Wiki hii tumeadimisha siku ya wanawake duniani.Na kesho ni siku ya mama zetu.Ni kipindi mwafaka cha kungalia mchango wa jinsia ya kike katika ngazi ya familia hadi taifa.Tukubali tusikubali,dunia imeendelea kutawaliwa na mfumo dume.Na bara letu la Afrika (na pengine sehemu kubwa ya Dunia ya Tatu) haki za akinamama na mchango wa jinsia ya kike vimeendelea kupuuzwa.Kwa bahati nzuri kwangu,kabla wiki hii muhimu haijamalizika nilipata wasaa wa kuongea na bloga maarufu wa Kitanzania,Sarah Peter,mmiliki wa blogu ijulikanayo kama ANGALIA BONGO. Sihitaji kumpamba kwani ukitembelea blogu hiyo utaafikiana nami kuwa binti huyu licha ya udogo wake wa umri ana kipaji cha hali ya juu katika kuwasilisha ujumbe wake kwa wasomaji wa blog yake na jamii kwa ujumlaNimejijengea mazingira ya kutembelea takriban blogu zote za Watanzania wenzangu kila siku,au angalau mara kadhaa kwa wiki.Licha ya idadi kubwa ya blogu hizo kuwa kwenye blogroll yangu,nina orodha kubwa ya subscription kwenye Google reader,na inanisaidia sana kufahamu kinachoendelea kwenye blogsphere.
Back to Sarah.Nilianza kublog mwaka 2006 na tangu wakati huo blogging imekuwa sehemu muhimu ya maisha yangu.Lakini hadi jana nilikuwa sijakutana na bloga ambaye ndani ya dakika chache alinifumbua macho kwa kiwango kikubwa as to wapi panahitaji marekebisho bloguni mwangu na namna nyingine za kunoresha uwanja huu.Lakini ukidhani hilo ni kubwa zaidi,basi tembelea kwanza hiyo blog ya ANGALIA BONGO kisha utapata picha nzuri zaidi ya nachokieleza.
Nimekuwa nikifuatilia kwa karibu kuhusu blog hiyo hasa kiu yangu ya kumfahamu vema mmiliki wake.Awali nilidhani kuwa Sarah ni 'mtu mzima' (kiumri) kwani nyingi ya posts zake zimesheheni upeo unaoendana na utu uzima.Tofauti na dhana hiyo,kumbe Sarah ni binti aliyezaliwa miaka ya 80 hivyo ana miaka ishirini na kitu (lakini haifiki 25).Kwa kifupi,ni binti mdogo mwenye akili kubwa na kipaji cha hali ya juu.Na siandiki hivi kwa minajili ya 'kumpa ujiko' (hata ningekuwa nafanya hivyo ingekuwa kazi bure kwani tayari ana 'ujiko' wa kutosha)bali ni katika kutambua mchango wa jinsia ya kike katika fani ya habari hususan kwenye matumizi ya vipasha habari vya jamii (social media) kama blogu.
Hata hivyo,pamoja na mwonekano maridhwawa wa blogu ya ANGALIA BONGO na habari zenye kila ishara kuwa aliyeandika anajua vema anachofanya,kumwelewa vema Sarah kunahitaji uongee nae kama ilivyotokea kwangu jana.Alinipa darasa la chapchap kuhusu mambo mbalimbali ya maana.Na mie ni mwanafunzi mzuri napokutana na mwalimu mzuri.Na haikuchukua muda kwangu kabaini kwamba binti huyu ana akiba kubwa ya akili na kipaji,na hadi sasa kinachotumika ni kiasi kidogo tu cha kipaji na akili hiyo.Sasa kama kiasi kidogo ndio mambo makubwa namna hiyo,ni dhahiri kuwa bloga huyu atakuwa mbali sana akiamua kutumia uwezo wake wote(na anasema atafanya hivyo mbeleni).
Ukiangalia picha zake,unaweza kumhukumu isivyo.Ana mwonekano wa 'kisistaduu' (sina tafsiri sahihi ya neno hili) na ni rahisi kudhani ana 'pozi' (maringo).Lakini hata kama angekuwa hivyo (i.e. sistaduu mwenye pozi),which she is not,character hizo zingefunikwa na kipaji na upeo wake.Sarah anaeleza kwamba yuko into many stuffs japo amebobea zaidi kwenye mambo ya burudani (entertainment).Licha ya background yake kama journalist na radio producer,uwezo wake wa kufikiri na kuandika haraka unachangia sana kuifanya blog yake kuwa mahala pa kumridhisha kila msomaji anayepatembelea.Lakini kingine kinachopendeza katika wasifu wa binti huyu ni imani yake ya kiroho.Anasema kuwa dini ni kitu muhimu sana katika maisha yake,na kwa kuthibiths ahilo ameandika I...always believe in Jesus, Remember Ä°m a pure Christian.Imani thabiti katika dini inasaidia sana kuimarisha vipaji na kutanua upeo,na ni ishara ya karama za Muumba.
Ni dhahiri kuwa bloga huyu ana nafasi ya kufanya mambo makubwa huko mbeleni,na ni matarajio yangu kuwa siku moja Sarah ataitangaza nchi yetu si tu kupitia blog yake bali pia katika fani flani muhimu.Nilimtania kuwa this time in 2012 or so natarajia kumuona akiwa katika delegation ya Mama Asha Rose Migiro,sio kwa vile ni Mtanzania mwenzake bali akiwajibika katika wadhifa flani.Na kama si hilo,basi sintoshangaa akija na chapisho kama Ebony au The Source ya kitanzania.
Kila la heri Sarah!
0 comments:
Post a Comment