Wednesday, 3 November 2010

MGOMBEA urais kupitia tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo, (Chadema), Dk Willibrod Slaa amesema, atayakataa matokeo ya urais yatakayotangazwa na Tume ya Uchaguzi (NEC) kwa kuwa kumefanyika wizi mkubwa wa kura.Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dk Slaa alisema, kama NEC inaitakia mema nchi hii, ifute matokeo yote ya urais na uchaguzi urudiwe upya.

Dk Slaa ambaye pia ni Katibu Mkuu wa chama hicho, alisema wamekuwa wakifuatilia matokeo ya nchi nzima kwa umakini mkubwa na wamegundua kuna wizi mkubwa wa kura kwenye nafasi za urais na ubunge.

"Kuna uchakachuaji mkubwa wa kura na kazi hiyo inafanywa na usalama wa taifa,"alisema Dk Slaa

Chanzo: Mwananchi
ENDELEA KUFUAtILIA BLOGUNI HAPA

7 comments:

  1. kinachoshangaza wakati washabiki wa chadema wanalinda kura ccm washabiki hawakuonekana hiyo ni kuonyesha hawakuwapo ni mikaratasi tu, cha muhimu mafisadi wameshindwa mwanza, dsm, mbeya, arusha, iringa hiyo tu inanifurahisha pamoja na wanyonge wote

    ReplyDelete
  2. Kichekeeeeshooooo....SITAYATAMBUA MATOKEO!!!!!
    Mawakala walikuwepo...kura zilihesabiwa vituoni...takwimukila mtu anazo...leo tume inatangaza..ati sitayatambua matokeo....Mfa maji haachi kutapatapa....mashabiki wa chadema kweli walilinda kura...na kweli walisimamia zoezi lote lakini wameambulia.....viti 24 tu kati ya viti 239
    wapi na wapi.....nilikwambia bwana Chahali msomi wa shahada za Phd mbili na mjasiriamali wa ughaibuni...HATUDANGANYIKI........Huko chadema ilikopata kura ni kule ambapo sisi tuliweka wagombea ambao wana CCM hawakuwakubali...lakini tumejifunza...come 2015

    ReplyDelete
  3. ccm wanaona haya kuvaa magwanda yao njano na kijani wanajua hawakubaliki, chadema chama cha wanyonge tunawashukuru wanyonge wa mwanza la jimbo hilo tu limetuweka HURU, wakome wanaoshangilia mafisadi kushinda halafu wanawapa watu kofia na tshirt, mwaka huu wamesweat, koma we unaeumiza wanyonge , cha kukufurahisha kipi wagonjwa wafa hospitali bila dawa, na shule za kata michango kila siku

    ReplyDelete
  4. Ataukibeza wapinzani kwakweli kila mtanzania mwenye akili timamu anajua JK amechukua nchi kimabavu kipindi hiki. Inaonyesha wazi hata watu wandani ya CCM hawampi sapoti ndio maana wabunge wameanguka vibaya. Lakini hii ni dalili za mvua tu bado mvua yenyewe. Watu ndani ya CCM ndio wanaotoa siri zote za chama ndio maana unaona haya yanayoonekana. Ni vizuri tukijifunza kutenda mema wakati wote maana hujui mbaya wako atakua nani in the future. I can smell very bad days to come for some people in CCM. Kweli kila kitu kinamuisho wake. Mobutu na Moi waliweza kuangushwa nani ambaye hawezi kuangushwa????

    ReplyDelete
  5. mimi nafikiri Dr Slaa hana ushirikiano mzuri na wenzake kwani angeweza kumuuliza ndg Mbowe F. na Mrema L.A kama kuja watu wengi katika kampeni determines upendo wao kwao na ishara yao ya kuwa watakuchagua wewe, hili hakufanya ufuatiliaji na kuona kama waliokuwa wakijaa katika mikutano yake ni wana CCM ila ni kwa kuwa haikuruhusiwa kuvaa sare za chama chako ikwa ni tofauti kinachofanya mkutano anaosikiliza ukiwa katika mikutano ya kampeni ya chama kingine hapo ngejua kuwa wengi hawakuwa wafuasi wake bali ni wsikiliza sera ( mzee maskat wa kitangali.

    ReplyDelete
  6. hebu kapaukie mbele we unaejidai maskini wa maskati chadema chama cha wanyonge kwa hiyo wote waliojaa mwanza, mbeya, iringa walikuwa wafuasi wa ccm, haya huna mzee mzima la kutokuvaa sare za ccm kila mtu analijua sababu unahusishwa na mafisadi, kwa aibu inabidi wasivae

    ReplyDelete
  7. Anon hapo juu labda ujiulize tu nini kilimtoa Lowassa monduli kwenda halmashauri ya Arusha wakati majibu yanataka kutangazwa? Na pia ujiulize nini kilimtoa Kikwete Dar kwenda Mwanza wakati majibu yanataka kutangazwa? Vile vile ni kwanini inalazimika kumlinda mbunge wa Shinyanga ambaye wanasema amechaguliwa na kura nyingi na wananchi? Kama amechaguliwa na wananchi wengi si hao waliomchagua wamuhakikishie usalama hapa kwanini jeshi la Polisi. Natumaini wewe ni mtu mwenye akili timamu unaweza ukapata majibu sahihi ya maswali kama hayo la sivyo utakua unatanguliza hisia kabla yakufikiri.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget