Haya ndio matokeo ya kumkabidhi mtu mbabaishaji kuongoza nchi.Naam,namzungumzia Rais Jakaya Kikwete.Wengi wanaomfahamu vizuri wanatambua kwanini nchi yetu inazidi kupoteza mwelekeo.Majambazi waliojivika joho la uongozi wanazidi kufilisi nchi yetu, Na sasa kila Mtanzania amebebeshwa deni la takriban shilingi laki tano kila mmoja kutokana na zigo zito la misumari la deni la ndani la taifa la shilingi 22,000,000,000,000 (TRILIONI 22). Na hilo ni deni la NDANI TU.
Wakati tunakabiliwa na mzigo huo wa deni hilo kubwa,serikali ya Kikwete imelipa takriban SHILINGI MILIONI 100 kugharamia makazi ya Naibu Waziri wa Uchukuzi Dkt CHARLES TIZEBA (Ni muhimu kujikumbusha Waziri KAMILI wa Uchukuzi ni yule anayetajwa kama kuwa mfano wa viongozi safi wachache ndani ya CCM, Dkt Harrison Mwakyembe).
Uchunguzi wa gazeti la Kiingereza la Guardian umefukua uhuni huo unaotokea katika Hoteli ya Kitalii ya New Africa jijini Dar,ambapo gharama za makazi ya Dkt Tizeba zimeendelea kuchajiwa hata pale anapokuwa nje ya jiji la Dar.
Gharama za malazi katika hoteli hiyo zinaangukia katika makundi matatu: vyumba vya kawaida dola 160 kwa usiku mmoja; vyumba vya klabu dola 180 kwa usiku mmoja; na vyumba maalumu (suites) dola 300 kwa usiku mmoja.Dkt Tizeba anaishi kwenye chumba maalumu (suite) lakini hoteli hiyo imekubali kupunguza gharama hadi dola 250 kwa usiku mmoja.
Hadi kufikia Jumamosi iliyopita (Januari 12, 2013) Naibu Waziri huyo angekuwa ameishi hotelini hapo kwa sangalau siku 247,na hivyo kufanya gharama za malazi yake hotelini hapo kufikia dola 61,750 (sawa na SHILINGI MILIONI 98.8)
Hata hivyo jumla hiyo ni ya malazi na kifungua kinywa tu ( bed and breakfast), ikimaanisha kuwa gharama za jumla zinaweza kuwa kubwa zaidi ikijumlishwa na zile za mlo,ambapo mlo mmoja (buffet) unagaharimu angalau shilinhi 21,000.
Kadhalika,kwa vile Naibu Waziri huyo ana familia,gharama hizo zinaweza kuwa kubwa zaidi.Hivi karibuni Naibu Waziri Tizeba alitembelewa na wanawe wawili walioishi hotelini hapo kwa zaidi ya wiki kwa gharama ya dola 100 kwa kila usiku.
Alipotafutwa na gazeti hilo,Dkt Tizeba ambaye ni Mbunge wa jimbo la Buchosa kupitia CCM, alishauri suala hilolielekezwe kwa mamlaka zinazohusika na makazi ya mawaziri na viongozi wengine wa umma.
"Siwezi kujipangia makazi mie mwenyewe...kuna mamlaka zenye jukumu hilo,kwahiyo tafadhali ongea nao na upate tamko rasmi.Hata hivyo,vyanzo vya gazeti hilo vimeeleza kuwa gharama za makazi ya Naibu Waziri huyo hotelini hapo zinabebwa na Ofisi ya Waziri Mkuu.
Hta hivyo,Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Paniel Lyimo alikataa kuzungumzia suala hilo,hususan haja ya kupunguza gharama kwa kumpatia Dkt Tizeba makazi ya kudumu badala ya kuishi hotelini na hivyo kuongeza gharama.
Katibu huyo Mkuu alimtaka mwandishi kumtumia ujumbe mfupi wa maneno (SMS), akidai maongezi kwenye simu hayakuwa sawia.Lakini masaa mawili baadaye,mwandishi alipokea ujumbe kutoka kwa mtu aliyedai kuwa ni Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo akisema:
"Kuhusu taarifa ulizokuwa ukisaka kutoka kwa Lyimo,Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, ningependa kukufahamisha kuwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa Uchukuzi ameshapangiwa nyumba kitambo sasa."
Hata hivyo kuna taarifa kuwa Dkt Tizeba amekataa kuhamia kwenye nyumba hiyo,ambayo awali ilikuwa ikitumiwa na mtangulizi wake, Athuman Mfutakamba. kwa madai kuwa "haiendani na hadhi yake."
Lakini alipotakliwa kutoa msimamo wake, Dkt Tizeba 'aliponda' tuhuma hizo akidai zinasambazwa na maadui zake.ambao walikuwa wakipambana na harakati za Wizara yake kuweka mambo sawa (kupambana na ufisadi).
Gazeti hilo limepata taarifa kuwa Naibu Waziri wa Fedha, Saada Mkuya, naye aliishi hotelini hapo kwa angalau miezi miwili baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo.
HII NDIO SERIKALI YA RAIS KIKWETE AMBAYO IAN DENI LA NDANI LA SHILINGI TRILIONI 22 NA DENI LA NJE (HADI KUFIKIA AGOSTI MWAKA JANA) LA DOLA BILIONI 10.35 (SHILINGI 16,050,000,000,000),YAANI ZAIDI YA SHILINGI TRILIONI 16.KWAHIYO KIMSINGI JUMLA YA DENI LA NDANI NA LA NJE NI TAKRIBAN SHILINGI TRILIONI 40 (40,000,000,000,000) AMBALO LINAMFANYA KILA MTANZANIA KUDAIWA TAKRIBAN SHILINGI MILIONI MOJA KILA MMOJA (NI WASTANI WA SHS 888,888,.89 )
LAKINI LICHA YA UZITO WA DENI HILO BADO SERIKALI YA KIKWETE HAIJALI KUMLIPIA NAIBU WAZIRI TAKRIBAN SHILINGI MILIONI 100 KWA MAKAZI YA HOTELINI (MNAZIKUMBUKA ZILE NYUMBA ZA MAWAZIRI PALE VICTORIA JIRANI NA KAMBI YA USALAMA WA TAIFA NA HOSPITALI YA KAIRUKI?)
SIJUI HALI YA NCHI YETU ITAKUWAJE HAPO 2015 KIKWETE ATAKAPOONDOKA MADARAKANI.ILA MOJA LILILO WAZI NI KUWA DENI HILI LA MATRILIONI YA SHILINGI LITAKUWA LIMEZALIANA KWA KASI PENGINE ZAIDI YA KASI YA KUZALIANA KWA MAFISADI HUKO NYUMBANI.
0 comments:
Post a Comment