wateja wao.

Kuna hayawani flani amekuwa akisambaza SMS za kumchafua mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa.Haihitaji uchambuzi wa aina yoyote kufahamu uhuni huo wa SMS usingekuwepo laiti Dokta Slaa asingekuwa tishio.

Na japo CCM wamekanusha kuhusika na uhuni huo lakini kama waliweza kuchafuana wenyewe kwenye mchakachuo wa kura za maoni watashindwaje katika mpambano huu wa kufa na kupona hapo Oktoba 31?Unajua tatizo la CCM ya Jakaya Kikwete ukilinganisha na ile ya Mwalimu,Mwinyi au hata Mkapa,ni ombwe kuuuuubwa la uongozi katika chama hicho.Kama ambavyo Kikwete amemudu kutengeneza ombwe la uongozi wa kitaifa akiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano,ndivyo ambavyo ameshindwa kwa kiasi kikubwa kumudu nidhamu ndani ya CCM.Tatizo kubwa linalomkabiri Kikwete ni kujazana kwa viumbe kadhaa waliofadhili kampeni zake za kupata urais mwaka 2005.Hana jeuri ya kuwadhibiti (japo angeweza kufanya hivyo kama angemudu kuweka ushkaji pembeni).

Katika mazingira ya sasa ambapo CCM imekuwa kama povu linaloelea angani likisubiri japo pini litoboke,chizi yoyote yule anaweza kukurupuka na mkakati wa kihuni wa kusambaza SMS dhidi ya Dokta Slaa.Baadhi ya taarifa zinamhusisha mhuni huyo na familia ya fisadi mmoja mwenye wadhifa mkubwa ndani ya CCM (Like Father Like Son).Au inawezekana kabisa kuwa SMS zina baraka zote za CCM na Kikwete mwenyewe.Katika siasa za kichakachuaji lolote linawezekana.

Back to my point kuhusu uwezekano wa Class Action.Makampuni ya simu yanayoruhusu wateja wao kubughudhiwa na SMS hizo hayawezi kukwepa lawama kuhusu uhuni huu.CCM wanakiri kuwa wao wanatuma SMS njema tu.Je nani anawapa namba za kutuma SMS hizo njema?Jibu ni makampuni yetu ya simu.

Sasa,iwe ni SMS njema au za kihuni kama hizo za dhidi ya Dokta Slaa,lililo dhahiri ni kuwa makampuni hayo yanavunja haki za wateja wao kutobughudhiwa.Na hapo ndipo napojaribu kuwahamasisha wanasheria wazalendo kuangalia uwezekano wa Class Action dhidi ya makampuni hayo.

Nilishawahi kuandika kwenye makala zangu kwenye jarida la Raia Mwema kuhusu upole wa Watanzania hata pale wanaponyimwa haki zao za msingi.Kwa mfano,ni Watanzania wangapi ambao nyumba na mali zao zimeshawahi kuungua kutokana na uzembe wa Shirika la Umeme (TANESCO) lakini wahanga hao wameishia kunung'unika tu badala ya kuwashikisha adabu wana-umeme hao?Ni dhahiri kuwa laiti TANESCO wangefikishwa mahakamani kwa kusababisha shoti japo ya pasi ya umeme tu wangekuwa makini kabla ya kukurupuka kuzima umeme kila wanapojiskia.

Au ni Watanzania wangapi wamepoteza wapendwa wao (kama sio wao wenyewe kupoteza viungo vyao) kutokana na ajali zinazochangiwa na mchanyato wa ufisadi wa matrafiki na wamiliki wa vyombo vya usafiri,lakini wahanga hao wameishia kuomba msaada wa Mungu badala ya kudai fidia?Of course,hakuna fidia inayotosheleza kifo cha mtu lakini tunafundishwa kwenye sosholojia kuwa negative sanctions (kwa mfano adhabu kama faini,kifungo,nk) zinaweza kuzuia wakosaji kurejea tena makosa yao.

Pengine hakuna mwanasheria mzalendo anayepita kwenye blogu hii.Lakini pengine unamfahamu mwanasheria wa aina hiyo.Basi ombi langu ni kumfikishia ujumbe huu wa kuangalia uwezekano wa Class Action dhidi ya makampuni ya simu yanayopuuza haki za wateja wao kwa kuruhusu SMS za kihuni.

TUSIPOZIBA UFA TUNAWEZA KUJENGA UKUTA.LEO SMS NI DHIDI YA DOKTA SLAA KWA VILE MAFISADI HAWATAKI AINGIE IKULU.KESHO KUNAWEZA KUWA NA SMS ZA KUHAMASISHA YALEYALE YA WAHUTU DHIDI YA WATUTSI AU WAISLAMU DHIDI YA WAKRISTO.NA HAYO YANAWEZEKANA ZAIDI KATIKA MAZINGIRA HAYA YA OMBWE LISILOELEZEKA (INCONCEIVABLE) KATIKA MEDANI YA UONGOZI WA TAIFA LETU "CHANGA".




Awali nilitundika taarifa ifuatayo baada ya kuiona huko Jamii Forums kabla ya post husika kufutwa.Mzembe mmoja akanitumia email akidai mie ndio mtunzi wa taarifa hiyo.Mchumia tumbo huyo alikuwa na kila sababu ya kukasirika just like mafisadi wanavyokasirika kusikia uwezekano wa Dokta Slaa kuingia Ikulu baada ya Uchaguzi hapo Oktoba 31.Anyway,naiwasilisha tena kama ilivyo (lengo sio kumridhisha huyo mzushi aliyenituhumu bali kusambaza ujumbe husika)

Taarifa ya Siri-Mikakati ya Kuiba Kura Inavyoendelea
From:
From:
To Journalists   


To:Yahya Mkombe ; Yahya Charahani ; Waziri Kindamba ; Tobias Nsungwe; Thisday [The Editor] ; Theodatus Muchunguzi ; Tanzania Daima ; Tanzania Daima ; Sweya ; Stephen Ernest Kasambo ; Stella Mchiwa ; Stanslaus Kirobo ; Sosthenes Paulo Mwita ; Sofia Machagga ; Siyovelywa Hussein; Sisa Suzy ; Simon Mkina ; Simbaulanga ; Siahanna; Sherbanu Mussa ; Sauli Giliard ; Sarah Mwaga ; Sani; Samson Mwigamba ; Salehe Mohamedi ; Said Michael ; Saed Kubenea ; Rusibamayila ; Ruhazi Ruhazi ; Rookie ; Robert Nyimbo ; Richard Lupembe ; Reginald Simon Miruko ; Ramadhani Semtawa; Raia Mwema ; Prudence Karugendo ; Privatus Karugendo ; Peter Nyanje ; Patien Celkanah ; Paschally Mayega ; Othman Juhudi; Oscar Mkoma ; Oneo Yolazi ; Omari Kaseko ; Omar; Nthelezi Nesaa ; Nombo ; Nkwanzi Nkuzi ; Nikita Naikata; Ngwada ; Ngowe ; News Editor [Thisday] ; News [The Citizen]; Ndyesu ; Ndimara Tegambwage ; Ndesanjo Macha ; Nathan; Nadra Mussa ; Mzee Mwanakijiji ; Mwitete ; Mwesigwa; Mwenyekiti wa Baraza ; Mwankemwa ; Mwanahalisi; Mwachapite ; Mutahungurwa ; Musa Ngarango ; Mumba Mabu; Mum China ; Mtoha ; Matinde Nyagonda ; Mary Fwaja; Martin Malera ; Makwaia wa kuhenga ; Majid Mjengwa ; Mabala wa Mabalaa; Lusungu Hemed ; Lula wa Ndali Mwanzela ; Lukawe ; Ludger Bernard Nyoni ; Lucy Ngowi ; Lucy Mchiwa ; Leo Jasson ; Lawrence Kilimwiko; Laumbe ; Latrix ; Kyembe ; Kwariko Mahmoud ; Kumburu ; Kobelo ; Kiwango ; Kitambo Robert: Padre ; Kililui; Kiangosekazi wa nyoka ; Kevin Makyao ; Kaselema Luhanga; Kambi Mbwana ; Kally ; Kagomba ; Kady Fanny; Julius Samwel ; Joseph Petro ; Joseph Moses Ndumbaro ; Joseph Mgullo; Joseph Kulangwa ; Joseph Kulagwa ; Johnson Mbwambo ; Johnson Mbwambo ; John Mnyika ; Jeff Msangi ; Ipimilo ; Innocent Mwesiga; Ibrahim Lipumba ; Hoja ; Hilda Super ; Herry Gasp ; Henry Kimani ; Hellen [Mama] ; Haruna Sauko Mohamed ; Haruna Sauko Mohamed; Haruna Sauko Mohamed ; Happines Katabazi ; Halifa Shabani ; Hakielimu ; Habibu Miradji ; Habib Miradji ; Godfrey Mogellah ; Gloria William; Gervas Zombwe ; Freddy Macha ; Fred Macha ; Financial Times; Financial Times ; Ezekiel Kamwaga ; Evarist Chachali Uskochi ; Endakig ; Emmanuel Elias ; Elias Mhegera ; Edward Kinabo; Edison Kamukara ; Duhu Daniel ; Deusdedit Jovin ; Deus Bugaywa ; Deogratius Temba ; Dawson Mongi ; David Mhando ; Dattani ; Daniel Mwaijega ; Coster ; Chesi Mpilipili ; Che Chenjah; Charles Semiono ; Charles Nkwabi ; Charles Mullinda ; Charles Kayoka; Charles G. Mnyeti ; Changamoto ; Changamoto ; Chacha Nyakega ; Catherine Justus ; Carol Njiro ; Bwire ; Bwire; Business Times ; Bollen Ngetti ; Beatrice Kawanara ; Beatrice Kallaghe ; Balinangwe Mwambugu ; Bai ; Ayub Rioba ; Asubuhi Njema; Ansbert Ngulumo ; Angetile Osiah ; Angela Semaya; Angel Tenga ; Amina Emmanuel ; Amani ; Alloyce Komba; Alli Gilla ; Alfred Chonya ; Aghan Daniel ; Adam Lusekelo; Absalom Kibanda ; Abdulhamid Njovu ; Abass Juma Msahaury 
Kama nilivyoipokea nami nawatumia. Napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia CHADEMA msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%.
Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya CHADEMA wawasihi CHADEMA wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na NEC/Usalama wa taifa. MAJID KIKULA ambaye ni Government Security Officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005.
Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia Kibaki kupora ushindi wa Odinga. Kikula ww.yahooanatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa NEC na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka Kurugenzi ya IT ya idara ya Usalama (DITA) ambao wako ndani ya NEC kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao.
Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa Undali. Shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya SALVA RWEYEMAMU na MINDI KASIGA kutoka Kurugenzi Ya Mawasiliano Ikulu. Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; MAHARAGE CHANDE ambaye ni mfanyakazi wa VODACOM na EDGAR MASATU wanafanya kazi kwa karibu na NZOWA wa Idara Ya Usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali KUBENEA. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini TANGA kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na Ndg. SINYAU.
Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima JK ashinde kwa 80%.
Ndani ya Idara Ya Usalama Wa Taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa CCM hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura JK, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi.
Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya TISS. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa Usalama Wa Taifa wanafanya nini ndani ya Tume Ya Uchaguzi wakati huu
.

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget