Monday, 11 October 2010


Nimekumbana na post ifuatayo hapo Jamii Forums.Naiwasilisha kama ilivyo kisha tujiulize kwa pamoja (kama tuhuma hizo ni za kweli) wanafanya hivyo kwa faida ya nani?

Taarifa ya Siri - Mikakati ya Kuiba Kura Inavyoendelea USALAMA WA TAIFA
Napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia chadema msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%. Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya chadema wawasihi chadema wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na nec/usalama wa taifa. Majid Kikula ambaye ni government security officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005. Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia kibaki kupora ushindi wa odinga.
Kikula anatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa nec na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka kurugenzi ya IT ya idara ya usalama (DITA) ambao wako ndani ya nec kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao. Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa undali shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya Salva Rweyemamu na Mindi Kasiga kutoka kurugenzi ya mawasiliano ikulu. Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; Maharage Chande na Edgar Masatu wanafanya kazi kwa karibu na Nzowa wa idara ya usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali Kubenea. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini tanga kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na ndg SINYAU.
Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima jk ashinde kwa 80%. Ndani ya idara ya usalama wa taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa ccm hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura jk, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi. Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya tiss. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa  karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa usalama wa taifa wanafanya nini ndani ya tume ya uchaguzi wakati huu.



1 comment:

  1. HAPO INAONYESHA KWAMBA USALAMA WA TAIFA KAMA TAASISI NDIYO KINARA WA HAYA YOTE MATUKIO YA UFISADI, NA PIA WANATAKIWA WABADILISHE JINA SIYO TENA IDARA YA USALAMA WA TAIFA. NI IDARA YA USALAMA WA MAFISADI. PIA HIZO PILIKA PILIKA ZINAZOFANYIKA ZA KUCHACHUA MATOKEO YA KURA ZA UCHAGUZI NDIYO VITU VYA HATARI KWA AMANI YA TANZANIA NA SIYO KUKUIMBILIA KWENDA KUWATISHA WANANCHI KUWA MTU/WATU/KIKUNDI KITACHOJISHUGHULISHA KUVUNJA AMANI WATAWASHUGHULIKIA IPASAVYO KUMBE KIMSINGI WAO WENYEWE TAASISI ZA SERIKALI NA IDARA ZAKE NDIYO WASIOTAKIA MEMA HALI YA AMANI NCHI YAO KWA MATENDO YAO YA KIHALIFU.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget