Mmoja ya mabloga ninaowaheshimu,Bwana Nkwazi Mhango (pichani juu) amenishushia tuhuma nzito akidai nimepokea hongo ya mafisadi kama inavyoonekana kwenye baruapepe ifuatayo (BONYEZA PICHA KUIKUZA)
Kama hukuweza kuisoma vizuri basi nainukuu hapa chini
Anonymous has left a new comment on your post "Nova Kambota: VIVA KAMANDA LOWASSA":
Publish
Delete
Mark as spam
Moderate comments for this blog.
Posted by Anonymous to Kulikoni Ughaibuni at 11/12/2011 01:16
Chahali umenisononesha. Umeingiwa na nini hadi unampamba huyu fisadi wa kunuka? Sikuamini kuona naweka shairi langu la kumjibu huyu mtoto changudoa wa maadili wa Lowassa na ukalifuta. Kweli binadamu si viumbe wa kuamini. Hata hii futa kwa maslahi yako. Ila jua legacy uliyokwisha ijenga ina thamani kuliko hiyo hongo ya mabaki ya ufisadi.
Nkwazi Mhango Publish
Delete
Mark as spam
Moderate comments for this blog.
Posted by Anonymous to Kulikoni Ughaibuni at 11/12/2011 01:16
Lakini cha kusikitisha ni ukweli kwamba baruapepe yenye shairi la Mhango analodai nililifuta (kutokana na hongo ya mafisadi) lilinifikia masaa mawili na dakika 31 baada ya barua pepe ya lawama.Kama ulivyoona katika picha ya hapo juu,Mhango alinitumia braua pepe ya kwanza (ya lawama) saa 7 na dakika 11 usiku kwa muda wa hapa Uingereza (angalia kulia juu kwenye email utaona imeandikwa Sent: Sun 11/12/2011 01.17).
Sasa angalia picha ya email ya shairi la Mhango hapa chini (cha muhimuni ametuma muda gani)
Kama picha inavyoonyesha,shairi la Mhango lilitumwa saa 9 na dakika 48 usiku kwa saa za hapa kama inavvoonekana katika picha hapo juu (kulia juu kuna maandishi kuhusu muda ambapo inasomekana bayana Sent on 11/12/2011 03.48
Anyway,nimekuwa nikimheshimu sana Bwana Mhango (na mmoja wa ushuhuda wa heshima yangu kwake ni makala hii ya Januari MWAKA 2008 isemayo MPAYUKAJI MSEMAOVYO...AU MSEMAKWELI? (bonyeza link kuisoma)
Tangu nianze uandishi wa blogu na makala sijawahi kupata tuhuma nzito kama hizi.Kinachosikitisha zaidi ni ukweli kwamba Mhango anafahamu fika nimetoka wapi katika vita yangu ya jeshi la mtu mmoja (one-man army) dhidi ya ufisadi.Anafahamu pia masahibu yaliyonikumba kutokana na mapambano hayo.Kwa hakika ngepaswa kuwa mtu wa mwisho kabisa kusema hayo aliyosema.Lakini kama alivyoandika mwenyewe,KWELI BINADAMU SI VIUMBE WA KUWAAMINI.
Natumaini baada ya kubaini kuwa alikurupuka kunilaumu kabla ya kuangalia vema kama shairi lake limeshanifikia,atafanya uungwana wa kuniomba samahani.
Bwana Chahali, kwanza nasikitika pili nimeshangaa. Hizo shutuma kwa ufupi si zangu. Nadhani watu wameamua kutafuta umaarufu kwa kugonganisha majina yetu. Kwanini nisikuandikie email kwanza wakati nina anwani yako. Yawezekana chanzo cha yote haya ni makuwadi wa mafisadi wanaotaka publicity kwenye blog zetu ili wanaowatuma waone "wanavyochapa kazi hii chafu." Muhimu usiyape uzito hayo madai. Najua chanzo cha huu ujumbe ni Jamii forums ambapo kuna watu wanajiita Mhango, Mpayukaji na hata kutumia avatar zangu kiasi cha kunilazimisha kubadili kila mara. Pole sana ndugu yangu.
ReplyDelete