Ni matumaini yangu kuwa muwazima na mnaendelea na majukumu yenu ya kujenga Taifa au ustawi wa familia zenu popote mlipo.
Ni kitambo kidogo nilitoweka katika ulimwengu wa Kublog, na hiyo ilitokana na majukumu yangu ambayo yalinifanya nihamie Arusha kwa muda ambapo nilijikuta nikiwa na wakati finyu sana kuutenga kwa ajili ya kublog.
Najua kwa wale wapenzi wa Blog ya VUKANI, watakuwa wame-miss makala zangu ambazo kwa kweli zilikuwa zikiibua mijadala mipana ambayo ilikuwa ikifurahisha kuchangamsha na wakati mwingine kukera kidogo.......lakini yote kwangu yalikuwa ni heri tu... lakini pia kwa wale waliokuwa wakifuatilia maoni yangu popote pale nilipokuwa nikichangia mada mbalimbali nao pia walikuwa wanani-miss kwa kuwa napo huko nilikuwa siishi uchokozi.
UCHAGUZI UMEKWISHA!
katika kipindi kizima cha kampeni za uchaguzi karibu blog zote zilikuwa zimedorora, nadhani sikuwa peke yangu, nawapongeza sana wale walioendelea kutupasha habari mbalimbali wakati wa kampeni hususan kaka zangu Evarist Chahali, Mubelwa Bandio,Prof. Matondo,Prof Mbele, Mzee wa Karibu Iringa, Magid Mjengwa Simon Kitururu, Chacha Wambura, Kamala Fadhy Dada yangu Subi, Yasinta na wengine ambao sikuwataja hapa, lakini nilikuwa napitia blog zenu na kujifunza japo mawili matatu.
sasa baada ya uchaguzi kwisha ni vyema wote turejee na nguvu mpya tukiwa na fikra pevu za kuijenga nchi yetu, kuna haja sasa ya kuwa na sauti moja yaani wanablog na wasomaji wa blog kuwahamasisha viongozi wa serikali wasome blog zetu hizi kwani kuna mawazo mengi yanayotolewa katika eneo hili la blog lakini yameachwa tu yapotee bila sababu.
Ni vyema kuunganisha nguvu zetu bila kujali vyama, maana najua wengi tumeumia mioyoni mwetu baada ya kuona yule tuliyemtegemea hakutangazwa na tume kuwa ndiye mshindi, lakini mimi naamini kuwa kwa kiasi kikubwa vyama vya upinzani vimeshinda uchaguzi wa mwaka huu, kwani kwa nguvu ndogo walizokuwa nazo kwa maana ya nguvu ya kifedha, lakini wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa kuzoa wabunge na madiwani wengi nchini na hivyo kuonyesha kuwa wananchi wamewakubali.
Tunahitaji sasa kuonesha mshikamano, na kumsaidia bwana mkubwa aliyeko madarakani ili aweze kutuvusha katika miaka mitano hii aliyobakiza salama.Tunatakiwa kukosoa kwa nia ya kujenga na kuelekeza na ikibidi kufundisha........katika tasnia hii ya wanablog naamini kuna vichwa vilivyojaa hekima na mawazo mapya, na ninaamini hata wao wanalitambua hilo
Nimerejea lakini sidhani kama nitakuwa na nguvu kama ile ya kipindi kilichopita kwa sababu ya kutingwa na mambo ya kujiimarisha kiuchumi......
nawatakia kila la kheri na mafanikio mema katika kipindi hiki cha kuumaliza mwaka huu wa 2010.
Ni mie Koero Japhet Mkundi
ASANTE SANA DA KOERO.NAMI NAKUTAKIA HERI NA MAFANIKIO MEMA KATIKA KIPINDI HIKI KILICHOSALIA KABLA YA KUMALIZA 2010 NA SIKU ZOTE.
ASANTE SANA DA KOERO.NAMI NAKUTAKIA HERI NA MAFANIKIO MEMA KATIKA KIPINDI HIKI KILICHOSALIA KABLA YA KUMALIZA 2010 NA SIKU ZOTE.
0 comments:
Post a Comment