Thursday, 10 June 2010

Uandishi wa blogu si jambo rahisi kama inavyodhaniwa na wengi.Na ni jambo gumu zaidi kwa akina sie tunaoelemea zaidi katika kuandisha mambo yanayogusa maslahi ya mafisadi na vibaraka wao.Kwa mfano mara kadhaa nimekuwa nikipata comments zenye matusi ya kila aina kutoka kwa baadhi ya wasomaji.Huwa siyachapishi matusi hayo kwa vile naamini wanaotukana wana mtindio wa mawazo na tafakuri.Hoja hujibiwa kwa hoja na wala si matusi.

Ninafahamu matusi hayo yanatoka wapi,na pia natambua kwanini badala ya hoja zangu kujibiwa kwa hoja zao wanakimbilia kutukana.Ni hivi,ukiona mtu anakusema vibaya au kukutukana wakati hujamkosoea lolote ujue mtu huyo hana zuri upande wake,na maneno mabaya au matusi dhidi yako inakuwa kama njia ya mkato ya kupunguza matatizo yake.Watu wa aina hii wanahitaji ushauri nasaha badala ya kuwatukana.Na kibaya zaidi ni kwamba ukimtukana chizi,basi watu watashindwa kutofautisha kati ya nani mzima au mwenye busara na nani chizi.

Lakini wapenda matusi hawa wananipa faraja moja kubwa.Kwamba hadi kufikia hatua ya kutukana kwa njia ya comment kwenye blogu hii inamaanisha walitumia muda wao kusoma nachoandika.Hiyo ni faraja kubwa kwangu kwani walengwa wangu wakuu ni watu makini na sio vichwa panzi kama hao mabingwa wa matusi.

Ujumbe wangu mfupi kwa wazembe hao wa kufikiri ni huu: kasheshe nilizokumbana nazo huko nyuma kutokana na mtizamo wangu ni mara alfu ya hivyo vijimatusi mnavyotuma kama comments.Kwahiyo endeleeni kupoteza muda wenu kutukana lakini mkae mkifahamu kuwa mnachofanya ni sawa na kutegemea damu kutoka kwenye jiwe.

Anyway,nasikitika kupoteza muda wangu muhimu kuwazungumzia wazushi hawa.Lakini yote katika yote,hivi ni vijimambo tu ambavyo once ukiingia kwenye fani ya kublogu lazima utakumbana navyo.

Bring it on!

Related Posts:

  • Ukiona Mtu Anajikuna Basi Ujue AnawashwaUandishi wa blogu si jambo rahisi kama inavyodhaniwa na wengi.Na ni jambo gumu zaidi kwa akina sie tunaoelemea zaidi katika kuandisha mambo yanayogusa maslahi ya mafisadi na vibaraka wao.Kwa mfano mara kadhaa nimekuwa nikipat… Read More
  • Sarah,the Brains Behind Angalia BongoWiki hii tumeadimisha siku ya wanawake duniani.Na kesho ni siku ya mama zetu.Ni kipindi mwafaka cha kungalia mchango wa jinsia ya kike katika ngazi ya familia hadi taifa.Tukubali tusikubali,dunia imeendelea kutawaliwa na mfum… Read More
  • Kutoka kwa Dada Koero Kundi: UJIO WANGUNi matumaini yangu kuwa muwazima na mnaendelea na majukumu yenu ya kujenga Taifa au ustawi wa familia zenu popote mlipo.Ni kitambo kidogo nilitoweka katika ulimwengu wa Kublog, na hiyo ilitokana na majukumu yangu ambayo yalin… Read More
  • UOGA: UGONJWA UNAOTUKWAZA WATANZANIAHivi karibuni niliandika makala flani kuhusu milipuko ya mabomu huko Mbagala, jijini Dar es Salaam. Kwa kutambua kuwa blogu yangu haina idadi kubwa ya wasomaji (japo nawathamini sana wachache wanaotumia muda wao kuitembelea) … Read More
  • My Honest Reply to the So-called "Meya wa Mzumbe"You posted the following comment on this blog.I have tried to reply on your blog but it doesn't seem to work.I know my reply will offer you a rare chance of publicity,but,well,there's nothing I could do about that.Perhaps tha… Read More

2 comments:

  1. Tena hao ni wendawazimu maana wanategeme na kufikiri kwamba ufisadi utaendelea mille!!! La asha kila kitu kina mwisho wake na hasa suala haki mara nyingi inacheleshwa tu japokuwa lazima ipatikane. Bwana Chahali sishangai kwa hao wanakuandikia lugha chafu za kimaluhuni kwa sababu sifa ya mafisadi wote wote na hao watetezi wao ni wazuri sana kwenye divert topic. Na kuleta mada sisizokuwa na kichwa hata miguu. Angalia sasa umelazimika KUTUMIA muda, akili, hekima na utashi wako kuwajibu hawa wanyama(mafisadi na wapambe wao). Nikisema wanyama nina maana ya kuwa hawa mafisadi na wapambe wa wao kuwa wana akili tuu, na hiyo ni sifa ya mnyama pori ama wakufugwa. Binadamu hai na kamili anasifa hizi utashi, akili na hekima. HIvyo Bwana chahali husipoteze muda wako tena kuwajibu hawa wendawazimu

    ReplyDelete
  2. Asante sana bwana chahali ndo maana naona blog nyingi siku hizi huwa hawaweki comment sasa nimeelewa saabau.

    ReplyDelete

Categories

Unordered List

Sample Text

Blog Archive

Labels

Follow Us on FaceBook

Popular Posts

Recent Posts

Recent Comments

Recent Premium Themes

Your Links

Flickr

Powered by Blogger.

Blog Archive

Followers

Download

Your Links

Blogger Tricks

Popular Posts

Recent Posts

Text Widget