Sunday, 28 March 2010


Kwa mara nyingine,baadhi ya Watanzania waishio Uingereza walipata nafasi ya kuhudhuria mkutano uliobeba jina la Diaspora Forum 2.Binafsi sikuhudhuria,sio kwa vile sikuona umuhimu wa kufanya hivyo bali nilitingwa na majukumu binafsi.Hata hivyo,laiti ningehudhuria ningejaribu kutoa mchango wa kwanini uhamasishaji kwa Watanzania walio nje kurejea nyumbani au kuchangia maendeleo ya taifa unaweza kuendelea milele pasipo kupatikana mafanikio yanayokusudiwa. Pamoja na nia nzuri ya kuwepo forums kama hiyo ya Diaspora,lakini ni muhimu kutambua kuwa kikwazo kikubwa cha maendeleo yetu kama taifa hakijawahi kuwa kwenye mipango mizuri.Tanzania tumebahatika kuwa na viongozi wenye uwezo wa hali ya juu katika kuongea na kubuni mipango mizuri.Lakini,kwa bahati mbaya au makusudi,wengi wa viongozi hao ni wazembe wa daraja la kwanza linapokuja suala la utekelezaji mipango including waliyoibuni wao wenyewe.Unajua kuna tofauti kati ya uzembe katika kutekeleza mawazo ya mwenzako na uzembe katika kutekeleza mawazo yako binafsi.Kwa mfano,hakuna mtu aliyeishauri CCM kuja na kauli-mbiu ya "ARI MPYA,KASI MPYA NA NGUVU MPYA" au ile ya "MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA".Uamuzi wa kuja na kauli-mbiu hiyo ulikuwa wa CCM binafsi pasipo shinikizo kutoka kwa wafadhili,viongozi wa dini,wananchi au kikundi chochote kile.Nafahamu wapo watakaobisha kuwa kauli-mbiu zote hizo zimeishia kuwa kauli-mbiu tu pasipo matokeo kuonekana,lakini ukweli ndio huo,na shurti uwekwe wazi.

Back to the Diaspora thing.Kwanza,katika mazingira ya kawaida,haihitajiki kumhamasisha mwananchi kurudi nyumbani kwake au kuchangia maendeleo ya alikotoka.Wengi wa Watanzania walioko ughaibuni hawahamasishwi kusaidia ndugu na jamaa zao walio Tanzania bali wanafanya hivyo kwa vile wanatambua kuwa ni wajibu wao.Naamini kuwa wengi wa wanaokumbuka ndugu na jamaa nyumbani wanasukumwa zaidi na namna misaada yao inavyosaidia walengwa huko nyumbani.Sidhani kama kuna mtu ambaye kila wiki au mwezi anakwenda Western Union,Moneygram au "Kwa Wapemba" kutuma pauni zake alizopata "kwa mbinde" only for watumiwa huko Tanzania kuendeleza libeneke la anasa.

Ninajaribu kutumia mfano wa ndugu na jamaa kama mahala pa kuanzia kabla ya kuangalia namna Watanzania walio nje wanavyoweza kufanya the same kwa nchi yao.Kwa bahati mbaya,forums kama Diapora 2 hazitoi sura ya pili ya hali ilivyo huko nyumbani.I wish miongoni mwa waalikwa wangekuwa taasisi zinazohamasisha Watanzania walio nje kuchangia kuleta mabadiliko ya haraka kwenye mwendendo na hatma ya taifa letu.Yah,Diaspora forums zinaweza kuhamasisha Watanzania wote walio ughaibuni kurejea nyumbani au kuchangia asilimia kadhaa ya vipato vya kujenga taifa letu "changa" (sijui lini litakua),lakini kwa hali ilivyo sasa,watakaoendelea kunufaika ni wateule wachache wafahamikao kama MAFISADI.

Na tatizo jingine linalotukabili Watanzania wengi ni usikivu uliotukuka pasipo udadisi.I hoped mshiriki mmoja angemuuliza Waziri Membe kuhusu commitment ya watwala wetu katika kupambana na ufisadi underlining mifano kama dilly-dallying za kuwachukulia hatua majambazi wa Kagoda au hili skandali jipya la trilioni za stimulus package ambapo tunaambiwa kuwa mafisadi came up with some phony companies to create another EPA-like swindle.

Binafsi napenda kuamini kuwa moja ya negative legacy za itikadi ya Ujamaa ni kwa wananchi kupenda kunyenyekea viongozi "kikasuku".Utaona wananchi wakihangaika kupata nafasi za kupiga picha na kiongozi badala ya kumkalia kooni kumuuliza kwanini mamabo yanaenda mrama.Unadhani laiti Mugabe au Waziri wake akija UK na kukutana na Wazimbabwe waishio hapa "patatosha"?And I don't mean kufanyiwa vurugu bali kubanwa na mwaswali ya msingi kwanini mambo yanakwenda mrama.Lakini kwa akina sie,mdau akishapata picha na kigogo kisha akaipenyeza bloguni basi anakuwa ame-achive lengo kubwa kabisa.

Naamini,hata kama ntapingwa,kuwa Watanzania walio nchi zinazojitahidi kuwatumikia wananchi kwa namna inavyostahili (kama hapa Uingereza,though it couldn't always be absolutely perfect) hawawezi kukwepa lawama za michango yao hafifu katika kuboresha hali ilivyo huko nyumbani.Siamini kama ni ubinafsi au imani kwamba "hata tukisema haitobadilisha kitu" bali ni kasumba ileile inayokwaza mabadiliko huko nyumbani kwamba kwa namna ya miujiza,watu walewale wanaokwaza maendeleo yetu wataamua kwa hiari yao kubadilika na kisha kuutumikia umma kwa ufanisi.Hivi,kwa Watanzania walio Uingereza,hatuoni namna Labour wanavyobanwa mbavu katika jitihada zao za kurejea madarakani?Na si kwamba wame-perform vibaya kihivyo-compared to our CCM-lakini taxpayers wa Uingereza wanaamini kuwa good is not good enough,they want better if not the best from Labour.

Juzijuzi,Makamu Mwenyekiti wa CCM,Pius Msekwa,alifanya ziara hapa UK lakini akanusurika pasipo kubanwa na wana-CCM wenzake kwamba,kwa mfano,kwanini chama hicho kinashindwa kuwachukulia hatua viongozi wanaotuhumiwa kuhusika na ufisadi.Mimi si mmoja wa wanaobeza uanachama wa CCM nje ya nchi kwa vile natambua kuwa hiyo ni haki ya kikatiba ya kila Mtanzania.By the way,kuna Democrats Abroad na Republicans Abroad which are more or less the same as na matawi ya CCM nje ya nchi.Nadhani wanaopinga uanzishwaji wa matawi ya CCM nje ya nchi au unachama wa matawi hayo wanasukumwa zaidi na ukweli kwamba kuna madudu mengi yanayolelewa na CCM huko nyumbani.Sasa inatarajiwa kuwa wana-CCM walio nje ya nchi wakisaidie chama hicho tawala kutambua kuwa mwenendo wake unawaangusha Watanzania.Na wanatarajiwa kufanya hivyo kwa vile wana advantage ya ku-compare and contrast as to kwanini,kwa mfano,Labour inaweza lakini CCM inashindwa.Yaani,kama Labour inaweza kuwakalia kooni wabunge wake kwenye expenses scandal kwanini basi CCM ishindwe kumbana mtu kama Mzee wa Vijisenti ambaye hadi muda huu ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ndani ya chama hicho?

Nimaelizie kwa kupongeza waandaaji wa Diaspora Forums kwani naamini kuwa wanachofanya kina umuhimu mkubwa.Hata hivyo,umuhimu huo unakwamishwa na ukweli kwamba mazingira ya nchi yetu kwa sasa yanakwaza wengi wa Watanzania walio nje kuchangia jitihada za ujenzi wa taifa.Hakuna anayetaka kuona fedha anazochuma kwa mbinde zinaishia kunufaisha nyumba ndogo za mafisadi huko nyumbani au kuongeza idadi ya mahekalu yao.Diaspora forums zinaweza kufanywa hata kila baada ya wiki lakini hazitazaa matunda yanayokusudiwa-au kubaki photo ops tu-laiti mwenendo wa mambo huko nyumbani hautarekebishwa.

2 comments:

  1. JARIBU KUIMODIFY BLOG YAKO INAUMIZA MACHO EITHER BADILI RANGI UNAZOTUMIA AU CHANGE BACKGROUND, I WONDER IF NOBODY HAS EVER TOLD YOU THIS. LUCY.

    ReplyDelete
  2. Hili la kutouliza viongozi sijui litaisha lini?
    Tunachanganya UOGA na AMANI.

    Wala hapa sitachangia saana maana nahisi forums nyingi zinaiacha nje jamii hitajika katika hili

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget