Sunday, 20 June 2010

RAIS Jakaya Kikwete ameliponda Shirika la Haki Elimu kwa kusema ni waongo, wazushi na wanafiki.

“ Ukweli siku zote hujitenga na uongo Haki Elimu ni waongo, wazushi na wanafiki wanapodiriki kuwatangazia umma wa watanzania eti kuna uhaba wa nyumba za walimu zipatazo 22,000 nchini na kwamba Serikali ya Nne kwa kipindi chote cha utawala wake kimemudu kujenga idadi ya nyumba za walimu zipatazo 300 tu haya ni matusi kwetu….kweli akutukanae hakuchagulii tusi…..watu wazima ovyoo” amesema Rais

---------------------------------------------------------------------------------------------------------
RAIS Jakaya Kikwete amesema Serikali ya Awamu ya Nne imetekeleza kwa vitendo ahadi zote za uchaguzi ilizowaahidi wananchi ukiwamo ujenzi wa miradi mikubwa mitatu ya barabara kuu za mkoa wa Rukwa zenye urefu wa kilometa 657.5 kwa kiwango cha lami.

“Tuliyowaahidi wananchi tumeyatekeleza kwa hakika tumefanikiwa vizuri sana katika ujenzi wa barabara, elimu na afya,”

Alisema hayo juzi wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kiwanja cha michezo cha Nelson Mandela mjini hapa, huku akishangaa wanaobeza safari zake za nje ya nchi.

Alisema watu hao hawamnyimi usingizi hata kidogo na alihoji kama asingekwenda Marekani kuonana na Rais George Bush (mstaafu) nani angefadhili ujenzi wa mradi mkubwa wa barabara ya Tunduma – Laela – Sumbawanga yenye urefu wa kilometa 224.5 kwa kiwango cha lami.

LAKINI NI MAJUZI TU GAZETI LA HABARI LEO LILIMNUKUU RAIS AKISEMA YAFUATAYO

AHADI ambazo hazijatekelezwa na Serikali ya Awamu ya Nne zitatekelezwa katika Bajeti hii ya mwaka 2010/11, imeelezwa.

Akizungumza jana mjini hapa katika kikao cha kazi na wakuu wa mikoa na wa wilaya pamoja na makatibu tawala wa mikoa yote Tanzania Bara, Rais Jakaya Kikwete aliwataka viongozi hao kusimamia shughuli za Serikali kikamilifu.

Aliwataka kutokwenda likizo katika kipidi hiki cha kuelekea uchaguzi na wasimamie kazi kama wanavyofanya wakati wote.
Rais Kikwete alisema katika kipindi cha miaka mitano tangu Serikali yake iingie madarakani mengi waliyoahidi yametekelezwa.

“Juzi kabla ya Bajeti hata kwenye Baraza la Mawaziri, tulizungumzia ahadi zetu na nyingi tumeshazitekeleza, lakini zilizobaki na majukumu tuliyojipangia kwa miaka yote hii tutatekeleza katika Bajeti hii … tulipoingia mwaka wa kwanza, tulitekeleza ya Awamu ya Mzee Mkapa (Rais mstaafu Benjamin) sasa tunaendelea na kutekeleza yetu,” alisema.

SASA KAMA AHADI ZOTE ZIMESHATEKELEZWA,HIZO ZINAZODAIWA KUTEKELEZWA KATIKA BAJETI HII YA 2010/11 NI AHADI ZIPI TENA?

NA SOTE TUNAKUMBUKA THE MOTHER OF ALL PROMISES,ILE YA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA.HIVI KWELI RAIS KIKWETE ANATAKA KUTUAMBIA KUWA KILA MTANZANIA HIVI SASA ANA MAISHA BORA?

KADHALIKA JK ALITAMKA BAYANA KUWA ANAWAFAHAMU WALA RUSHWA KWA MAJINA NA KUSEMA ANAWAPA MUDA WAJIREKEBISHE VINGINEVYO ANGEWACHUKULIA HATUA.JE RAIS ANAPOTUAMBIA KUWA AHADI ZOTE ZIMESHATEKELEZWA ANAMAANISHA TATIZO LA RUSHWA NALO LIMEKWISHA?AU ANAMAANISHA WALA RUSHWA ALOSEMA ANAWAFAHAMU KWA MAJINA WAMEAMUA KUJIREKEBISHA?

-----------------------------------------------------------------------------------------------
RAIS Jakaya Kikwete amewataka wanaume wasiwe 'mafataki', wawaache watoto wa kike wasome.

Kikwete amesema, wanaume wanapaswa kuwafuata wanawake wakubwa wenzao na si watoto, na kwamba, wanawake wapo wengi.

“Ninachowaomba wanafunzi wa kike washuhulike na masomo, mambo ya mimba yaacheni… kina baba waacheni watoto wa shule kina mama watu wazima wamejaa tele acheni kupiga ufataki” Rais Kikwete ameyasema hayo wakati anajibu swali la mtoto Rehema Abbas wa Dar es Salaam.

HAYA NI MAENDELEO MAPYA BAADA YA KIKWETE HUYUHUYU KUSEMA YAFUATAYO HIVI KARIBUNI

JK: Mimba kwa wanafunzi ni kiherehere chao

Monday, 07 June 2010 07:33
Rais Jakaya Kikwete amesema matukio ya mimba kwa wanafunzi wa kike nchini yanasababishwa na viherehere vya wanafunzi wenyewe.

Aidha, Rais Kikwete amekiri kwamba matukio ya mauaji ya vikongwe pamoja na watu wenye ulemavu wa ngozi (albino), yanalidhalilisha taifa.

Rais Kikwete alitoa kauli hizo katika kijiji cha Kisesa wilayani Magu jana wakati akihutubia wananchi kwenye ufunguzi wa mashindano ya ngoma kwa kabila la Wasukuma; ngoma ambazo zinajulikana kama 'Bulabo'.

" Kila anayepata Ukimwi anaufuata mwenyewe na wengine ni viherehere vyao; kwa mfano watoto wa shule," alisema Rais Kikwete wakati akijibu risala ya Mkurugenzi wa Makumbusho ya Bujola, Fadha Frasince Sandhu, ambaye alisema ujumbe wa mashindano hayo mwaka huu ni vita dhidi ya mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi.

Kwa mujibu wa Rais Kikwete, suala la zinaa kwa bianadamu, siyo la lazima hivyo binadamu anaweza kujizuia ama kujikinga kwa kutumia kondomu.
-------------------------------------------------------------------------------------------------------------

4 comments:

  1. Mimi nahisi kumwa huyu JK anakuwa na kichocheo cha ulevi pengine wakati anaongea mambo makini na kulihutubia Taifa...hizi kauli zake kujijitetea kusema wanaomkosoa ni wanafiki ....nadhani hiyo hali anayo yeye mwenyewe bila kujitambua kwamba mara nyingi kauli zake ni za kinafiki na kejeli kwa watanzania maskini...Upumbavu na ujinga wa sisi wapiga utathibitishwa iwapo tuu tutampitisha tena kipindi cha pili cha utawala wake na wabunge wa CCM kuwa wengi bungeni na hapo ndiyo tutajua sisi tunapenda na pia tumeridhika kuwa mafukara wa kutupwa

    ReplyDelete
  2. waacheni mademokrasia wachukue nchi, ccm wakikaa miaka minne bila kazi ndio watajifunza. Biashara mashindano, maendeleo yanataka challenge.

    ReplyDelete
  3. Kweli mkuu umefanya "pictorial analysis" ambayo haina kubishana wala kulumbana.... wenye macho wanatakiwa kuona na sio kulumbana.... this is fantastic .... thanx sana

    ReplyDelete
  4. Ni hali ya kusikitisha sana na ya kutia hofu pale Rais wa nchi anavyoweza kutumia lugha ya kejeli au ya kinafiki katika kuhutubia umma!...Na hii ni mwanzo tu,kwa kuangalia picha zote hapo juu,na kwa kusoma habari yote iliyo andikwa kwa umahiri,mimi sioni haja ya kuendelea kumpa nafasi katika kipindi hiki cha pili!.Hakuna ahadi yoyote ile ambayo imetekelezwa kwa asilimia mia,nyingi ya ahadi zake ni chini ya asilimia 50,hii ni kuwafumba macho wale wenzangu tunaoangalia yaliofanyika jana bila kuzingatia uimara wake!...

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget