Leo ni kama vita hapa Uingereza, lakini sio vita inayohusisha majeshi bali timu za taifa za England dhidi ya Scotland, na Wales dhidi ya Jamhuri ya Ireland
Vita kubwa zaidi leo ni mpambano 'wa kisasi' kati ya England na Scotland katika Uwanja wa Wimbley. Kwa hakika nchi hizi zina uhasama mkubwa kisoka japo kama tunavyofahamu wengi, England ipo katika sayari nyingine katika anga za soka la kimataifa. Pengine tatizo kubwa la soka la Scotland ni ukweli kwamba kwa miaka mingi ligi kuu ya hapa imekuwa kati ya timu pinzani kupindukia, Celtic na Rangers zote za hapa Glasgow.
Jana kulikuwa na pambano la utangulizi kati ya Timu za Taifa za England na Scotland kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 21, na kama matokeo ya mechi hiyo yanatabiri chochote, basi Scotland leo ina kazi kubwa.Hadi mechi inamalizika, matokeo yalikuwa England 6 Scotland 0
0 comments:
Post a Comment