Naomba niwe mkweli. Kila nikiskia Mwarabu flani anawekeza sehemu, hisia ya kwanza ni jinsi twiga na wanyama pori wetu wanavyotoroshwa na Waarabu...na sakata la Loliondo lililopelekea kifo cha mwandishi mahiri wa habari za Uchunguzi, Marehemu Stan Katabalo.
Kwa kifupi, picha iko hivi: Mwaka jana Rais Jakaya Kikwete alipokwenda huko Uarabuni, aliwahamasisha wafanyabiashara wa huko kuja kuwekleza Tanzania akidai kuwa nchi yetu ina "fursa zisizo na kikomo" (unlimited opportunities) kwa Waarab hao.
Kufuatia ziara hiyo ya JK na wito wake kwa Waarabu hao, siku chache baadaye (Januari mwaka huu) zikapatikana taarifa kuwa kundi la wafanyabiashara wa Oman likiongozwa na kampuni ya AL-HAYAT DEVELOPMENT AND INVESTMENT COMPANY wanapanga kuwekeza dola za kimarekani milioni 100 kufufua shirka la ndege la Tanzania (ATCL), na memorundum of understanding ikasaniwa kati ya ATCL na bosi wa kampuni hiyo ya Oman Sheikh Salim Al-Harthy
Hata hivyo, mwezi Juni mwaka huu, Naibu wa Mawasiliano na Uchukuzi, Dkt Charles Tizeba, aliliambia Bunge kuwa 'mwekezaji huyo wa Oman ameingia mitini' Kadhalika, Naibu Waziri huyo alieleza kuwa hakukuwa na makubaliano yoyote yaliyosainiwa kati ya 'wawekezaji' hao na ATCL
Cha kushangaza, vyombo mbalimbali vya habari huko nyumbani vimeripoti jana kuwa mtu yuleyule SHEIKH SALIM AL-HARTHY na kampuni ileile ya AL-HAYAT DEVELOPMENT DEVELOPMENT AND INVESTMENT COMPANY inatarajia kuufanyia ukarabati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, jijini Dar, kwa kutumia uwekezaji wa dola za Kimarekani milioni 100.
Hivi ndugu msomaji, hata tukiweka kando rekodi ya 'wawekezaji' wa Kiarabu katika kuhujumu uchumi wetu, inaingia akilini kweli kwa mtu yuleyule aliyeleta uzushi kuhusu uwekezaji kwenye ATCL, na kisha kuingia mitini, kukabidhiwa dhamana ya kuifanyia ukarabari aiport yetu kuu?
'Mwekezaji' huyo Mwarabu alinukuliwa na gazeti moja akida (nanukuu)
“Nimekuja kuwekeza hapa kwa kuitikia mwito wa Rais Jakaya Kikwete, amechoka sana inabidi sisi tumsaidie, ana nia nzuri ya kuhakikisha nchi hii inakuwa kiuchumi inabidi tumsaidie kuwekeza katika maeneo kama haya” alisema. Katika hatua nyingine mwekezaji huyo ametangaza kuwekeza ndege nane kwenye Shirika la Ndege la Tanzania(ATCL), mradi ambao unatarajiwa kugharimu dola za Marekani 100 milioni.
Tafadhali zinatia maneno hayo ya rangi nyekundu.
Cha kusikitisha zaidi, ni ukweli kwamba hata Waziri pekee anayeonekana kupigania haki za wanyonge, Dkt Harrison Mwakyembe, naye kaingia mkenge kwa kumsapoti Mwarabu huyo, na kunukuliwa akisema kuwa serikali imefanya kazi kubwa ya kuvutia wawekezaji hao...
0 comments:
Post a Comment